Faida za Ualimu wa special needs education

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,104
Reaction score
1,924
Shule za watoto wenye mahitaji maalum Tanzania ni nyingi, ila zina uhaba mkubwa wa waalimu wabobezi. Zifuatazo ni faida za kuwa mwalimu wa special needs education:-

1. Ajira niyakufikia, ie zipo njenje

2.Vipindi mwisho ni saa 6 mchana, unaendelea na shughuri zako

3.Vipindi ni simple na walimu wanajaliwa vizuri na uongozi

Kama wewe ni mwalimu unataka kujiendeleza, kama wewe ni form 6 ama form 4, usiende vyuo vya arts kipindi hiki, nenda ualimu wa vipaji maalumu!!
Vyuo vipo vingi tu,ikiwemo Patandi-Arusha
 
Nadhani hujui kama maisha hayana formula,,,, unachokiona leo kina soko kesho kinabumaaa huwezi amini....... endelea kujipa moyoo tuuu
 
Acha kupotosha watu humu.Sasa hivi watu wapo kibao walimaliza hizo shahada za elimu maalumu na bado wapo kitaa wanaangaika ajira hakuna.

Hiyo kozi ilikua na soko sana kipindi cha Jk ila kwa sasa haina soko sana kama unavyosema labda kwa walemavu wenyewe waliosomea hiyo kozi kwa sababu wao wapo wachache especial upande wa viziwi wale waliosomea hiyo kozi then wanaenda kuwafundisha wenzao wanaelewana fresh sana kuliko sisi.

Unaambiwa sasa hivi wanaangalia matatizo haya kwao;
  • Mitaala isiyo rafiki kwao
  • Uzingatiwaji wa lugha ya alama kwa viziwi(Wale walimu wanaoendelea sasa wanapatiwa mafunzo ya lugha ya alama mara kwa mara mashuleni mwao)
  • Sera bora ya elimu kwa walemavu
  • Ma role models yaaani walemavu wenyewe wawa inspire wenzao mashuleni nk

Sasa hivi tunashuhudia hao walimu wa elimu maalum wanashushwa shule za msingi tena za kawaida sasa soko lipo wapi?
Kumbuka soko kubwa la walimu wa elimu maalum ni shule za serikali kwa sababu serikali ndiyo inamiliki shule au kuingia ubia na shule za kanisa zinazochukua wanafunzi walemavu ukiangalia shule nyingi za makanisa zenye watoto wenye ulemavu walimu karibia wote wanalipwa na serikali.Ukianzisha shule binafsi za walemavu bila kuingia ubia na serikali nani atawalipa walimu?Wazazi wenye watoto walemavu hawapo tayari kutoa mamilion ya hela kuwasomesha shule binafsi pia uchache wa walemavu unachangia watu kuogopa kuanzisha shule binafsi za walemavu wataingia hasara.

Madhara ya kusomea kozi hii ni kwamba usipoiva vizuri kwenye maeneo haya hearing impairment,Cogntive disability,Visual impairment and Speech impairment unakumbana na ugumu wa kupata kazi kwenye NGOs nyingi.

Kuchukua somo moja la kufundishia nalo ni tatizo kwa sababu mtu unashindwa kupata kazi kwenye shule za kawaida ambapo wanahitaji Mwalimu mwenye masomo mawili ya kufundishia eg BIOLOGY/CHEMISTRY wakati wale wa special education wanachukua BIOLOGY/Hearing impairment au Visual impairment nk yaani somo moja la kufundishia na lingine la aina ya ulemavu so shule nyingi za kawaida binafsi zinaogopa kumuajiri Mwl wa aina hiyo kwa sababu gharama atafundisha somo 1.

Sasa hivi kuna vyuo vikuu kama 3 ambavyo ni SEKOMU,UDOM,AMUCTA-TABORA pia UDSM wameanzisha kozi ya lugha ya alama ya Tanzania pale kwenye idara ya isimu na lugha za kigeni wakati PATANDI wao wanawa-train wale walimu wa kawaida wa shule za msingi wenye vyeti ili waweze kuwafundisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu.Ukitaka kujiunga na PATANDI lazima uwe Mwl uliyefanya kazi angalau miaka 2 kwenye shule yoyote ya kawaida thenn ndo unaomba kujiunga huko.

Miaka ya nyuma hiyo kozi ilikua na soko sana kwa sababu vyuo vilikua vichache sana na watu walikuwa hawapendi kusomea hiyo kozi hasa vijana form 6 fresh badala yake waliachiwa wazee tu so ikaifanya iwe na mahitaji makubwa sana ila kwa sasa graduates wapo tele kitaa tena wana shahada zao za elimu maalumu wanawait ajira.Pia issue za uongozi zilikua miaka ile kwa sababu walihitajika maafisa elimu maalum.

Labda usome halafu uanzishe NGOs yako ila sikushauri sana kwa sababu sasa hivi zipo nyingi sana ila ni utaalamu wako tu so kila kitu na wakati wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…