Watanzania tunashida sana ya kupenda short cut..
Binafsi nilikuwa Mdau wa NSSF na nimeshachukua fao langu la kujito, Siwezi kukubali kwamba kuna usumbufu kwani nilipojitoa sikutoa hata senti 5 na wala sikuwahi kuonana na mtu yoyote Kiufupi niko Dar es salaam na niliposubmit document zangu tawi la kinondoni op Mlimani city waliniambia 30 days wataniwekea hela yangu bank, baadaya ya siku 22 nikapokea sms ya mtego inasema hivi, " Mr Jubilant ni mimi ........natarajia kukuwekea mafao yako bank leo...Sikuijibu hiyo sms, na kweli baada ya 24 hours nikaenda bank account yangu ilikuwa imejaa na kufurika....
Nakushauri kabla ya kujitengenezea mazingira yatakayo kusumbua na kukumalizia hilo fao lako fuata taratibu utafanikiwa bila usumbufu wowote...
Huwezi amini rafiki yangu alijitoa akatafuta short cut kweli hela ilitoka baada ya 14 days ila walimla milioni 1....Tafakari na chukua hatua