Je, unawahi kujiuliza nini hutokea pale taifa linaposhindwa kutekeleza wajibu wake kwa wananchi wake? Katika lugha ya kisiasa, hali hiyo huitwa “failed state” yaani, nchi iliyoshindwa kufanya kazi kama taifa. Sio lazima vita vipige, bali kuna dalili kadhaa zinazotufundisha kwamba mambo si shwari.
Serikali kushindwa kudhibiti maeneo yake: Maeneo yanatawaliwa na wahalifu, magenge au wanamgambo badala ya serikali halali. Ukiona serikali haina sauti baadhi ya maeneo, ujue hali si nzuri.
Usalama wa raia kuwa mashakani: Ghasia, utekaji, mauaji au hofu ya mashambulizi ya kila mara. Wananchi wanapoishi kwa woga kila siku, hiyo ni dalili mbaya.
Huduma za msingi kudorora au kutoweka kabisa: Shule hazina walimu, hospitali hazina dawa, maji safi ni ndoto, miundombinu ni ya aibu. Hii ni alama kuwa mfumo unayeyuka.
Uongozi usio na uhalali wala uwakilishi: Iwapo watawala hawachaguliwi kwa njia huru au hutawala kwa mabavu, basi wananchi hawana sauti. Uongozi wa mabavu ni ishara ya kushindwa.
Rushwa, ufisadi, na kuporomoka kwa taasisi: Taasisi haziwajibiki kwa umma. Mambo yanaendeshwa kwa rushwa, undugu, au ukabila. Sheria zinakuwa za matajiri na wakubwa tu.
Uchumi kuyumba na wananchi kuzama kwenye umaskini: Bei kupanda, ajira kupungua, mishahara kuchelewa, biashara kufa. Watu wanapoteza matumaini ya maisha bora.
Migogoro ya kikabila, kidini au kisiasa isiyodhibitiwa: Pale jamii inapotengana kwa chuki za asili, na hakuna jitihada za kweli za kuleta mshikamano, taifa hupasuka vipande vipande.
Wimbi la wakimbizi au watu kukimbia nchi yao wenyewe: Unapoona watu wanakimbilia nchi jirani au kujiuza utumwani ili tu waishi, ujue wamekata tamaa kabisa na taifa lao.
Kukandamizwa kwa uhuru wa kujieleza: Vyombo vya habari vinaponyamazishwa, wanaharakati kufungwa au kupotea, na sauti ya umma kufutwa, hiyo ni red flag.
Wananchi kukata tamaa kabisa: Watu wakisema, “Hii nchi haina tena tumaini,” au “Serikali haijali,” basi taifa limeanza kuparaganyika.
Hatuwezi kusubiri tufikie mahali pa vita ndipo tuanze kusema “nchi imefeli.” Mambo haya huanza taratibu, kwa ukimya, kwa mazoea, kwa uzembe. Viashiria hivi vinaweza kujitokeza taratibu au ghafla. Kadri vinavyoongezeka, ndivyo nchi inavyoyumba kuelekea kuwa “failed state”. Hata nchi yenye amani leo inaweza kufikia hatua hiyo ikiwa haitashughulikia kwa haraka changamoto hizi.