Alegria do povo
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 293
- 441
Michezo imehama muda sana kutoka kwenye hali ya kuwa kitu cha kujifurahisha nacho na kuburudisha, na sasa imekuwa biashara inayohitaji uwekezaji sahihi.
Bidhaa ni soka la kuvutia la timu yako, wateja ni mashabiki. Tofauti na biashara nyingine, michezo inavutia wafanyabiashara wengine kuitumia kujitangaza. Huu ndio upekee wa biashara ya michezo ambao unaifanya kuwa zaidi ya kiwanda cha kawaida au kampuni ya kawaida.
Soka likiwa sehemu ya michezo ndilo linalotengeneza sehemu kubwa ya mchezo unaopendwa zaidi duniani. Nchi zilizoendelea zinahakikisha kuwa michezo yenye muitikio mkubwa inapewa kipaumbele.
Nchi zinazoendelea nyingi zinatakiwa kuhakikisha zinakuza sekta hii, lakini hili ikue zaidi inatakiwa zifanye uwekezaji wenye tija na wa mipango kama sekta nyingine za kiserikali. Lakini sehemu kubwa ambayo nchi kama Tanzania inatakiwa kufanya ni kuhakikisha inapata wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Hii huleta chachu ya vijana kuchukulia mchezo huu kama ajira rasmi, na kuchochea kukua kwake. Lakini hili haliwezi kufanikiwa kama kutakuwa na sintofahamu kati ya viongozi wa vilabu, viongozi wa nchi, mawakala wa wachezaji na wachezaji wenyewe.
Hawa wote lazima wazungumze lugha moja ukiachilia mbali faida ambayo kila mmoja anahitaji kuipata. Tatizo kubwa la watanzania na vyombo vyake vya habari ni kuwa tumezoea kulala upande wa kulia huku kushoto tukipaacha.
Tunashangilia ya Samata kuliko kuwaweka sawa akina Msuva. Mashabiki nao wapo tayari kumng'ang'ania Okwi kuliko kulilia Ajib akomazwe kiuchezaji wa kulipwa. Tumejawa uoga wa kifikra katika kutambua lipi ni sahihi zaidi kwetu.
Kwa miaka ya karibuni sijapata kuona miguu ya kushoto yenye thamani katika jezi za bluu za taifa hili achilia mbali vilabu vyetu. Ni wakati huu ambapo Singano hakupata lishe bora ya akili ya soka, ni kipindi hiki ambacho hata beki wa kushoto wa timu ya Taifa alikuwa Erasto Nyoni kisha Shomari Kapombe.
Nilifarijika sana kushuhudia ujio wa vijana Farid Mussa, Mwinyi Haji na Hussein Tshabalala. Lakini machozi ya damu yananitoka rohoni kwa namna ambavyo nahisi wanaelekea. Hivi ni kweli Tanzania haina watu sahihi wa kurekebisha akili hii isiyo sawa? Hivi ni sahihi kila mwandishi wa habari na makala kuwekeza kwa Samata na Ulimwengu kuliko kuwekeza akili juu ya namna ya kuwafanya vijana hawa wafike mbali?
Ipo wapi safari iliyotajwa ya Faried Mussa kwenda nje ya nchi? Vimelala wapi vyombo vya habari vilivyoripoti habari hii iliyokuwa faraja kwa watanzania? Kobe hubeba nyumba yake Muda wote, ni mzigo lakini ndiye mnyama mwenye uhakika wa usalama zaidi. Hawa Kobe wetu hata nyumba zao tumewavua.
Safari zao tunazihamua sisi, uwekezaji wa soka letu umepewa sura tofauti. Azam inataka kuishi kama Bayern Munich na sio kama FC Porto, Simba hupenda maisha ya Manchester United lakini sio Benfica na Yanga wanapuuza akili ya River Plate na wanataka mawazo ya Chelsea.
Midomo ya Watanzania imejaa Lawama kuliko matendo. Baada ya Daudi hakuna mwingine aliyejaribu tukio la kumuua aina ya Goliath. Hakuna njia fupi tena katika maisha ya kisasa kama unataka kudumu. Azam walianza vyema, waliinua vijana, wakawakuza wakawapa nafasi tukaona akina Sure boy, tukapata akina Himid Mao, tukawapenda Mudathiri. Lakini kumbe lafudhi ya nyumbani bado ipo, kabila la simba na Yanga bado linaishi na kuuza wachezaji bado ni ndoto kubwa?
Kibaiolojia mtoto haendi mbali sana na wazazi wake lakini walau jamii inawezekana ikachangia kwa kiasi kikubwa tabia na mienendo yake. Adhabu kubwa kwa soka la Tanzania ilitakiwa iwe mafanikio ya Azam FC.
Hawa wangesababisha hata MO Dewji asiililie Simba na badala yake aanzishe timu jirani kabisa na ule uwanja wao wa bunju usiojengwa kila kukicha.
Safari ya mpiganaji haijawahi kufika mwisho. Hupigana hata na kifo kilichomkaribia, inawezekana hii ikawa njia sahihi Sasa hivi ya wachezaji wetu kufika mbali. Ni dhambi kubwa kushuhudia kipaji cha Faried kikigota nchini, kisha nikapoteza Muda wangu kumsifia Samata.
Tunahitaji muda wa kuwasaidia waliopo nyuma zaidi kuliko kuwaongezea mwendo waliokwisha tangulia. Kinachouma tu ni kuwa sakata la Faried serikali na wadau wa soka wapo kimya, lakini tunasubiri atwae Ile tuzo ya Aubameyang tumpe kiwanja Bagamoyo na sanamu pale Posta wakati huo utakuta Kichuya alikosa uangalizi wa milioni 5 tu kufika Sporting Lisbon.
Unaweza kujiuliza kwanini sijawalaumu Azam au kwanini sitaki kuwalaumu. Moto ukiwaka ukimtafuta mchomaji utapoteza Mali zako, uzime kwanza.
Elimu ya dhati inatakiwa kwa vijana hawa. Utajiri wa kwanza ni uelewa wa kile unachokifanya. Nimechoka kuandika juu ya nini kifanyike, maana tumevaa Pamba makusudi kwenye masikio yetu. Pengine niseme na vijana wenyewe. Faried Mussa, tizama mkataba wako, unahitaji mwanasheria sahihi, unahitaji kutembea na saa mkononi.
Najua kabisa na ninatarajia kuwa siku chache zijazo itakuja Range Rover jirani na nyumba unayoishi Sasa, itakuja na kadi unayotakiwa kujaza jina lako tu. Ukiitamani basi safari ya Ufaransa sio halali yako, ukihitaji hata timu ya Taifa haitokuwa mahala salama kwako lakini ukiitafuta hakika utapishana na Mahrez pale Leicester City.
Taifa hili lina mwewe na kunguru wengi kuliko njiwa, tamaa yako ya gari litalokuja jirani na wewe ndio kifo chako kisoka. Ukipata Muda zungumza pia na Kichuya, kisha mng'ate sikio na Ibrahim Ajib, mkumbushe kuwa Nicasius kasema vilabu vya Tanzania na viongozi wake lafudhi yao inafanana, msitamani Range zao.
Ahsanteni.
By Nicasius Coutinho Suso