Faragha zetu mtandaoni

chofachogenda

Senior Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
107
Reaction score
200
FARAGHA MTANDAONI

‘’Ogopa sana Mungu na Teknolojia’’ hii ni kauli iliyowahi kutolewa na marehemu Ruge Mutahaba aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group (CMG). Msingi wa kauli hii ni kuonyesha kwamba teknolojia hasa mtandao huwa hausahau, unarekodi na unaumbua kwa maana unaweza kuweka faragha zako hadharani.

Kwa hiyo kitu unachokifanya leo kinaweza kutumika kama reference na kinaweza kupatikana kwa urahisi huko miaka ya mbeleni na kuweza kuharibu heshima yako ama kuathiri mahusiano yako na jamii hivyo chunga sana unachokifanya mtandaoni ama unachokihifadhi kwenye vifaa vyako (Devices) maana vinaweza kutumika kama silaha ya kukuangamiza huko mbeleni.

Kila mtu ana haki ya kuwa na faragha katika maisha yake hii ni kwa mujibu wa ibara ya 12 ya tamko la haki za binadamu la umoja wa mataifa

Faragha ina maana pana sana lakini msingi wake ni haki ya kuwa na usiri wa maisha yako binafsi bila kuingiliwa na mtu au taasisi yoyote ile bila ruhusa yako. Je umetafakari kuhusiana na faragha yako mtandaoni. “Faragha hasa kwa nchi za Afrika ni hakuna kabisa na wahusika wanachukulia rahisi sababu wanaona hawana cha kupoteza” Ghazar Hadid mdau wa teknolojia toka Songea.

Kila kitu ambacho tunachofanya mtandaoni ni aidha kinahifadhiwa ama kurekodiwa kwenye nyaraka za google (google archives), Seva za facebook, computer cookies (kumbukizi zinazobaki katika website au browser) au kwenye ghala za umeme (Electronic vaults) huko NSA. Kama mtu ataamua kuunganisha taarifa zetu ambazo zimesambaa mitandaoni basi angejua mengi au vitu vingi kuhusiana na sisi mfano picha zetu, Brands tunazopenda, movie tunazotazama, mlengo wetu wa kisiasa, tupo kwenye mahusiano ama la n.k.

Data mining firms kama eXelate na Intellidyn inafanya hii kazi ya kukusanya taarifa kuhusiana na tabia zetu za mtandaoni (Online behavior) na kutoa kwa washirika wake kwa sababu za kimasoko au kibiashara .

Facebook inafahamu umri wetu, jinsia zetu, miaka yetu, elimu yetu, makazi yetu, mtazamo wetu wa kisiasa na vitu ambavyo tunavyovipenda ama tusivyovipenda kwenye bidhaa mbali mbali au huduma mbali mbali hizi ni taarifa ambazo tunatoa wenyewe kwa hiyari yetu bila kulazimishwa au kulipwa.

Kwa mfano facebook wakiamua kuchukua taarifa hizo wakajumlisha na taarifa zako zingine ambazo ziko mtandaoni kama google, insta, linkedIN basi naweza kusema wanakuwa na taarifa nyingi zaidi kuhusiana na wewe inawezekana kuliko mtu wako wa karibu.

Kiukweli hata taarifa zako za google, facebook au LinkedIn zinaweza kutupa taarifa zaidi kuhusiana na wewe ambazo tunazichukulia kama binafsi ama faragha mfano mahali unapoishi, ofisi unayofanyia kazi, makadirio ya kiwango cha mshahara unacholipwa, mahusiano yako ya kimapenzi na mlengo wako wa kisiasa. Kwa hiyo kadri tunavyotumia muda mwingi kwenye mtandao ndio tuna hatari ya kuweka faragha zetu nyingi zaidi.

Ukanda wetu wa faragha unazidi kupungua sio tu tunapokuwa mtandaoni lakini pia tunapopiga simu na tunapotuma meseji zinaweza kuwa zinarekodiwa na serikali au watoa huduma ya mtandao (Internet provider) au makampuni ya simu (Mnayakumbuka ya kina Membe hapa), Lakini minara ya simu inaweza kuonyesha mahali tulipo au kurekodi movement zetu au hata baadhi ya apps zinaweza kuonyesha mahali tulipo jifikirie mtu anajua mizunguko yako ya kutwa nzima akiwa katulia sehemu na kifaa chake.

Lakini pia faragha ambayo tuliyonayo inazidi kupungua hasa pale tunapounganisha vitu tulivyonavyo na mtandao mfano nyumba zetu (cctv cameras), magari (gps tracker), saa janja, Tv kitu ambacho kinawaruhusu hackers kujua movement nzima za nyumba yako au kampuni iliyokuwekea gps au hackers kutambua mizunguko yako yote kwa siku mfano saa mbili unaenda ofisini, saa saba unarudi nyumbani kula, saa kumi na mbili unaenda gym, saa mbili unaenda bar hivyo inakuwa rahisi kupangiwa shambulio ama kutekwa n.k.

Kumbuka moja ya mbinu ambayo Osama kuishi kwa muda mrefu bila kukamatwa na wamerekani ni kuishi kisasa kwa kutumia mifumo ya kizamani mf Alikuwa anawasiliana lakini sio kwa kutumia simu wala mtandao bali alikuwa anatumia anatumia barua kitu ambacho hakiwezi kuwa hacked na teknolojia ya kisasa.

Itaendelea

CREDIT: The Internet Trap by Ashesh Mukherjee

By Benjamins
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…