Fanya yafuatayo ukigundua kuna majambazi nje ya Nyumba yako

Silaha kubwa ya kumshinda Adui ni uwe wakwanza Kumuona adui, Hivyo usilale kama mfu, mbinu zingene ni kama ulivyoeleza na zile zitazojitokeza wakati wa tukio.

Asante
Kuna jambo moja ambalo nalo ni muhimu hasa kwa wale wenye uwezo. Unapo-design nyumba yako siku zote tilia maanani suala la security hasa hasa wezi na moto. 1. MOTO. Kwa kuwa nyumba nyingi zinawekwa milango na madirisha yenye vyuma, kufuli na vitasa vya kuzuia wezi kuingia kwa urahisi jaribu ku-design system ambayo haichukui muda mrefu kutoka ndani ya nyumba kama moto umezuka. 2. WEZI. Jaribu kujenga kitu kinachoitwa ''panic room''. Hiki ni chumba cha siri ambacho kinakuwa na mlango imara sana na matundu/system ya siri ya kuweza kuona sehemu nyingine ndani/nje ya nyumba. Mlango wake unatakiwa uwe imara kiasi ambacho hata kama wezi wamefanikiwa kuvunja na kuingia ndani lakini itawawia vigumu kuuvunja. Unapokimbilia ndani ya hiki chumba hakikisha una silaha na mawasiano. Matundu utayatumia kuwatungua wezi mmoja mmoja!
 
Sishauri sana nyumba kuweka milango ya chuma ajili ya kuimarisha ulinzi..

Wakati mwingine ni hatari sana hasa ikitokea ajali ya moto,rejea ajali ya moto iliyotokea Mwanza ,mwaka 1995 ikihusisha nyumba mmoja maeneo ya Bugando iliyokuwa inamilikiwa na mhandisi wa Jiji la Mwanza wakati huo Manispaa..

Iliyopelekea kupoteza watu zaidi ya 9 wa familia husika ..
Kwa sasa suala la usalama ni vizuri kuweka kamera za usalama ili kuwabaini Majambazi na watu wowote wabaya.
 
Mkuu tunaongezea security camera getini na kwenye milango yote ya kutokea,Pia bado kufuga mbwa ni mlinzi wa kuaminika
 
Asnten
 
Hivi namba ya polisi ya dharura ni ipi na inafanya kazi? Nikiwapigia watakuja on time?
 
Mkuu asante kwa elimu uliyoitoa. Lakini ni vema wadau hapa jamvini wakafahamu kuwa majambazi wa siku hizi wako connected na mtu anayekufahamu vizuri. Hawavamii nyumba au ofisi yeyote bila kuwa na mchongo. Na mara nyingi anayewachorea ramani ni mtu wako wa karibu. Hivyo ni vema kuchukua tahadhari na watu wetu wa karibu. Usipende kumuamini kila mtu/rafiki na kuweka mambo yako wazi kwake.
 
Wazo zuri ila inategemea na aina ya vitasa pia maana kuna vitasa vingine funguo inatakiwa iwepo kweny mlango ili mtu mwingine asiweze kuingiza funguo na kufungua akiwa nje
 
Usiombe ukutane na tukio la kuvamiwa na majambazi, ni noma.
Hao uliwazungumzia mleta mada ni wale wa kizamani. Wa sikuhizi wakijua kuwa wanachokitaka toka kwako kipo basi lazima utatoa tu. Hata ufunge mlango na kitu wanabomoa ukuta kwa kutumia hata baruti.

Majambazi wa sasa si wa mchezo. Wanavamia mahali kuna pesa za kutosha. Ref matukio ya uvamizi kwenye mabenki na maduka ya kubadilsha fedha. Hawajali kama kuna ulinzi au makamera wanachotaka wanachukua.

Mleta mada jipange...
 
Hii imekaa vizuri ila majambazi ya siku hizi pamoja na kwamba mengi yanayokamatwa yana muonekano mzuri (wakiungwana) lakini yana roho mbaya kiasi kwamba yakikukosa yanaweza kuamua hata kuchoma nyumba tofauti na majambazi ya zamani yana sura nzito lakini yakishindwa kuingia yanasepa ama yakifanikiwa na ukaonesha ushirikiano hayakuigi hata panga (yatachukua yalichofuata na kuondoka zao)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…