Faida za unywaji wa maziwa

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Unywaji wa maziwa mtindi husaidia kuboresha afya ya mwili na kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini. Kaimu Mkurugenzi, ldara ya Sayansi ya Chakula ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TENC), Dk Elifatio Towo anavitaja virutubishi vilivyomo kwenye maziwa kuwa ni utomwili, kabohaidreti, mafuta , madini na vitamini.

Dk Towo anasema maziwa ni mojawapo ya vyakula vichache ambavyo ni mlo kamili na hiyo ni kwa sababu ya ubora wake wa virutubishi vilivyomo. Anasema maziwa yaliyochachushwa (mtindi) yanakuwa yameongezewa bakteria wazuri.

"Bakteria hawa wanasaidia kubadilisha sukari iliyoko kwenye maziwa halisi kuwa kwenye hali ya uchachu (asidi)," anasema Dk Towo. Mtaalamu huyo anasema maziwa yaliyochachushwa ni miongoni mwa vyakula bora na muhimu katika afya ya binadamu kwa sababu ya kuwa na virutubishi vingi ambavyo vina faida katika mwili wa binadamu. Anasema mtindi pia una vitamini Riboflavin (vitamin B2), na vitamin B12.

Dk Towo anasema wakati wa uchachushaji kuna vichocheo vingine vinavyojulikana kama antioksidants, hivi vinavyokinga mwili dhidi ya magonjwa ya kuharisha na aina mbalimbali za saratani.
milk.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom