Mto_Ngono
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 686
- 589
Niaje Wadau,
Nataka kutoa somo fupi sana.
Tanzania tunazo rasilimali nyingi sana na tunamshukuru Mola kwa utajiri huu. Unaweza kufaidika moja kwa moja (direct) au kwa namna nyingine isiyo ya moja kwa moja (indirect). Leo ntaangazia katika upande wa madini na ninaposema direct namaanisha ushiriki wa moja kwa moja katika kuchimba, kuchakata na kuuza ambayo mara nyingi hufanywa na kampuni za uchimbaji wa madini kama ilivyo Ashanti, Acacia na nyingine nyingi; indirect humaanisha uwekezaji katika kampuni hizi najua unaweza kujiuliza unawekeza vipi katika kampuni kubwa kama hizi zinazojishughulisha na madini! najua pia unaweza kuwa na mawazo ya kwamba mtaji mkubwa sana unahitajika katika kuwekeza ambayo si kweli.
Hapa nitaangazia uwekezaji katika namna ya hisa. Kampuni kubwa za madini zinatakiwa kuorodhesha hisa zake katika soko la hisa (DSE) ili kuruhusu watu mbalimbali kununua hisa hizo kama ilivyo katika kampuni za simu kwa sasa. Kwa kununua hisa hizo waweza kufaidika na gawio litokalo kwenye kampuni husika. Wewe haushiriki kufanya kazi katika kampuni hiyo lakini kwa kuwekeza kwako katika hisa inakufanya uendelee kula faida kupitia gawio. Kwa sasa zipo kampuni zinazoshughulika na madini ambazo zimeorodhesha katika soko la hisa kwa mfano Acacia etc. Chukua hatua sasa kwa kununua hisa ili ufaidike kupitia kampuni hizo kwa kuwekeza kwa namna nilivyoieleza hapo juu. Kwa hiyo wao watapata faida kupitia madini hayo nawe pia utapa faida indirect ila ukitaka kula direct ni vyema kujikusanya na uingie katika biashara hiyo ya madini.
[kula indirect kupitia madini]
Au we waonaje!!!