Fedha ya mtaji ninayo ila sina wazo la kufanyia kazi

Keylogger

Member
Oct 13, 2016
13
14
Vijana wengi nnaokutana nao na kuongea nao husema "Fedha ya mtaji ninayo ila wazo la biashara sina" au "Sina fedha ya mtaji ndo maana siwezi kujiajiri". Kijana katika makala hii najaribu kujibu maswali hayo na mengine yanayohusiana na kujiajiri uwe na mataji ama huna mtaji.

Mimi nita assume uko familia na maneno kama kujiajiri, ujasiliamali, biashara na mtaji. Ndugu yangu ukweli usiopingika kua kuna watu walijiajiri lakini hawafurahii au kuvuna matunda ya kile walichojiajiria, kipindi hiki na miaka kama miwili(2) kurudi nyuma yaani 2015 vijana wengi walio maliza vyuo vikuu walikua na wanatamani sana kujiajiri na kiukweli nawasifu malecturer wanaofundisha course ya ujasiriamali, lakini tatizo asilimia kubwa ya vijana wale walijiajiri katika kilimo na wengine hadi leo ambao wanamaliza ukimuuliza atakwambia "bwana mimi nataka nijiajiri kweye kilimo" na wengine kama nilivyokwambia "natamani kujiajiri lakini sina wazo".

Namna ya kupata wazo la biashara kwanza tuwekane sawa kila wazo la biashara ni zuri, usije ukafikiria kuna wazo baya la biashara hapa duniani kinachofanya mengine yaonekane bora ni utekelezaji yaani kulitendea haki lile wazo husika, bila shaka kidogo tupo sawa?. Ili upate wazo la biashara inayo kufaa kitu cha kwanza kabisa inabidi ujitambue wewe mwenyewe, ndio ujitambue yaani wewe ni nani?, umekulia mazingira gani?, unapenda vitu gani?, unaweza kufanya vitu gani? Na sio kufanya tu.

Yaani unaweza kufanya vitu gani vikakamilika kwa asilimia 90-100, mfano unaweza kulima je unaweza kulima kuanzia kuandaa shamba mpaka kuvuna? Kitu ambacho unasema unaweza ukakifanya ni lazima ukikifanya uhakikishe unakitendea haki sio unakurupuka tu.

Kijana ulie chuo pale unapokua unafanya usajiri wa mwaka wa kwanza inabidi uanze kujitambua mpaka unapomaliza hiyo miaka 3 au 4 basi unakua unajitambua sio unakua kama wale waliomaliza chuo wanachojua ni minyoo au misuko ipi ndo inawapendeza. Baada ya kujitambua sasa consider vitu viwili yaani unapenda nini? Na unaweza kufanya nini?

Basi hapa katikati ya maswali hayo ndo kuna wazo lako la biashara, ni hivi labda tuchukue kamfano ushamsikia yule jamaa pale Sinza wa kuitwa Mak, ndio makjuice yule jamaa alijiuliza mimi napenda nini yakaja majibu mengi lakini la juice nalo lipo, akajiuliza tena naweza kufanya nini kati ya vyote ninavyovipenda? Akapata jibu kua ni juice ndo anaweza akaitendea haki vizuri Mak akapata wazo la kufanya biashara ya juice, eeeh ndio juice!, unakumbuka tulisema hakuna wazo baya la biashara?

Nani alifikiria kama juice inaweza ikaleta faida kama anavyo pata Mak na ile ile makjuice? ni nan yupo Dar es Salaam hataki kwenda kunywa juice makjuice? Sasa kijana sio wewe unapenda nguo na unaweza kufanya biashala ya nguo, wewe ukakurupuka ukaenda kwenye kilimo wakati wewe umekulia mchikichini hata mmea wa mpunga huujui wewe unauonaga mchele tena sio mpunga! Dukani kwa mangi, eti kisa unataka kujiajiri unasema nimepata wazo la kilimo naenda kulima mpunga Kilombelo au Kyela.

Sawa kaka/dada umeanzisha biashara usioiweza fanya kitu kimoja ipende biashara yako, ukiipenda utajituma na ukijituma utapata matunda ya biashara yako.
 
Safi kabisa ila ujasema unaanzaje kufanya kitu unachokipenda wakati huna pesa, unaitoa wapi wengi tupate kutoka
 
Hongera mleta mada, iko vizuri.

Tukumbushane tu jamani, tunaolalamikia mitaji,
Ujasiriamali ni pamoja na kujua mtaji unatoa wapi? Na hapa ndo wengi tunashindwa kwa kdhani mtaji utajileta. Hivi unadhani kuna MTU hana mtaji? Kila MTU anaweza kupata mtaji.

Mtaji ninaomaanisha ni kutumia ulichonacho kufanya unachoweza kwa mazingira uliyomo.

Shida inakuja pale unapowaza biashara ya mtaji wa million 10 wakati hata laki 5 huna, kwa kujifariji hiyo ndo inayolipa. Utakaa miaka nenda rudi ukilalamikia mtaji na hutaupata.

Ukiona una wazo la biashara ambayo huna mtaji wake, hilo wazo si saizi yako usipoteze muda, tafuta la saizi yako kwanza na weka malengo ya muda mrefu yatakayokuwezesha kufika hapo pa swali.

Warren buffet alianza kwa kutembeza magazeti nyumba kwa nyumba akiwa kijana mdogo, baadae akauza JoJo! Angesubiri mtaji asiokuwa nao, angengoja hadi kesho.

Kuna màma mmoja clip yake iko YouTube, alianza na mtaji wa elfu 3 kwa kuuza ubuyu,
 
Back
Top Bottom