Kwanza naitoe shukrani ya dhati kwa Muheshimiwa Raisi kwa kuwajali wazee wetu kwa kuwarudishia kikokotoo cha zamani kwa hilo nakupongenza maana ndio ilikuwa hoja kuu kwenye kikao chako na wadau wa mifuko ya jamii.
Turudi sasa kwenye mada ulizungumzia swala la wafanyakazi wa mikataba ya muda mfupi kwanini pesa zao zikae mpaka wafikishe miaka 55? Ulisema wapewe pesa zao wakafie mbele. Chakusikitisha mpaka leo unaenda NSSF wanakwambia hawajapata taarifa yoyote kutoka makao makuu.
Kitu ambacho nimejifunza kwanza Muheshimiwa Raisi wetu ulifanya makosa makubwa sanaa kukifanya kikao live. Maana umewachanganya watu kupita kiasi. Kwasababu kila ulicho ongea kimeonekana ni tamko. Umesema mifuko irudi kwenye kanuni zao za zamani kanuni zipi za kikokotoo au kwa ujumla na je Fao la Kujitoa lipo au halipo.
Tuseme limeshatokea hilo la kutokea hii mifuko ina wasemaje na wanalipwa mishahara kwahiyo wanasubiri mpaka tutukane huku kwenye mitandao ndio watatoa miongonzo kwa nini huwa hatujiamini kwenye taaluma zetu. Yule Mama wa watu ulimtumbua bure maana sisi huwa hatuwajibiki ipasavyo au watu niwaoga wa kufanya Kazi. Tunaiomba mifuko ya jamii itupe taarifa sahihi acheni siasa katika Maisha ya watu.
Sent using
Jamii Forums mobile app