Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,348
- 26,144
[h=3]Real Madrid[/h]WWWDWHuo muda wa mtanange ni kwasaa za EA?
Leo mnamo tarehe 2/3/2013 saa kumi na mbili jioni,FC Barcelona wataanza kazi yao.Baada ya kubezwa,kudharauliwa,kuonekana hawafai,kuonekana kiwango kimeporomoka na mambo yafananayo na hayo,Barcelona wataanza kuwaonesha kiwango chao halisi Real Madrid watakapopambana nao uwanjani Santiago Bernabeu.
Wakisheheni kila aina ya kipaji cha soka,Barcelona walipokea kebehi za kutosha baada ya kupigwa kumbo mara mbili na AC Milan kwa kuzabwa mabao 2-0 na baadaye kuonja shubiri ya mabao 3-1 kutoka kwa Real Madrid siku chache zilizopita. Leo wataanza kazi rasmi ya kuziba midomo ya wakejeli wao kwenye mechi ya La Liga.
Wataonesha kuwa wana plan B na hata C ya ushindi. Kila atakayekuja mbele yao,kuanzia na Real Madrid,atakumbana na kiwango cha hali ya juu cha Barcelona. Wapo watakaoishinda Barcelona na kuifurusha kwenye michuano mbalimbali.Lakini,wataishinda Barcelona ya kweli.
Muda wa kazi ni sasa!
NB: Mimi ni shabiki wa Yanga na AC Milan lakini ninayependezwa na kiwango cha Barcelona.
cc Gang Chomba Mourinho na wengineo
Mkuu Gang Chomba,Madrid hufungwa sana nyumbani kwake. Madrid inazama leo.Lakini,nina imani kubwa na Milan kusonga tar.13/2 ingawa mechi itakuwa kali na ngumuHaikufaa rangi, je itafaa chokaa?
Juzi kala thalatha kwake...unategemea leo atashinda ugenini?
Leo ndio utaijua Barcelona Mkuu king khalfanBarca lazima akae!
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mkuu Gang Chomba,Madrid hufungwa sana nyumbani kwake. Madrid inazama leo.Lakini,nina imani kubwa na Milan kusonga tar.13/2 ingawa mechi itakuwa kali na ngumu
Barca lazima akae!
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Leo mnamo tarehe 2/3/2013 saa kumi na mbili jioni,FC Barcelona wataanza kazi yao.Baada ya kubezwa,kudharauliwa,kuonekana hawafai,kuonekana kiwango kimeporomoka na mambo yafananayo na hayo,Barcelona wataanza kuwaonesha kiwango chao halisi Real Madrid watakapopambana nao uwanjani Santiago Bernabeu.
Wakisheheni kila aina ya kipaji cha soka,Barcelona walipokea kebehi za kutosha baada ya kupigwa kumbo mara mbili na AC Milan kwa kuzabwa mabao 2-0 na baadaye kuonja shubiri ya mabao 3-1 kutoka kwa Real Madrid siku chache zilizopita. Leo wataanza kazi rasmi ya kuziba midomo ya wakejeli wao kwenye mechi ya La Liga.
Wataonesha kuwa wana plan B na hata C ya ushindi. Kila atakayekuja mbele yao,kuanzia na Real Madrid,atakumbana na kiwango cha hali ya juu cha Barcelona. Wapo watakaoishinda Barcelona na kuifurusha kwenye michuano mbalimbali.Lakini,wataishinda Barcelona ya kweli.
Muda wa kazi ni sasa!
NB: Mimi ni shabiki wa Yanga na AC Milan lakini ninayependezwa na kiwango cha Barcelona.
Real Madrid watakuwa uwanjani bila Ike Casias pamoja na Angel Di Maria wakati Barcelona watamkosa Xavi Hernandes
cc Gang Chomba Mourinho na wengineo
Nipo Mkuu,nimeloa ndembendembe.Lakini,Barcelona wameonesha kiwango kizuri. Na 'wamenyimwa' penatiPetro upo????mbona umeyeyuka?
Nipo Mkuu,nimeloa ndembendembe.Lakini,Barcelona wameonesha kiwango kizuri. Na 'wamenyimwa' penati