Faida za kumtoa "OUT" umpendaye

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,446
Reaction score
7,990
Wapo baadhi ya wanandoa wengi wao ukiwauliza mara ya mwisho walitoka out lini na wenza wao? huenda majibu yao yakakunyima raha kabisa, huenda majibu yao yakakunyima raha kwa sababu wapo wataokwambia hawajawahi kabisa kufanya hivyo, lakini wapo baadhi watakaokwambia mara ya mwisho walifanya hivyo walivyokuwa kwenye hatua ya uchumba pamoja na majibu mengine kama hayo.

Ila ukweli ni kwamba moja kati ya vitu vinavyoongeza radha mwanana katika mahusiano ya ndoa ni pamoja na kutoka matembezi na yule umpendaye (out). Kutoka matembezi (out) kuna faida lukuki katika mahusiano miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuonesha unamjali na kumheshimu sana yule umpendaye.

Kutoka matembezi huenda kwako ukaona kama ni kitu cha kipuuzi sana, ila usichojua ni kuwa kutoka out wakati mwingine kunasaidia sana kumpa uhuru yule uliyenaye kwenye mahusiano ya ndoa kuweza kuongea hata yale ambayo mtu huyo mara nyingi alikuwa haongei. Nadhani kwa wale wenye tabia hii ya kutoka out na wenza wao watakubalina na ukweli huo.

Kutoka out husaidia sana kwenye mahusiano ya ndoa kwa sababu wakati mwingine huenda huko out mkapanga mipango ambayo ni mizuri itakayowasiaidia kuweza kupata maendeleo yenu binafsi na yenye kuleta mafanikio makubwa sana maishani mwenu.

Enyi watu wote mlioko kwenye mahusiano ya ndoa jifunzeni kutoka matembezi (out ) maana kuna faida sana. Usiwe ni mtu ambaye upo bize kwa siku zote 365 kwa mwaka bali, jitahidi kutenga siku kadhaaa kati hizo kwa ajili ya kufanya matembezi na yule umpendaye.
 
Out ya nini, mwanamke akishazaa havutii tena tumbo kubwa, havai nguo za mitego hapana akae nyumbani alee watoto ntatoka na washkaji na wachuchu wenye matumbo flat

ikitokea nimemtoa tutatembea kama Bata mimi mbele yeye atanifata nyuma...alisikika mkulungwa akiongea peke yake.
 
Hapa michepuko itachukua nafasi
 
Kama ndivyo unavyofanyiwa pole sana.
Hilo tumbo ndilo lililompa heshima huyo Mwanaume ya kuitwa baba flani.

Huko kutokuvutia wenda ni jitahada zake za kutengeneza mazingira ya watoto wenu kuvutia na ww mwanaume ukasahau kumsaidia kurecover ili avutie tena.

Hizo nguo za mitego asizozivaa sahiv ni kwa sababu ya watoto wenu, anajaribu kiwafundisha kuwa miili yao ni ya thamani sana wajitaidi kuisitiri. Mara moja moja jaribu kumnunulia hizo nguo za mitego uone kama hatokuvalia mkiwa chumbani.
 
ahsante kwa pole nimezipokea....
 
Ni ulimbukeni tu mwanamke muda wote ni mzuri hata akizaaa
 
Aisee!

Huyo mkulungwa kwenye chama chetu tunaomba ajiuzulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…