DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,679
Bi Mwenda ni mzaliwa wa Mara Wilaya ya Bunda kijiji cha Ikwizu Nyamuswa, ni mtoto wa Mtemi Makongoro, ambaye alikuwa rafiki na ndugu wa yamini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Anasema katika maisha yake wakati yupo darasa la tano mpaka anamaliza alikuwa akiishi Ikulu jijini Dar es Salaam, na alihamishiwa Shule ya Msingi Kinondoni iliyo karibu na Mahakama ya Kinondoni. Wakati huo wenzake walikuwa wakisoma Shule ya Mwenge na kupelekwa na gari.
Fatuma Makongoro "Bi Mwenda"
Bi Mwenda, anasema alijiingiza kwenye michezo mbalimbali akiwa darasa la nne. Katika Shule ya Msingi Ikwizu alijihusisha na michezo mbalimbali kama ngoma za asili, netiboli na mbio za kijiti. "Mara nyingi nilikuwa nikijitolea, kwa kuwa michezo ilikuwa ndani ya damu," anasema Bi Mwenda. Anasema alipomaliza elimu ya msingi, kwa kuwa alikuwa hana kazi nyingine ya kufanya ndipo akaolewa, akiwa ndani ya ndoa alikuwa hajihusishi na jambo lolote zaidi ya kukaa nyumbani kama mama wa familia.
Hata hivyo anasema mwaka 1998 ndipo alipotamani tena kurudi kwenye michezo hasa na zaidi alivutiwa na uigizaji. Anasema watu ambao kwa kipindi hicho walimvutia sana katika kuigiza alikuwa Mzee Onyango, Mzee Bashir na Mwita Maranya waliokuwa wakiunda kundi la Tausi na wasanii Warid, Richirich, Bishanga ambao walikuwa wakiunda kundi la Mambo Hayo.
Anasema alitamani sana kuigiza kwa kuwa uigizaji upo ndani ya damu yake na kuongeza kuwa muda huo ndipo akakutana na kiongozi wa kundi jipya la Kaole Sanaa Group na hatimaye kujiunga na kundi hilo.
"Kipindi hicho kundi la Kaole lilikuwa na watu 14, ambao ndiyo walionipokea," anasema huku akifikiria majina ya watu hao. Bi Mwenda anasema miongoni mwa wasanii aliowakuta hapo ni Mzee Pwagu, Mzee Kipara, Mama Haambiliki na wengine, wakiwa chini ya uongozi wa Chriss Muhenga.
Kwa mara ya kwanza kundi hilo lilianza kuandaa filamu kwa mfumo wa mkanda na filamu hiyo ilijulikana kwa jina la Ndoa ya Lazima. Hata hivyo, hawakufanikiwa kuutoa mkanda huo, kwa sababu walipata nafasi ya kupeleka mchezo wao katika kituo cha televisheni cha ITV baada ya kikundi ilichokuwepo kuondolewa.
Mchezo wao wa kwanza kurushwa uliitwa Kabla Hujafa Hujaumbika ambao Bi Mwenda aliigiza kama mama yake Dk. Cheni. Igizo hilo lilimpatia umaarufu mkubwa, hasa alipoigiza kama mama mchawi, akishirikiana na muigizaji mwenzake mfupi Mlopelo kuwaloga watu na kuwageuza paka.
Anasema kwenye igizo hilo aliweza kuuva uhusika, ambao ulimpelekea kila mmoja kuwa na mawazo tofauti juu ya uhalisi na uigizaji wake wa uchawi. "Sikuwa na lengo lolote zaidi ya kuelimisha jamii kwamba matukio kama hayo yapo. Lakini waandishi na jamii ikaanza kunijadili tofauti,"anasema.
Tangu hapo Bi Mwenda anasema akaanza kupata mialiko ya filamu za nje, wakitaka aigize uhusika wa mama mchawi au mwenye roho mbaya, sababu aliweza kuuvaa uhusika huo vizuri. Anasema yeye hakuweza kukataa kwa kuwa alikuwa akiongozwa na muongozaji wa filamu pamoja na mswada wa filamu (script) yake inavyosema.
Akiwa kwenye kundi hilo alishiriki katika maigizo mbalimbali ikiwemo, Hujafa Hujaumbika, Fukuto, Jahazi, Dira, Tetemo, Tufani, Sayari, Baragumu, Gharika, Taswira na Zizimo.
Kundi hilo pia lilikuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Steven Kanumba, Vicent Kigosi ‘Ray', Muhogo Mchungu, Kipemba, Dk. Cheni, Mtunisi, Frank, Nina, Nana, Norah, Sinta, Kibakuli, Nyamayao, Max, Zembwela, Bambo, Kingwendu, Kemmy, Benny, Swebe, Chuz, Mashaka, Kissa, Johari, Mainda, Thea, Maya, Sajuki, Dino, Pembe, Senga, Tito, Mboto, Kelvin, Zawadi, Bi Kidude na wengine wengi.
Bi. Mwenda anasema katika uigizaji wake hatoweza kusahau matukio mengi yaliyomkuta ambayo yalimkatisha tamaa na kutaka kuachana na uigizaji. Anasema hii inatokana na kuuvaa uhusika na wapo wengine ambao wana matendo kama hayo, hivyo wanahisi kama wanadhalilishwa na kufichuliwa kwa kazi zao na ndiyo maana walikuwa wakimwandama.
Hali ambayo anasema ilichangiwa sana na baadhi ya vyombo vya habari vilivyokuwa vikimwandika bila ya uchunguzi na jamii ikawa ikimwangalia vibaya. Kwa mujibu wa mama huyu miongoni mwa matukio ambayo hatoyasahau ni la mwaka 2002, akiwa katika maeneo ya Kariakoo sokoni alipokwenda kununua mahitaji.
Mwaka 2005 ndipo Bi Mwenda akajiingiza kwenye uigizaji wa filamu, na alianza kwa kushiriki filamu iliyokuwa ikijulikana kama Riziki, iliyoandaliwa na Chiki Nchome akiwa kama mama yake Steven Kanumba. Aliendelea kuigiza filamu mbalimbali ambazo zipo zilizofanikiwa kutoka kama vile Johari na nyingine, na sasa anaigiza kama Mama Maria Nyerere kwenye filamu ya Steve Nyerere, iliyopewa jina la Respect Nyerere.
Anasema hadi sasa hamna maslahi makubwa kwenye filamu kwa kuwa bado wananyonywa na wasambazaji kutokana na usimamizi mbovu wa Serikali. Bi Mwenda anasema fedha kidogo wanazopata hutumika kwa ajili ya kujikimu katika maisha ya kila siku.
Anaishauri Serikali kuwaangalia na kuwajali wasanii wakongwe, hasa kutokana na wao kujitolea katika kuchangia majanga makubwa na kutoa mfano namna wasanii walivyosaidia waathirika wa mabomu Gongo la Mboto, mafuriko na mengine. Bi Mwenda anaiomba Serikali kutambua mchango wao na wasanii wanapozeeka waweze kuwekewa fungu kwenye Wizara ya Michezo na Utamaduni. Fedha ambazo zitakuja kuwasaidia kipindi ambacho wanakutwa na matatizo kama yalivyotokea kwa marehemu Saidi Fundi ‘Mzee Kipara'.
Baadhi Ya Picha Zake:
Wageni wangu, Hukumu Ya Ndoa Yangu, Bibi Yangu, Mkono wa Mungu, Binti Mfalme, Kiranga Changu, subiri Mama, Jungu la Urithi, witch Doctor, Dendeko, Lupepo Village, Detective, Chozi la Zinaa, Deni La Haki, True Love, Ukungu, From China with love, n.k
Chanzo: Bongo Cinema Online Movies.
NB : Kumbe ni Dada Wa Mtia Nia Kwa Tiketi Ya CCM Charles Makongoro Nyerere.