Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

Excellent.This is a very imformative and useful thread.Sio ngono,ngono, ngono na ujinga mwingine.Keep it up.
 



Poa sana mkuu hii inatujenga kiafya, God be with you.
 
AVOCADO NA FAIDA ZAKE











Avocado likiwa linaandaliwa kwa kukamulia limao ili kuongeza ladha


Leo napenda niendeleze mada ya tunda la avocado pamoja na faida zake. Kabla ya kuongelea faida zake ningependa nielezee kwanza vitu ama virutubisho vinavyopatikana ndani ya tunda hilo. Vitu hivyo ni kama ifuatavyo;



MAJI: tunda hili lina kiasi kidogo cha maji tofauti na matunda mengine tuliyozoea kula.

MAFUTA: avocado lina kiwango kikubwa cha mafuta na ndani ya kiasi hicho cha mafuta kuna tindikali (acid) mbalimbali zinazosaidia kukinga na kutibu maradhi katika mwili.

PROTINI: tunda hili pia lina kiwango cha juu cha protini kutegemeana na aina ya tunda lenyewe. Ndani ya protini pia kuna tindikali (acid) aina ya amino.

VITAMINI "E": inadaiwa kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama, hata mayai hayana kiwango kikubwa ukilinganisha na tunda la avocado.

VITAMINI "B6": Nayo inapatikana kwa wingi.

MADINI YA CHUMA (Iron): Pia yapo kwa wingi.



Baada ya kuvielezea baadhi ya virutubisho vinavyopatikana katika tunda hili, sasa tuangalie faida zinazotokana ama kwa kula au kutumia tunda la avocado au matumizi ya mmea wenyewe. Kwanza kabisa ningependa ujue kwamba majani ya mti wa avocado pamoja na magamba ya mti wake yakitengenezwa vizuri yanatumika kutibu maradhi ya kuharisha, kuondoa gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo. Dawa hii haishauriwi kutumiwa na akina mama wajawazito kwani inaweza kuwaletea matatizo yanayoweza kuharibu mimba. Aidha kwa wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, wanaweza kutumia mchanganyiko huo kwa nia njema ya kuwawezesha kuingia kwenye period.



Tunda la avocado ni chakula kizuri kwa watoto, pia lina madini ya potasiam (potassium) na vitamin B6 na E ambazo zinaweza kuleta nafuu kwa wale wenye matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na uanithi. Tindikali aina ya oleic (oleic acid) iliyomo ndani ya tunda hili inasaidia kukinga dhidi ya magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa. Aidha tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani tunda hili lina "fiber" ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya artery wanashauriwa kula tunda hili mara kwa mara. Tunda la avocado limethibitishwa kupunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa wale wenzangu na mimi ambao ni wanene.



Matumizi ya nje ya mwili kwa tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa makwinyanzi, kung`arisha na kulainisha nywele na kuzifanya zionekane nadhifu, linasaidia ukuaji wa nywele na pia kuimarisha na kuzuia kukatika kwa nywele.



Hakika tunda hili lina maana sana kwa maisha yetu ya kila siku na inashauriwa kula tunda hili mara kwa mara kutegemeana na uwezo wako kwani hautopoteza chochote utakapokula tunda hili. Mada ijayo nitakupa vidokezo vichache namna ya kuandaa tunda hili kabla ya kuliwa.
 
KAROTI NA FAIDA ZAKE
Habari za maisha wakuu wenzangu! Naomba leo niwape japo kidogo kuhusu matumizi ya zao la karoti pamoja na faida zinazopatikana kutokana na utumiaji wa zao hilo, ambalo kimsingi mizizi yake ndiyo hasa zao lenyewe. Napenda niwaombe radhi wale ndugu zangu waliouliza maswali juu ya kujikinga ama namna ya kuondokana na unene. Mada inayohusu unene na athari zake nitaitoa wiki ijayo na nitakupa dokezo ambazo zitakusaidia kuondokana na unene au kitambi.Tukirudi kwenye mada ya leo, kumbuka kuwa karoti inalimwa karibu kila pembe ya dunia hii. Zao hili linatofautiana katika rangi, kwani kuna karoti nyeusi, zenye rangi ya pinki, nyekundu na njano. Karoti yenye rangi nyekundu na njano ndiyo hasa tunayolima hapa TZ. Karoti za rangi nyekundu na njano ndizo zinasemekana kuwa na virutubisho vingi sana kuliko karoti nyingine. Karoti ina protini kidogo na haina mafuta kama tulivyoona kwa tunda la avocado. Pia ina asili ya wanga, na ni chanzo kizuri cha vitamini B, C na E. Aidha ina madini mengi ikiwemo madini ya chuma. Kuna kitu kinaitwa beta-caroteneambayo imo ndani ya karoti na hii ikiingia mwilini inabadilishwa na kuwa vitamini A. Vile vile karoti ina kirutubisho kinachoitwa fiber ambacho ni muhimu kwa kukinga kuta za utumbo.Karoti ikitumiwa vizuri na tena mara kwa mara inasaidia kukinga na kuponya magonjwa yafuatayo: macho hasa kutoona gizani au kwenye mwanga hafifu, ngozi, kupunguza tindikali inayodhuru tumboni na kukinga magonjwa yenye asili ya kansa. Karoti inaweza kuliwa kwa namna mbalimbali kama vile, ikiwa mbichi kwa kutafuna, inaweza kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga zingine, inaweza kusagwa na kupata juisi ambayo pia inaweza kuchanganywa na juisi zingine, aidha kukatwakatwa na kuchanganywa kwenye salad ya matunda au mbogamboga. Machicha ya karoti iliyosagwa yanaweza kutumika kama dawa kukinga ama kuponya maradhi ya nje ya mwili. Kama

karoti imestawishwa kwa kutumia madawa ya mimea na mbolea au kama huna uhakika na usafi wake, ni vizuri ukwangue maganda yake ya juu na kuyaondoa. Unaweza kuamua kukata vipande virefu au vya mviringo, kukata na mashine maalum vipande vidogo vidogo au kula nzima nzima.Karoti ni tamu vyovyote utakavyoamua kuila, iwe mbichi au iliyochemshwa. Ingawa kula karoti mbichi ni bora zaidi, lakini hata ukila iliyopikwa bado

haipotezi virutubisho vyake, zaidi inaelezwa kuwa, kambalishe, virutubisho pamoja na sukari yake inapatikana kirahisi na hivyo kuifanya kuwa tamu.Jambo la kuzingatia kama ukiamua kuipika, usiipike sana, bali inatakiwa kuchemshwa au kupikwa kwa muda mfupi ili virutubisho vyake visipungue au kupotea kabisa.
DONDOO ZA KUTENGENEZA KAROTIUnaweza kuitengeneza karoti kama unavyotaka ili kupata ladha tofauti bila

kupoteza virutubisho vyake. Unaweza, kwa mfano, kutengeneza saladi ya karoti kwa kuchanganya na majani yake kwa kukatakata vipande.Aidha, unaweza kutengeneza saladi kwa kukata vipande vidogo vidogo kisha kuchanganya tufaha na matango na kula pamoja kwenye mlo wako wa siku kama kachumbari.
Unaweza kutengeneza supu ya karoti kwa kuchemsha vipande vyake na nyanya. Chukua karoti na nyanya ulizochemsha, kisha

weka kwenye ‘blender’ au chombo kingine unachoweza kusagia. Saga mchanganyiko huo ili kupata supu, unaweza kuongeza viungo vingine ili kupata ladha. Unaweza pia kuinywa ikiwa ya moto au ikiwa imepoa.
Kinywaji kingine unachoweza kutengeneza kwa afya yako ni juisi ya karoti, ‘soymilk’ na ndizi mbivu. Tengeneza nusu glasi ya juisi ya karoti, chukua glasi moja ya soymilk na ndizi mbivu moja kisha changanya kwa kutumia

‘blender’. Kama huna changanya kwa kutumia kijiko au mwiko na kupata ‘milk shake’ ya ukweli.
KAROTI IKIZIDI MWILINI Ingawa siyo rahisi kutokea lakini inawezekana kuna watu matumizi ya mboga hii kwao yako juu. Karoti ikizidi mwilini, huweza kumfanya mtu aonekane ‘wa njano’, hasa katika sehemu za viganja vya mikono, nyayo za miguu na nyuma ya masikio. Kitaalamu hali hii hujulikana kama ‘carotoderma’.Hata hivyo, hali hiyo

hutoweka pale mtu huyo anapopunguza ulaji wa karoti au vyakula vingine vyenye kiwango kikubwa cha virutubisho vya ‘carotene’ na hakuna madhara mengine anayoweza kuyapata.Mwisho, katika nchi za Asia, ambako ndiko karoti inaelezwa kuanzia, inaaminika pia kuwa na uwezo wa

kurekebisha masuala ya nguvu za kiume na ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi (sexual dysfunction & sexual drive).
Pia karoti inaaminika kuimarisha ufanisi wa figo na kuondoa hewa chafu na baridi mwilini. Baada ya kujua faida za karoti, bila shaka kuanzia leo umepata sababu ya kuiangalia upya karoti kama ‘mzizi’ muhimu kwa afya yako
 
KABICHI:Kinga kubwa dhidi ya saratani​

Ugonjwa wa saratani (cancer) ni miongoni mwa magonjwa hatari yanayosumbua watu duniani hivi sasa, Tanzania ikiwemo.

Wagonjwa wanaongezeka kila kukicha katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, ambayo ni maalum kwa ugonjwa huu.

Katika makala ya leo, tutajifunza faida za kabichi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, licha ya kuchukuliwa kama ni mboga ya kimaskini na ambayo huliwa kwa shida zaidi kuliko kimanufaa ya kiafya.

Ingawa inaonekana kuwa kabichi ni miongoni mwa mboga za majani zinazolimwa kwa wingi na kusambazwa kwenye masoko mengi nchini, hasa katika miji mikubwa, lakini ni watu wachache sana wanaopenda kula mboga hii.

Katika miji mikubwa, kabichi inatumika zadi kwa walaji wa chips. Hata hivyo hawaitumia ipasavyo kwa sababu huwa inapikwa na kukaangwa kwa mafuta kwa muda mrefu na hivyo kupoteza baadhi ya virutubisho vyake muhimu.

KINGA DHIDI YA SARATANI
Miongoni mwa faida nyingi zinazopatikana kwa kula kabichi (nyeupe na nyekundu), inayoongoza ni ile ya kutoa kinga dhidi ya ugonjwa hatari wa saratani.

Inaelezwa kuwa zaidi ya tafiti 475 zimefanyika kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye kabichi na kuthibitisha kuwa vina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani na wakati mwingine kutibu.

Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee katika kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za virutubisho;
‘Antioxidant', ‘Anti-inflammatory' na ‘Glucosinolates,' ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa nyemelezi kadhaa ambayo husababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.

Kwa kuzingatia madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuzia ulaji wake. Laiti kama watu wote tungejua sawasawa faida za kabichi, bila shaka mboga hii ingekuwa ghali kuliko hata samaki.

AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO
Mbali ya kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, juisi ya kabichi inaelezwa kuwa na faida nyingi tumboni, hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo (peptic ulcers). Ikitumika mara kwa mara huwa kama tiba kwao. Hali kadhalika mfumo wa usagaji chakula tumboni, huwa imara.

HUIMARISHA MFUMO WA MOYO
Utafiti mwingine uliofanyika kuhusu kabichi umeonesha kuwa mboga hii huimarisha mfumo mzima wa moyo kwa kudhibiti utengenezwaji wa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini ambayo inapozidi mwilini, husababisha matatizo ya moyo.

VITAMINI ZINAZOPATIKANA KWENYE KABICHI
Ndani ya kabichi, kuna kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin, hususan Vitamin K, Vitamin B1, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Ili kupata faida za kabichi na kujenga kinga imara dhidi ya magonjwa ya saratani, weka mazoea ya kula kabichi mara kwa mara, angalau mara tatu kwa wiki, kwa namna ambayo utaona mwenyewe inafaa, iwe kama mboga au kachumbari.




Katika miji mikubwa, kabichi inatumika zadi kwa walaji wa chips. Hata hivyo hawaitumia ipasavyo kwa sababu huwa inapikwa na kukaangwa kwa mafuta kwa muda mrefu na hivyo kupoteza baadhi ya virutubisho vyake muhimu.

KINGA DHIDI YA SARATANI
Miongoni mwa faida nyingi zinazopatikana kwa kula kabichi (nyeupe na nyekundu), inayoongoza ni ile ya kutoa kinga dhidi ya ugonjwa hatari wa saratani.

Inaelezwa kuwa zaidi ya tafiti 475 zimefanyika kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye kabichi na kuthibitisha kuwa vina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani na wakati mwingine kutibu.

Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee katika kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za virutubisho;
‘Antioxidant', ‘Anti-inflammatory' na ‘Glucosinolates,' ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa nyemelezi kadhaa ambayo husababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.

Kwa kuzingatia madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuzia ulaji wake. Laiti kama watu wote tungejua sawasawa faida za kabichi, bila shaka mboga hii ingekuwa ghali kuliko hata samaki.

AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO
Mbali ya kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, juisi ya kabichi inaelezwa kuwa na faida nyingi tumboni, hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo (peptic ulcers). Ikitumika mara kwa mara huwa kama tiba kwao. Hali kadhalika mfumo wa usagaji chakula tumboni, huwa imara.

HUIMARISHA MFUMO WA MOYO
Utafiti mwingine uliofanyika kuhusu kabichi umeonesha kuwa mboga hii huimarisha mfumo mzima wa moyo kwa kudhibiti utengenezwaji wa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini ambayo inapozidi mwilini, husababisha matatizo ya moyo.

VITAMINI ZINAZOPATIKANA KWENYE KABICHI
Ndani ya kabichi, kuna kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin, hususan Vitamin K, Vitamin B1, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Ili kupata faida za kabichi na kujenga kinga imara dhidi ya magonjwa ya saratani, weka mazoea ya kula kabichi mara kwa mara, angalau mara tatu kwa wiki, kwa namna ambayo utaona mwenyewe inafaa, iwe kama mboga au kachumbari.
 
NANASI:KINGA DHIDI YA MAGONJWA YA UVIMBE

​



Mwili unapokosa kinga imara, huwa katika hatari ya kushambuliwa na kila aina ya magonjwa. Katika orodha hiyo ya magonjwa, yamo pia yale ya kutokwa na uvimbe yakiwemo majipu. Kitaalamu magonjwa haya yanajulikana kama ‘Inflamatory diseases’.

Katika kukabiliana na matatizo kama hayo, nanasi ni moja kati ya matunda yenye vitamin nyingi na virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuupa kinga mwili wako dhidi ya magonjwa hayo na mengine.

Siri na umuhimu wa nanasi upo kwenye kirutubisho aina ya ‘Bromelain’ ambacho kinapatikana kwa wingi kwenye tunda hili. Virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa muhimu sana katika kujenga na kuimarisha kinga ya mwili.

Ukilipa umuhimu na ukiliweka nanasi katika orodha ya matunda unayokula mara kwa mara, utajiepusha na utajipa kinga dhidi ya magonjwa mengi hususan ugonjwa wa kuwashwa na kuvimba koo, ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis) na ugonjwa wa gauti (Gout).

Ili upate kinga dhidi ya maradhi hayo kwa kula nanasi, unashauriwa kula tunda hilo kabla au baada ya kula mlo wako. Usile nanasi pamoja na chakula kingine kwa wakati mmoja. Kwa kufanya hivyo, virutubisho vitafanya kazi nyingine tofauti na uliyokusudia. Faida nyingine za nanasi ni kama ifuatavyo;

USAGAJI WA CHAKULA
Nanasi lina virutubisho vinavyouwezesha mfumo wa usagaji chakula tumboni kufanya kazi yake ipasavyo. Pindi mfumo huu unapowezeshwa kufanya kazi yake vizuri, mtu huweza kupata choo laini na kwa wakati kama inavyotakiwa.

KINGA YA MWILI
Nanasi linaaminika pia kuwa miongoni mwa matunda yenye Vitamin C kwa wingi ambayo kazi yake ni kuupa mwili kinga dhidi ya ‘wavamizi’ mbalimbali (free radicals), ambao wanapoingia mwilini, kazi yao huwa ni kuharibu chembembe hai za mwili.

Kwa kuongezea, Vitamin C inaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Mwili huwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya magonjwa madogo madogo kama vile mafua, kikohozi, homa na maambukizi mengine.

CHANZO CHA MADINI
Mbali ya kuwa ni chanzo kizuri cha vitamin C, nanasi pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya ‘Manganese’ ambayo yanaaminika kuwa na uwezo wa kuboresha ufanisi wa vimeng’enyo mbalimbali vya mwili, vikiwemo vya kuzalisha nishati na kinga. Hali kadhalika tunda hili lina kiwango cha kutosha cha Vitamin B1 (Thiamine).

KUIMARISHA NURU YA MACHO
Inawezekana karoti ikawa ndiyo inayojulikana na watu wengi kuwa na uwezo wa kuimarisha nuru ya macho lakini nanasi nalo lina uwezo mkubwa wa kuimarisha nuru ya macho. Utafiti unaonesha kuwa ulaji wa tunda hili na matunda mengine, kiasi cha milo mitatu kwa siku, kunaondoa hatari ya kupungua kwa nuru ya macho kwa asilimia 36 kwa watu wazima.

NANASI BORA
Nanasi bora ni lile kubwa na lililoiva vizuri. Ni kweli kwamba nanasi kubwa lina nyama nyingi kuliko nanasi dogo lakini hakuna tofauti ya ubora wa virutubisho kati ya nanasi dogo na kubwa, ili mradi lisiwe limeoza au lenye michubuko mingi. Chagua nanasi lilioiva vizuri na lenye kunukia.

Mara baada ya nanasi kumenywa na kukatwa vipande, linatakiwa kuliwa mara moja, iwapo litahifadhiwa kwenye jokofu kwa ajili ya kuliwa baadaye, njia sahihi ya kuhifadhi ni kuliweka kwenye chombo chenye mfuniko (container). Hii husaidia kuhifadhi virutubisho vyake kwa kipindi cha hadi siku tano bila kupoteza ubora wake, ikiwa pamoja na ladha. Unaweza kula vipande vya nanasi au juisi yake, vyote vina faida.

 

Attachments

  • Pineapple.jpg
    23.1 KB · Views: 13,416
Huo mchanganyiko wa matunda, unachanganya na maji na kuongeza sukari? au ni matunda pekeyake?
Huo mchanganyiko wa matunda unaweza kutia sukari kijiko kimoja kikubwa na maji kama glasi moja tu ili kuifanya iwe tamu au waweza kuachia bila ya kutia sukari itakuwa pia bora mkuu.
 
Tiba ya juisi kwa mwathirika wa Ukimwi


Juicer, Kifaa cha kusagia matunda (Blender), karoti nne (kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kinga mwilini na kuongeza kiwango cha CD4 kutokana na viini lishe vya ‘beta carotene’).

Robo ya kiazi kinachofahamika kama ‘beetroot’ (ili kuongezea nguvu maini na kuzuia uwezekano wa kuzalishwa vitu visivyohitajika mwilini kwani kiazi hicho kina kiini lishe kiitwacho ‘betane’).

Kipande cha tangawizi (kwani ina madini ya ‘selenium’ ambayo hupunguza kuongezeka kwa virusi mwilini. Pia huhamasisha kuzaliana kwa kinga zaidi mwilini).

Kiasi kidogo cha binzari (turmeric- kwani ina madini ya curcumin yenye uwezo mkubwa wa kupambana na sumu na kuzuia kuongezeka kwa virusi. Binzari ni rafiki mkubwa wa maini).

Kipande cha kitunguu chekundu (kina madini viini lishe maalumu –aquercetin- vinavyoongezea uwezo wa kuponya wa Vitamini C, mpambanaji muhimu wa virusi vya Ukimwi huku pia kikiwa na ‘allicins’ inayozuia kuwapo na magonjwa nyemelezi).

Vipande vinne vya vitunguu swaumu (hivi huondoa sumu kwenye chembe hai zote mwilini. Ni silaha zenye nguvu za ‘allicins’, ‘selenium’ na chembe hai nyingine muhimu kupambana na virusi).

Majani nane ya ‘spinach’ (Haya yana utajiri wa ‘chlorines’ ambayo huongeza kinga mwilini na kupambana na maradhi. Pia yana SOD au ‘Super Oxide Dismutase’, ‘sterols’ na ‘sterolins’. Madini haya huongeza CD8 pamoja na CD3).

1. Vioshe vyema vitu hivi.
2. Osha mbogamboga vizuri kwa maji safi.
3. Weka mbogamboga hizo kwenye bakuli lisilopitisha hewa.
4. Tia maji safi ya kunywa hadi yafunike mbogamboga hizo.
5. Koroga na funika haraka kwa mfuniko thabiti.
6. Baada ya dakika tano ondoa kifuniko, toa maji na kamua mbogamboga kupata juisi yake.

JINSI YA KUTENGENEZA

1. Weka juisi hiyo kwenye ‘blender’ kisha ongeza:

a) Vijiko viwili vya unga wa karanga za Brazil. Karanga hizo zina asili ya utajiri mkubwa wa ‘selenium’ miongoni mwa vyakula vingi vikavu. ‘Selenium’

huzuia kuongezeka kwa virusi na husaidia kuponya mgonjwa. (Vyakula vingine vyenye ‘selenium’ ya kutosha ni mbegu za alizeti, samaki, maini na

nyama ya nguruwe (bacon). Hivi unaweza kuvila tofauti kwani haviwezi kusagwa pamoja na juisi)

b) Parachichi nusu.

2. Saga mara moja. Usitunze kwenye jokofu.

Nyongeza:

i. Kunywa juisi hiyo walau mara mbili kwa siku wakati tumbo likiwa halina kitu. Kadri ya kiwango utakachotumia ndivyo utakavyopata nafuu

ii. Kama inawezekana pia kunywa juisi halisi ya nanasi kila siku kusaidia tiba hiyo ya maji ya matunda (juice therapy). Nanasi lina madini ya ‘bromelain’ yenye uwezo mkubwa wa kupambana na virusi.

iii. Juisi ya tikiti nayo ni nzuri kwa mgonjwa wa Ukimwi. Hii ni kwa sababu matikiti yana virutubisho viitwavyo ‘glutathiones’ vinavyozuia kuongezeka kwa virusi.

3. Furahia maisha huku ukiusaidia mwili wako kupambana na wavamizi (virusi vya Ukimwi)!
 
katika pita pita zangu nikakutana na waraka ulioeleza waziwazi kuwa endapo mama mjamzito akitumia tunda aina ya nanasi basi anaweza kupata matatizo, ambayo yanaweza kusababisha hata ujauzito kutoka au kitoto kufariki kabisa!!! Pia walaka huo uliendelea kueleza kuwa wanawake wengine hupata "heart burn" wanapotumia tunda hili pindi wawapo wajawazito. Kwa mwenye taarifa zaidi kuhusiana na tunda hili tafadhali unakaribishwa, uweze kuchangia madhara ya tunda hili kwa mama mjamzito, karibun wakuu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…