Faida za juisi za matunda kiafya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,814
34,196
FAIDA ZA JUISI.jpg
FAIDA ZA MATUNDA JUISI KIAFYA.jpg

FAIDA ZA JUISI ZA MATUNDA KIAFYA

JUISI YA MCHANGANYIKO WA NDIZI NA CHUNGWA: Chukua ndizi
kama mbili au zinazotosha kutengenezea kiasi cha juisi upendacho na chungwa au machungwa. Kisha osha vizuri matunda yako na

menya ndizi halafu zikate vipande vidogo. Ndizi ninazozungumzia
hapa ni ndizi mbivu na si vinginevyo. Weka vipande vya ndizi zako kwenye blenda kisha saga upate juisi yako. Chukua chungwa au

machungwa na kamua ili upate juisi yake kisha changanya na saga
kwa pamoja ili upate mchanganyiko ulio sahihi. Chukua maji safi na salama kama glasi moja kisha changanya. Unaweza kuweka sukari

au asali kidogo ili kuleta ladha. Unaweza kuweka mchanganyiko wa juisi yako kwenye friji ili ipate ubaridi kidogo na iwe tayari kwa matumizi.

FAIDA ZA JUISI HII KIAFYA: Kumbuka tunda la ndizi lina madini ya potasiam na sodiam kidogo. Madini haya yana vitamini B na pia kuna magneziam ndani yake. Virutubisho vilivyomo vinasaidia

mzunguko wa damu kwenye arteri kuwa mzuri. Pia katika
mchanganyiko huu wa juisi kuna vitamini C na A.

Aidha juisi hii inasaidia kutunza na kuufanya moyo ufanye kazi yake vizuri na ina uwezo wa kuzuia shinikizo la damu (High Blood Pressure).

JUISI YA MCHANGANYIKO WA APPLE NA PARACHICHI: Chukua maparachichi na apple zinazotosha kutengeneza kiasi cha juisi

yako. Osha vizuri matunda yako kwa usalama wa afya yako kisha
menya na ondoa mbegu. Kata vipande vinavyoweza kusagika.
Weka kwenye sahani au bakuli kisha saga kwenye blenda ili upate

mchanganyiko sahihi. Unaweza kuchanganya na asali vijiko vikubwa vya chakula viwili au vitatu na maziwa kidogo. Weka kwenye friji ipate ubaridi kidogo.

FAIDA ZAKE KIAFYA: Virutubisho vilivyomo ndani ya matunda haya vina uwezo mkubwa wa kupunguza cholesterol kwenye damu hivyo kupunguza uwezekano mkubwa wa mtumiaji wa juisi hii kupatwa na magonjwa ya arteri/kuziba kwa mishipa ya damu. Aidha
mchanganyiko huu unazuia magonjwa kama anaemia (ukosefu wa

madini ya chuma na upungufu wa damu mwilini)
, kwani parachichi na apple vina viwango vikubwa vya madini ya chuma. Pia huzuia kansa ya colon.

Kumbuka matumizi ya juisi hizi ni ya mara kwa mara. Unapokunywa juisi kama hizi mara moja kwa mwezi haitokusaidia kitu. Pangilia juisi hizi kama sehemu ya mlo wako wa kila siku.

JUISI YA KAROTI NA APPLE: Chukua kiasi cha karoti na apple kinachotosha kutengeneza juisi kwa kiasi ulichokusudia. Usikose kipande cha limao kiasi cha nusu. Anza kuandaa juisi yako kwa

kuosha na kumenya karoti na apple kisha katakata katika vipande vidogo vinavyoweza kusagika kirahisi kwenye blenda.
Saga mchanganyiko wako ili upate juisi. Baada ya kupata mchanganyiko wa juisi yako kamulia limao kwa ajili ya kuongeza

ladha. Unaweza kuiweka kwenye friji ili ipate ubaridi kidogo na tayari kwa kuinywa. Siyo lazima kuongeza sukari kwenye juisi kwani matunda yana sukari asilia.

JUISI YA KAROTI NA APPLE: ina uwezo wa kutunza ngozi kwani tunda la apple linaondoa uchafu kwenye ngozi na karoti nayo kwa kutumia kirutubisho cha beta-karotini chenye uwezo wa
kutengeneza Vitamin A hulinda na kurejesha uhai katika ngozi

ambapo inaifanya ionekane nyororo. Pia juisi hii husafisha tumbo na kuondoa uchafu tumboni. Aidha juisi hii inafanya ini lifanye kazi yake vizuri kwa kulainisha nyongo na kusaidia kuondoa uchafu.

JUISI YA VIAZI MVIRINGO: Chukua viazi mviringo vinavyotosha kwa juisi. Andaa kwa kuviosha na kumenya kisha katakata vipande vidogo kwa ajili ya kuvisaga. Saga ili upate juisi uliyoikusudia.

JUISI YA VIAZI MVIRINGO: inatumika kama dawa ya kuondoa au kupunguza asidi au gesi tumboni. Juisi ya viazi mviringo inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya figo, kisukari, unene au kitambi.

JUISI YA MBOGAMBOGA: Juisi hii ina mchanganyiko wa mbogamboga kam vile karoti, nyanya na matango. Maandalizi yake ni kam juisi nyingine. Anza kwa kuosha kisha kumenya na

kukatakata vipande. Saga mchanganyiko huo kwenye blenda ili upate juisi uliyoikusudia. Unaweza kuweka kwenye friji ili ipate ubaridi kidogo.

JUISI hii inasadaidia kuzuia kansa hasa ile ya kwenye mfumo wa kumeng`enya chakula, kukinga mapafu na artery. Pia inasaidia kuimarisha kinga.

JUISI YA TIKITI MAJI: Chukua tikiti maji (watermelon) na osha kisha likate vipande na chukua nyama yake ya ndani ambayo utaisaga na kupata juisi.

JUISI YA TIKITI MAJI ina uwezo wa kusafisha figo pamoja na njia ya mkojo. Inazuia unene kwa kuwa na kiwango kidogo cha calories.

Kwa aina hizo chache za juisi unaweza kujua umuhimu wa juisi za matunda na mbogamboga tunazotumia. Kwa leo ninaishia hapo na siku zijazo nitaendelea kukupatia ufahamu kwa aina zingine za juisi pamoja na kazi zake.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169

Attachments

  • JUISI MBALI MBALI.jpg
    JUISI MBALI MBALI.jpg
    9.4 KB · Views: 308
Kesho nitaaanza na hii ya chungwa na ndizi
Ukiwa unakunywa juisi za matunda asili kwa kutengeneza nyumbani kwa kutumia mashine ya blenda utajikuta unaweza kukaa hata miezi 6 mpaka mwaka bila ya kuumwa na Maradhi yoyote yale na wala kumuona Daktari. Kwani juisi za matunda na mboga za majani ni Dawa na kinga tosha dhidi ya maradhi kuingia mwilini. Kwani juisi zina Alkaline kazi yake kupambana na vijududu (Bacteria) na Virusi (Virus) vya maradhi na pia Alkaline ina kukinga na maradhi kutoingia mwilini mwako. Mkuu tumia juisi za matunda utakuja kuniambia siku za mbele faida yake.
 
Tulimiss vitu vizuri mkuu Dr MziziMkavu
Mkuu kweli nilipotea tangu mwaka 2015 nilikuwa nipo Busy kuwatibia wagonjwa wangu 4 watatu walikuwa wana maradhi ya siku hizi AIDS/HIV na mmoja alikuwa anayo maradhi ya Hepatiti B Virus. kati ya hao wagonjwa wangu 4 wawili wamesha pona wamebaki 2 Mgonjwa mmoja mwenye AIDS/HIV amepona na mgonjwa mmoja alikuwa anayo maradhi ya Hepatiti B Virus amepona ninashukuru Mungu Dawa zangu zinawasaidia na nipo busy siku hizi kwenye What's App ninazungumza na watu karibu 50 kwa siku basi wananifanya ninakuwa hata shughuli zingine zinanipita lakini ni wagonjwa ninao zungumza nao si chat na marafiki bali ni wateja wangu kila siku lakini nimerudi tena mkuu utakuwa unapata faida zangu .
 
Kunywa juisi badala ya kulila tunda lenyewe ni sawa na ile ishu ya kukoboa mahindi na kusaga then ndio kula ugali badala ya kusaga moja kwa moja.
 
Kunywa juisi badala ya kulila tunda lenyewe ni sawa na ile ishu ya kukoboa mahindi na kusaga then ndio kula ugali badala ya kusaga moja kwa moja.
Mkuu huwezi kufananisha kukoboa unga wa ugali na juisi ya matunda sio sawa sawa kabisa. Kwani unapo kula tunda moja na mtu anayetengeneza juisi ya hilo hilo tunda ulilo kula wewe, faida zake zipo tofauti kidogo.Kwani tunda huwezi kula zaidi ya matunda 2 kwa wakati mmoja, lakini juisi ya glasi moja ukiitengeneza nyumbani unaweza kutengeneza matunda karibu matunda 5 kwa juisi ya glasi moja tu. Kwa hiyo kula tunda moja au mawili na kunywa juisi glasi moja bora kunywa juisi ya glasi moja. Lakini juisi yenyewe ni juisi ya kutengeneza wewe mwenyewe nyumabani sio juisi ya maboksi au juisi za viwandani juisi za chupa na juisi za maboksi hazifai kabisa kiafya.
 
Umeandika shallow sana.

Unaweza kula matunda zaidi ya moja kwa wakati mmoja,mpaka mtaani unaoata ukitaka.

Matunda yenyewe yana roughage ambayo ukitengeneza juisi unaikosa.Kama nanasi ukisaga lazima uchuje utoe makapi.na kumbuka yamekua makapi baada ya blending.
 
yees hii point na nimekupata.kuns vitu baadhi vinatoka ukisaga matunda hasa zile nyuzi nyuzi mfano kwenye maembe,machungwa pia baadhi ya maganda ambayo ni muhim mfn ktk tango.
 
Ukihisi una uelewa wa kitu flani na unataka ku share na wanajamii nao wafaidike kwa ujuzi wako una anzisha thread yako safi kabisa...watu tutapita tutasoma na kukushukuru kwa upendo...kama nami kwa sasa navo mshukuru dr.MZIZI MKAVU!kwa sababu sijalipia alicho nifundisha..ntakitumia milele....

Sasa unakuja ku crashi alichoandika mwenzakk na kusema yuko shalo....ko we ndo uko deep???
Kama ni ivo si ungeanza wewe kutoa elimu!!
 
Asante sana mzizi mkavu kwa elimu,juice hizo ni nzuri sana Na hata hupaswi kuchuja maana ukiblend inalainika kabisa hata mbegu za tikiti zinasagika zile nzito zinatuama chini unaweza kuziacha au ukala pia nimefurahia sana sana juice hizi asante.
 
Mzizi mkavu hapo umegusa penyewe.mimi kwangu huwa kila Siku tunakunywa juice ya mchanganyiko wa matunda na tuna muda sana hatujaenda hospital maana miili iko fiti sana.nimekuelewa vzr mkuu
 
Mkuu kweli nilipotea tangu mwaka 2015 nilikuwa nipo Busy kuwatibia wagonjwa wangu 4 watatu walikuwa wana maradhi ya siku hizi AIDS/HIV na mmoja alikuwa anayo maradhi ya Hepatiti B Virus. kati ya hao wagonjwa wangu 4 wawili wamesha pona wamebaki 2 Mgonjwa mmoja mwenye AIDS/HIV amepona na mgonjwa mmoja alikuwa anayo maradhi ya Hepatiti B Virus amepona ninashukuru Mungu Dawa zangu zinawasaidia na nipo busy siku hizi kwenye What's App ninazungumza na watu karibu 50 kwa siku basi wananifanya ninakuwa hata shughuli zingine zinanipita lakini ni wagonjwa ninao zungumza nao si chat na marafiki bali ni wateja wangu kila siku lakini nimerudi tena mkuu utakuwa unapata faida zangu .
Tunahangaika huku kwa zaidi ya miaka 30 sasa kutengeneza chemical formulas ili kupata dawa ya kutibu HIV/AIDS na hao retroviruses wengine, kumbe wewe unazo dawa?!

Hebu tuletee hiyo formula uwe bilionea! Kwa nini ufe maskini?!
 
Back
Top Bottom