Poleni na kazi za siku nzima wana JF, leo naomba nizungumzie familia bora.
Kwanza lazima iwe na utii na nidhamu kati ya wanandoa, hii itasadia kueshimiana na kujishusha miongoni mwao ili kuondoa tofauti pale migogoro inapotokea.
Pili iingozwe katika misingi ya imani, kimusingi imani ya dini inasaidia sana katika familia zetu, kwani imani ya dini inasisitiza amni, upendo, unyenyekevu na mgawanyo wa wajibu katika familia, rejea familia ya Bwana Yesu. Mimi niko katika ndoa kwa miaka 6 sasa, nguzo hii imenisaidia sana.
Mwisho nizungumzie tofauti ya kipato (mali) na elimu, hapo ndio kuna tatizo kubwa kwa tulio kwenye ndoa. Ikumbukwe kuwa tofauti ya mali au elimu siyo kigezo cha watu kufunga ndoa au kunyanyasana au kusalitiana.
Kumbuka afanyae hivyo ni dhambi kwani ndoa au familia ipo tu katika hali zote kupata au kukoswa, kikubwa ni amani na siyo mali au tofauti ya vipato au elimu.
Mungu atubariki, tudumishe amani na upendo katika familia zetu.