Issue hapa sio kufanya biashara. Hawa jamaa wanapitisha makontena kwa Tsh 1,500,000 contena la nguo. Huko china wanakwambia ukileta mzigo wanakuchaji kwa cbm na hawakupi risiti ya aina yoyote ukikamatwa na huo mzigo ni shauri yako.
Kuna Maneja mmoja wa pale longroom anaitwa kahise aliondolewa kwasababu alikamata contena lao. Maofisa wote wa forodha wanamjua na anatumia kampuni inayoitwa Silent Ocean pale china wateja wote wa kariakoo wanaijua. Yaani ni wahujumu uchumi namba moja na kama wewe unafanya biashara na kulipa kodi basi ujue huwezi kushindana na hawa jamaa na utafilisika maana mzigo wako umelipia ushuru full wao hawajalipia hata robo utashindanaje nao kwa bei.
Kwa lugha ya kuwaonea huruma tuwaite majambazi tusiwaite mafisadi maana wanaiba kodi za serekali na kodi za wafanyabiashara wenzao.