Fastjet washerekea Siku ya Mtoto wa Afrika

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
593
1,712
Siku ya motto wa Afrika imekuwa ikisherekewa toka mwaka1991 tarehe 16 ya mwezi wa 6. Mwaka huu 2016 siku hiiinasherekewa ikiwa na kauli mbiu ya “Migogoro ndani yaAfrika; Tulinde haki zote za watoto”

Kauli mbiu hii inakuja wakati ambapo baadhi ya nchi za Afikazimekuwa katika migogoro ya muda mrefu bila suluhisho la kudumu. Hivyo katitika kuadhimisha siku hii, Afrikainakumbushwa kwamba inawezakana kumaliza migogoro nahivyo kuwafanya watoto wa Afrika kuishi maisha salama kamawatoto waishio katika mabara mengine.

Fastjet ikiwa ni kati ya mashirika ambayo yamekuwa yakifanyakazi na jamii katika kuhakikisha watoto wanakua katikamazingira bora huku wakipata huduma zote muhimu pamoja naza kiafya, wanasheherekea siku hii kwa kutembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Moshi, Mabogini na kusikiliza mahitajiyao mbalimbali na kutoa misaada.

Afisa Uhusiano na Masoko wa Fastjet Lucy Mbogoro amesemakuwa Fastjet imekuwa Karibu sana na jamii hasa watoto, ambapo katika miaka yake mitatu toka shirika lianzishwe hapaTanzania, shirika limeweza kutoa misaada mbalimbali kwa vituokadhaa vya watoto yatima na pia limeweza kusafirishamadaktari zaidi ya 20 kuelekea vituo vyetu kwaajili ya kutoahuduma za kiafya au upasuaji kwa watoto wenye mahitajiambao walishindwa kufika kwenye hospitali zetu kubwazilizopo mijini.

Aidha Lucy aliendelea kwa kusema kuwa Fastjet inakaribishamaombi mbalimbali kutoka kwa madaktari ambao wanatarajiakwenda kutoa huduma za kiafya kwa watoto katika vituoambayo fstjet inafika, ili kuwapa huduma bora, pia shirikalitahakikisha linaendelea kushirikiana na madaktari ili kulindaafya za watoto na maisha yao kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom