Fedha a.k.a hela

KARIA

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Posts
717
Reaction score
473
Majina ya hii kitu yanabadilika kila idara! Mfano ukiitoa sehemu ya ibada inaitwa sadaka! Endelea........!
 
kwa fisadi ten pasenti a.k.a vijisenti!!!!!!!!!!
 
1 . Ukimpa polisi rushwa !
2. Ukitoa shule ada !
3. Ukimpa mkeo matumizi
4. Ukimpa hawara
hongo!
5. Ukipeleka Tanesco/idara ya maji bili .
6. Ukimpa mfanyakazi mshahara!
 
- Ukilipa nyumba kodi !
- Ukilipa TRA ushuru!
- Ukitoa Bonus bahshish
- Ukiwapa wasiojiweza wajikwamue itaitwa zaka.
- Ukiwalipa vibarua itaitwa ujira.
 
Ukirudishiwa dukani chenji
Ukiolea mke mahari
Ukimpa mbunge posho ya kikao
Ukiuza madini mrahaba
 
Ukizipigia miti , na kilauli kwa sana, Fisadi/Mfujaji
 
Wakubwa mniacha hoi porahh! Voçes ta fudidu pah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…