Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,963
- 3,675
Je, umedondosha simu yako
kwenye maji au imeingiwa maji?.
Usipate tabu, Ukichukua hatua za
haraka unaweza ukaiokoa
isiharibike.
Hatua ya kwanza kabisa itoe
kwenye maji haraka iwezekanavyo
kwani inavyozidi kukaa kwenye
maji ndivyo maji yanazidi kuingia
na kusambaa sehemu mbalimbali
za simu. Ukishaitoa kwenye maji
usifanye yafuatayo.
Usiiwashe
Usibonyeze button yoyote
Usiitikise au kuipigapiga
kwenye kiganja kwani hii
inaweza kusambaza maji zaidi.
Usiipulize kwani unaweza
kusambaza maji zaidi.
Usiiweke sehemu yoyote yenye
joto kama vile kuianika juani,
kuiweka kwenye dryer au
microwaving.
Fanya yafuatayo;
1. Izime kwa kutoa betri ili kuzuia
shoti.
2. Toa kava, line (SIM card) na
memory card.
3. Tumia kitambaa au taulo yenye
uwezo wa kunyonya maji.
Epuka kukausha kwa kufuta
kwani unaweza kusambaza
maji zaidi.
4. Zika simu yako kwenye mchele
(sio wali). Mchele una uwezo
mkubwa sana wa kunyonya
maji nah ii ni njia inayotumika
sana kukausha simu au
tablets. Kama una uwezo,
unaweza kutumia pochi
maalumu za kukaushia simu.
5. Iache simu yako kwenye mchele
au pochi kwa siku nzima au hata
siku mbili. Usiwe na haraka ya
kuiwasha kutaka kujua kama ni
nzima au la kwani kwa kufanya
hivyo unaweza kuharibu zaidi.
Tafuta simu nyingine utakayoweza
kutumia kwa muda.
6. Baada ya huo muda kupita,
unaweza kuitoa simu yako kisha
weka betri na iwashe.
7. Kama simu yako itawaka na
kufanya kazi kama kawaida,
utatakiwa kuendelea kuichunguza
simu yako ili kubaini kama kuna
mabadiliko yoyote. Unaweza
ukaplay muziki ili kujua kama
spika ziko sawa au unaweza
kumpigia mtu kujua kama mike iko
sawa, au unaweza kujaribu kupiga
picha ili kujua kama kamera iko
sawa. Spika, mike na kamera ya
simu ni vitu ambavyo huharibika
kwa haraka sana vinapoingiliwa
maji.
8.Kama simu yako haitawaka,
jaribu kuichaji, kama haichaji betri
inaweza kuwa imeharibika hivyo
jaribu betri nyingine. Kama bado
haiwaki , hapo sasa ndio unaweza
kuipeleka kwa fundi simu
unayemuamini (professional).
Kumbuka
Epuka kutembea na simu/au
kuwa makini unapoenda
sehemu za kuogelea, bafuni,
unapokuwa unafua au kuosha
vyombo au sehemu yoyote
yenye maji.
Simu inapoingiwa maji epuka
kuifungua (kama wewe sio
fundi) bila kufuata hatua
nilizoeleza kwani kwa kufanya
hivyo unaweza kuongeza
ukubwa wa tatizo.