MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Wasalaam wakuu!
Najua juu ya hili suala ni vigumu sana kuelewana lakini ni muhimu pia kutazama upande wa pili wa Shilingi kwa maana ya hasara za kutumbua majipu japo hakuna anayependa kuchezewa kwa rasirimali za umma.
Kwa moyo wangu mweupe kabisa nakubaliana na dhana ya utumbuaji majipu ili kujenga nidhamu ya kutumia vizuri dhamana za umma.
FAIDA ZA UTUMBUAJI MAJIPU!
Hii ni pamoja na kumpampa uwezo wa kujitambua na kujitatjmini mtumishi wa umma kwa dhamana aliyopewa, kuyajua vema majukumu yake, kujenga nidhamu na uwajibikaji ktk kutumia vizuri dhamana hizo, kupunguza umungu mtu kwa baadhi ya viongozi na kuwaona watanzania wote sawa.
I
HASARA ZA UTUMBUAJI MAJIPU!
Kwa mtizamo wangu Mimi hii pamoja na kusababisha msongamano mkubwa wa kesi mahakamani kutokana na watuhumiwa wengi kutimuliwa kazini pasipo na uchunguzi wa kutosha au kujiridhisha na tuhuma hizo, tatizo ni kwamba watuhumiwa wengi hushinda kesi zao kwa sababu tuhuma zao mara nyingi hua ni kihisia zaidi na sio kiuhalisia hali ambayo baadae huliingiza taifa katika hasara kubwa ya kulipa fidia. Hasara nyingine ni baadhi ya viongozi kufanya kazi kwa hofu na pupa kubwa bila kutambua mgwanyo kazi zao(Job description)! hali ni inatokana na woga wao wa kufukuzwa kazi na wateule wao na kupelekea ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kazi.
USHAURI WANGU!
Ni vizuri na bora zaidi kupambana na mfumo ulioyapa majipu hayo kufanya kazi kwa utaratibu huo na kujenga mfumo mpya wenye weledi na sio kufukuza tu kila panapohisiwa na kua na harufu ya tuhuma.
Inawezekana kabisa wengine waliingizwa mkenge na mfumo uliokuwepo na wengine nao waliingizwa na tamaa zao.