Well done Faraja Mlelwa! Wako wengi wanao-comment kiunafiki, lakini kiukweli kijana Faraja ulichokifanya ni mfano wa kuigwa kwa vijana wengi wanaodhani kuwa na elimu ya juu ni lazima upate kazi katika ngazi za juu. Hujakosea njia, cha msingi ni kukomaa. Pia ingendeza sana kama ungekuwa member wa humu ndani, ili uwe una-share experience za vikao vya mabaraza, na changamoto unazoziona kwa nia njema tu.
Waweza kutufungulia ukurasa mpya wa ulimwengu wa siasa kwa tz kama ambavyo mwingine kasema hapo juu. Pia ikawavutia vijana wengine wenye uwezo kama wako na juu zaidi kuweza kupanua uwezo wao wa kufikiri. Not necessarirly na wao wakawa madiwani wa CDM pia wanaweza kuwa wa CCM. Kwani tunahitaji ni mabadiliko na maendeleo ya kweli.
Natumaini uamuzi huu umeufanya kwa nia ya kuleta maendeleo, kila la heri Faraja Mlelwa, Mungu akuepushe na tamaa mbaya.