singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
HABARI njema zinaeleza kuwa serikali imesema bajeti ya mwaka ujao, hususan utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo, itatekelezwa kwa fedha za ndani.
Hiyo ni taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipozungumza wakati akiangalia shughuli za utendaji kazi za maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika mji wa Holili mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Katika kile kinachodhihirisha kuwa Serikali ipo makini katika hilo, Waziri Mpango alisema, makusanyo ya sasa ya Sh trilioni 1.7 kwa mwezi yanayokusanywa kwa nchi nzima, fedha zake zitaelekezwa kwa shughuli za maendeleo kwa mikoa yote nchini.
Waziri alisema si kweli kwamba Serikali ya Rais John Magufuli haihitaji msaada wa fedha kutoka nje, lakini msaada huo utahitajika kwa kiwango kidogo kuliko ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma.
Tamko hili la Serikali kupitia Waziri Mpango ni tamko la faraja na linaloleta matumaini kwa Watanzania wote kutokana na ukweli kwamba kwa miaka mingi, wananchi kupitia kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge wamekuwa wakilaani hatua ya bajeti ya Serikali kutegemea kwa kiwango kikubwa misaada ya nje.
Mkakati wa Tanzania kulenga kujiendesha bila kutegemea misaada kutoka nje ulianza miaka mingi, pamoja na kwamba mkakati huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchache wa makusanyo ya kodi na ushuru yanayodhoofisha utendaji wa serikali.
Pamoja na serikali nyingine kujitahidi kwa uwezo wao, ya Awamu ya Tano imedhihirisha kusimama kidete katika kulifanikisha hilo hasa kutokana na kauli ya Rais Magufuli kwamba Tanzania itajengwa kwa rasilimali na watu wake na si watu wa nje, na sasa kauli ya Waziri Mpango kwamba bajeti ya mwaka huu itatekelezwa kwa fedha za ndani.
Hakuna ubishi kwamba ingawa fedha za ufadhili kutoka nje zinasaidia katika kutekeleza miradi ya maendeleo, lakini zimekuwa ama zikitolewa kwa kuchelewa au zikiambatana na masharti mengi hatua ambayo imekuwa inakwamisha miradi kutekelezwa kwa wakati au wakati mwingine miradi kutotekelezwa kabisa.
Kama sehemu kubwa ya miradi nchini kote, iwe ni katika sekta ya elimu, sekta ya afya, sekta ya uchumi na biashara, sekta ya miundombinu na nyinginezo itatekelezwa kwa fedha za ndani na kutegemea fedha za nje kwa kiwango kidogo, ni wazi kwamba ufanisi utaongezeka mara dufu kwa vile kwanza miradi itajengwa kwa wakati lakini pia hakutakuwa na masharti mengi katika utekelezaji wake.
Ni kweli kama anavyorejea kusema mara kwa mara Rais Magufuli kwamba Tanzania ni nchi tajiri na hivyo hakuna sababu kwa nchi kama yetu kushindwa kupiga hatua kwa kutegemea rasilimali zake, kikubwa ni kuweka misingi imara ya kusimamia ukusanyaji na utumiaji wa mapato ya Tanzania ili fedha zinazopatikana zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.
Ni matumaini yangu kwamba, kama hilo litawezekana katika bajeti ya serikali ya mwaka huu wa fedha, utamaduni huo utaendelea kusimamiwa ipasavyo kwa miaka ijayo ya fedha na hiyo itakuwa mwanzo wa safari ya kuacha kutegemea fedha za nje kuendesha miradi ya maendeleo.
Kwa mantiki hiyo basi pamoja na kuipongeza Serikali Kuu kwa kufikia hatua hii, pia ni vyema kuwashukuru wadau wote ambao kwa njia moja au nyingine wamesaidia katika kuwezesha kuongezeka kwa makusanyo ya fedha za ndani, hatua ambayo sasa inaifanya serikali kutembea kifua mbele kuelekeza fedha hizo kwenye shughuli za maendeleo.
Nitumie fursa hii pia kuwaasa Watanzania kuunga mkono jitihada hizi za serikali kwa kujenga utamaduni wa kuona suala la ulipaji wa kodi si suala gumu au la kukimbizana, badala yake ni suala jema kwa vile linaiwezesha serikali kupata uwezo mkubwa wa kushughulikia masuala muhimu kwa mustakabali mzuri wa Taifa na ustawi wa Watanzania.