Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 724
- 249
Kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya uamuzi wa “sijui Bunge au Serikali” kutoruhusu urushaji wa moja kwa moja wa matangazo ya televisheni ya mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma. Wengi wamelaani na wachache wameunga mkono hatua hiyo, kila upande ukiwa na sababu zake.
Kadhalika, kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya uamuzi wa rais Magufuli kutangaza kuahirisha sherehe za kitaifa (Uhuru wa Tanganyika, Siku ya Ukimwi, na Muungano wa Tanzania) kwa kile kilichotajwa kama kubana matumizi na pia kuagiza pesa zilizopangwa zitumike kwa matumizi mengine. Hapa wengi wameunga mkono na wachache wamelaani hatua hiyo.
Hoja ambayo haijaibuliwa na ambayo mimi naiona kama faida ya “kuhariri bunge” na “kuahirisha sherehe” ni JITIHADA ZA KUREJESHA na KUJENGA UPYA UMOJA WA KITAIFA.
Tukianzia kipindi cha Bunge lililopita, tukaja wakati wa mchakato wa kuandika Katiba Mpya (midahalo na mijadala ya wananchi), na hasa wakati wa Bunge Maalum la Katiba, na tukafikia wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu (Agosti-Novemba), Watanzania wengi, kama taifa tuligawanyika sana kisiasa.
Mgawanyiko huu ulifikia kilele cha uadui na hata baadhi ya wananchi kupigana hadharani. Tumeshuhudia viongozi wetu, wawakilishi wetu wakilumbana na hata kuitana majina yasiyo ya staha ndani ya bunge linalopaswa kuwa mahali pa heshima kubwa. Ilifika mahali ikabidi askari waingie ndani ya ukumbi wa bunge kuwatoa baadhi ya wabunge nje. Kwenye baadhi ya halmashauri (Tanga na Kilombero) madiwani nao nusura wapigane. Huko Zanzibar wananchi wameanza kususiana kwenye masuala ya kijamii kutokana na tofauti za kisiasa.
Kungekuwa na furaha gani kuadhimisha sherehe ya Uhuru wa Tanganyika wakati uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa bado haujafanyika na kulikuwa na mvutano mkubwa juu ya uhalali wa marudio ya uchaguzi? Zanzibar wala ilikuwa “haina rais”. Sidhani hata viongozi wa vyama vya “ushindani” wangehudhuria sherehe hizo.
Kuna haja gani ya kuadhimisha sherehe za Muungano ilhali mpaka sasa Zanzibar hapajapoa sawasawa?
Mpaka sasa baadhi ya vyama vya siasa havijakubali kuwa vilishindwa uchaguzi mkuu uliopita, na bila shaka vingependa kutumia mkutano wa bunge kutetea hoja zao. Vingependa kutumia jukwaa la bunge kukashifu chama kilichoshinda. Wale walioshinda nao watataka kujibu mapigo. Na namna rahisi ya kupata wasikilizaji na kuungwa mkono ni kwa kuonekana kwenye televisheni.
Kwa uzoefu wa vikao vya bunge vilivyopita hatuoni hatari ya wabunge na wanasiasa wetu kuendelea kutugawa sisi wananchi?
Kama tunadhani ni lazima bunge lionyeshwe laivu lote, basi nashauri Bunge litunge kanuni kadhaa zitakazohakikisha wachangiaji hawatoi kauli au kufanya matendo yenye kuendelea kutugawa wananchi. Tusiseme eti kwa vile Hong Kong au Korea Kusini au India wabunge huwa wanapigana basi na sisi turuhusu hali hiyo tukidhani kuwa kila la nje ni zuri au ustaarabu.
Hata humu jukwaani si wengi wenye uvumilivu wa kisiasa!