Faida/Changamoto za biashara ya Mabasi

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,162
9,245
Wakuu

Kuna kitu hapa natamani tujaribu kujadiliana kwa pamoja juu ya hii biashara ambayo imeonekana kuacha watu wengi na maswali huku watu wengi pia wakiwa na majibu.

Tujadiliane kuhusu biashara hii ya mabus makubwa Engine Model za Scania, Yutong, Nissan, Diesel, Zhongtong Higer, Kinglong, nakadhalika.

Mimi kwa upande wangu biashara ya mabusi ndio biashara pekee ya ndoto zangu. Pamekuwa na kauli nyingi za ukweli na pia zipo za kupotosha, wapo wanaoamini huwezi kufanya biashara ya mabusi bila kuwa mshirikina wapo pia wanaoamini wamiliki wa mabusi wanapata faida maradufu.

Jamiiforums ina bahati kunipata mimi atleast wanajamiiforums wataweza kupata baadhi ya majibu wanayojiuliza kuhusu biashara hii, nasema baadhi ya majibu kwasababu si kila kitu kinafaa kuweka hadharani. Uchawi ndio neno kuu linalotawala mtu anapozungumzia biashara hii.

Je, wapigadebe wananafasi gani kwenye biashara hii. Je, ni kweli bank zinaongoza kukopesha wamiliki wamabusi

NB:Watu wenye nyota zenye asili ya moto au chuma wanaweza kufanya biashara hii na kufanikiwa

Je, wewe unafahamu nini kuhusu biashara hii?

----------------------

Baadhi ya michango

Hii biashara bhana, kuna kampuni kama dar express miaka ya nyuma hata kama gari lilikuwa lina abiria 9 gari lilikuwa linafanya safari hivyohivyo cha ajabu siku si nyingi nilikuwa natokea rombo na dar express tulivyofika njiapanda gari lilikuwa na abiria kama 21 hivi,ikabidi tufaulishiwe kwenye gari jingine lililokuwa linatoka Arusha sababu tulikuwa wachache tulikaa pale kituoni Zaidi ya masaa manne na kila basi lililokuwa linakuja la kampuni ya dar express lilikuwa limejaa tukiuliza imekuwaje hivi,wanasema ni maagizo kutoka kwa boss wao mr.mremi tukaja kupata gari saa8 mchana lakini sikufurahishwa kabisa na huduma zao dar express wa miaka ya nyuma si kama wasasa huduma ni mbovu,mabasi yamechakaa sana nakumbuka nilikaa siti ya dirishani kioo kilikuwa hakifunguki ukiangalia siti vitambaa havijafuliwa.

Kwa wale watu wa marangu,mwika na rombo nadhani mtakubaliana na mimi hii kampuni ilipendwa sana na watu wa kaskazini na binafsi mimi nilikuwa nipo radhi kukata tiketi hata ya basi la Arusha mradi nipande dar express nasikitika sana sijui nini kimeikumba hii kampuni kuna mtu nilisikia anasema mzee mremi anadaiwa pesa na stanbic sasa sijui labda hii ndio sababu inayopelekea kampuni hii kuyumba kingine nilichokiona katika hii kampuni ni aina ya mabasi wanayo agiza ni ya gharama mno,sasa fikiria umeagiza marcopolo ya bilioni 1 then bahati mbaya ikapata hitilafu si ndio itakuwa mwanzo wa kufilisika'

Ningemshauri mzee mremi anunue hata yutong,mbona kuna yutong nzuri tuu...mfano yutong kama za tahmeed japo hatodumu nazo lakini itakuwa afadhali kuliko Scania za gharama kubwa sababu kuna watu bado wana Imani na kampuni hii na wangetamani kuona huduma zake zinakuwa bora kama mwanzo ukiangalia sasa hivi kuna ushindani mkubwa sana

Kampuni kama tilisho,extra luxury,esther,marangu na first choice zinakuja kwa kasi sana kwa njia ya rombo dar express inabidi wabadilike na simaanishi wawe wanapakia abiria wachache kama mwanzo ila namaanisha wabadilike katika huduma.huduma ziwe bora na wazingatie usafi pia waige hata mfano wa Kilimanjaro express.

falcon mombasa

Habari Mkuu,

Biashara hii ya mabasi kwa ujumla wake ni biashara nzuri. Binafsi kama mtaalamu wa masuala ya biashara kuna makampuni ya hizi daladala zaidi ya 10 tushawahi kuyaandikia michanganuo ya biashara hii na kupata mikopo, kuna baadhi hadi sasa kuna baadhi ya makampuni hayo kwa hapa Dar yana mabasi zaidi ya 80 kwa kampuni moja. Na ukija upande wa mabasi makubwa kuna kampuni kama 5 tushazifanyia kazi hizo na kuna baadhi almost kampuni 3 zinaenda vema sana na kampuni 2 hazipo vema. Lakini juu ya yote biashara hii kwa uzoefu na mahojiano na wafanyao biashara hii inafanana na ya malori kiasi kikubwa. Biashara hii inaweza kuwekwa katika sehemu mbili

1. Kitaalamu
Kabla ya kuanza biashara hii ni vema kujitahidi kuijua vema "feasibility study" na kujua unataka nini kutoka katika biashara hii. Nikiwa na maana wataka FAIDA PEKEE au wataka JINA NA HESHIMA(Legacy) au vyote? Katika kuijua jitahidi ujue mambo

A: NJIA, MJI, WASHINDANI
1. Unataka kupeleka basi lako njia ipi?
2. Je barabara za mji uendao zina hali gani?
3. Je washindani wako wana mabasi ya aina gani?
4. Je washindani wako wanatoa huduma zipi za kipekee?
5. Je wewe una kipi cha kipekee na kilichoboreshwa katika kutoa huduma ya usafiri kwa wateja?
6. Umejipangaje kuwateka abiria wa washindani wako

B: MTAJI
Kwa uzoefu wa biashara hii hasa kwa nyakati hizi na nikitumia mfano wa mteja wa mwisho (Machi 2018), suala la mtaji kuwa kiasi gani litakuweka sokoni. Kwa sasa basi zilizopo sokoni na zenye soko Tanzania ni za Kichina. Basi lililo na vitu vya ziada kama Friji, Ac, viti siti za raha nk ie daraja la juu ilikuwa mil 400 kasoro kidogo (hapa bado hujalipa bima, Sumatra, Taboa nk lkn kila kitu tyr hadi usajili TRA) kwa basi moja. Sasa we kama mtaji wako mdogo itakusumbua sana kulishika soko. Vinginevyo toa basi za kawaida ambazo utazipeleka "ndani ndani" huko lakini sio sehemu za mijini kama Tanga, Mombasa, Arusha, nk. Laah hasha ukiwa mbishi basi zako ziwe za mwisho kutoka mji mmoja kwenda mji mwingine.

C: GHARAMA ZA UENDESHAJI
Hili nalo ni muhimu sana kujitahidi kujua kwamba gharama za safari moja "Trip expenses" zipoje. Je nauli na idadi ya abiria watakaopanda wataweka sawa hesabu na faida ikabaki? Lazima uwe makini na mkali hasa katika usimamizi na uendshaji mzima wa biashara hii. Maana kuongezeka kwa gharama yyt mfano lita 50 zaidi ujue hilo nalo ni gharama ambayo inakata faida.

D. JENGA JINA, HESHIMA NA VIWANGO
Kuna baadhi ya makampuni mpaka leo ukiongea au bado yanatolewa mfano kama vile scandinavia. Hawa jamaa walijenga jina, heshima na viwango hatimaye nauli ikajiweka juu yenyewe na mteja alikuwa anaridhika kupanda kwa nauli ya juu bila manung'uniko. Hii inajengeka kwa aina ya basi, ubora wa basi, usalama wa basi, mwendo wa kuridhisha wa dreva, kampuni kua sikivu na kuyafanyia kazi maoni ya abiria wake, wahudumu na huduma nzuri ikiwa pamoja kimavazi na kikauli nk

Hizi sababu nyinginezo ni kutokana na "research from field from owners" wanasema yafuatayo

1. ASILI
Wamiliki wengi waliofanikiwa wanakwambi biashara hii inahitaji nawe uwe na "asili ya chuma au uwe na nyota ya biashara hizi" ie kuwa uwe mtu mwenye kwendana na biashara zinazohusu vyuma kama vile magari aina yyt nk. Kama huna asili au tuseme bahati hij wanakwambia ni ngumu sana kutoboa. Wapo wengi wanatamani lkn wanakwambia hata wakifanya ataishia kuwa na basi si zaidi ya 10

2. ULOZI
Husema kutoa makafara. Ss hii siwezi kulisema sana coz sina ujuzi nalo (cc Mshanajr)

Je, Falcon Mombasa umejipangaje na haya?

Regards
 
Mada nzuri sana hii!

Je, nina basi moja kama lile la bm au kilimanjaro, je likipiga routi moja kutoka dsm to moshi/arusha naweza pata shi ngapi kama faida? Je gharama zake zikoje per day au per month?
 
tukirudi kwenye mada nadhani hii biashara inafaida sana tu,sababu tunaona kampuni kama super feo abood new force kilimajaro express adventure tahmeed nk. zinazidi kukua ina maana kusingekuwa na faida hizi kampuni zisingeendelea pia nadhani kuwa na management nzuri pia inasaidia pamoja na kuzingatia service sababu kuna kipindi kama cha mwezi wa12 kuna baadhi ya mabasi ya kaskazini yanapeleka abiria na kurudi usiku ili kesho wale vichwa tena nadhani na umakini wa dereva unachangia

kulikuwa kuna mabasi kama summry lakini leo hii yamekufa kutokana na kuharibika mara kwa mara na inawwezekana pia na aina ya baadhi ya mabasi hayaendani na hali ya barabara za nchi yetu hivyo kupelekea kuharibika mara kwa mara.
 
Wakuu hiv zile Eicher ama Tata zinazo piga ruti katika jiji la Dar es Salaam ni bei gani ikiwa mpya?
 
Anselim

Kwakweli umemaliza Kila kitu sina hata cha kujazia hapo. Kuongeza tu n kuwa Kwa sasa Rombo to Dar kampuni inayofanya vizuri n Easter na tilisho hizo ndo basi

Nazoweza kupanda endapo nakuja DSM. Au kutoka DSM kuja kaskazini

Dar Express now imekua mkocho tu kama Sai baba
 
Anselim

Aiseee summry Yale mabas cjui yalikua yamelaaniwa au nn maana every day
Yalikua yanauwa watu yan hyo kampany
Cjui Kama ilipata faida kabsa maana
Hata hayakudumu kwenye soko
 
Ukipata dereva mzuri ambaye anaheshimu kazi na gari pia itakuwa nzuri sana,,,Pia biashara sio nzuri sana sababu unashindana na mtu ambaye anapiga hesabu za mafuta tu basi,,,mfano kutoka Moshi to Dar ,nauli nauli ata charge 18k kwahyo ni hasara kwako utakosa wateja
2 ukianza hii biashara fitina lazima upige Lazima yani kwahyo jipange
3 Faida kwa mwezi 10000000
4 ukiweza kukwepa kupata ajali kama kilimanjaro ya moshi to Dar utapata wateja wakudumu kama Juma nature alivyo na mashabiki wakudumu
Zangu dua ufanikiwe mwamba
 
Sasa Ww Falcon Mbona Huna Ulichochangia Kma Jf Tuna Bahati Ya Kuwa Nawe?Embu Andika Mkuu Usintanie Tuelewe Na Utuambie Wewe Unarogea Wapi Pangani Au Pangarawe Kwenye Kizuizi?Au Umekuja Kuchukua Mawazo Ya Watu Ukaimplement Kwako Bila Nasi Kufaidika Na Yako?
 
Biashara ya bus kama huna roho ya paka lazima ufe presha, kwa miaka hii sio biashara ya kusena ujaribu inabidi ufanye utafiti wa kutosha ujiridhishe la sivyo utakula za uso...
Wengi waliopata faida nzuri ni wale waliofanya hii biashara miaka ya nyuma, hivi sasa ushindani ni mkubwa mno, usishangae bus kusafirisha hata abiria wasiozidi 15
 
falcon mombasa

Habari Mkuu,

Biashara hii ya mabasi kwa ujumla wake ni biashara nzuri. Binafsi kama mtaalamu wa masuala ya biashara kuna makampuni ya hizi daladala zaidi ya 10 tushawahi kuyaandikia michanganuo ya biashara hii na kupata mikopo, kuna baadhi hadi sasa kuna baadhi ya makampuni hayo kwa hapa Dar yana mabasi zaidi ya 80 kwa kampuni moja. Na ukija upande wa mabasi makubwa kuna kampuni kama 5 tushazifanyia kazi hizo na kuna baadhi almost kampuni 3 zinaenda vema sana na kampuni 2 hazipo vema. Lakini juu ya yote biashara hii kwa uzoefu na mahojiano na wafanyao biashara hii inafanana na ya malori kiasi kikubwa. Biashara hii inaweza kuwekwa katika sehemu mbili

1. Kitaalamu
Kabla ya kuanza biashara hii ni vema kujitahidi kuijua vema "feasibility study" na kujua unataka nini kutoka katika biashara hii. Nikiwa na maana wataka FAIDA PEKEE au wataka JINA NA HESHIMA(Legacy) au vyote? Katika kuijua jitahidi ujue mambo

A: NJIA, MJI, WASHINDANI
1. Unataka kupeleka basi lako njia ipi?
2. Je barabara za mji uendao zina hali gani?
3. Je washindani wako wana mabasi ya aina gani?
4. Je washindani wako wanatoa huduma zipi za kipekee?
5. Je wewe una kipi cha kipekee na kilichoboreshwa katika kutoa huduma ya usafiri kwa wateja?
6. Umejipangaje kuwateka abiria wa washindani wako

B: MTAJI
Kwa uzoefu wa biashara hii hasa kwa nyakati hizi na nikitumia mfano wa mteja wa mwisho (Machi 2018), suala la mtaji kuwa kiasi gani litakuweka sokoni. Kwa sasa basi zilizopo sokoni na zenye soko Tanzania ni za Kichina. Basi lililo na vitu vya ziada kama Friji, Ac, viti siti za raha nk ie daraja la juu ilikuwa mil 400 kasoro kidogo (hapa bado hujalipa bima, Sumatra, Taboa nk lkn kila kitu tyr hadi usajili TRA) kwa basi moja. Sasa we kama mtaji wako mdogo itakusumbua sana kulishika soko. Vinginevyo toa basi za kawaida ambazo utazipeleka "ndani ndani" huko lakini sio sehemu za mijini kama Tanga, Mombasa, Arusha, nk. Laah hasha ukiwa mbishi basi zako ziwe za mwisho kutoka mji mmoja kwenda mji mwingine.

C: GHARAMA ZA UENDESHAJI
Hili nalo ni muhimu sana kujitahidi kujua kwamba gharama za safari moja "Trip expenses" zipoje. Je nauli na idadi ya abiria watakaopanda wataweka sawa hesabu na faida ikabaki? Lazima uwe makini na mkali hasa katika usimamizi na uendshaji mzima wa biashara hii. Maana kuongezeka kwa gharama yyt mfano lita 50 zaidi ujue hilo nalo ni gharama ambayo inakata faida.

D. JENGA JINA, HESHIMA NA VIWANGO
Kuna baadhi ya makampuni mpaka leo ukiongea au bado yanatolewa mfano kama vile scandinavia. Hawa jamaa walijenga jina, heshima na viwango hatimaye nauli ikajiweka juu yenyewe na mteja alikuwa anaridhika kupanda kwa nauli ya juu bila manung'uniko. Hii inajengeka kwa aina ya basi, ubora wa basi, usalama wa basi, mwendo wa kuridhisha wa dreva, kampuni kua sikivu na kuyafanyia kazi maoni ya abiria wake, wahudumu na huduma nzuri ikiwa pamoja kimavazi na kikauli nk

Hizi sababu nyinginezo ni kutokana na "research from field from owners" wanasema yafuatayo

1. ASILI
Wamiliki wengi waliofanikiwa wanakwambi biashara hii inahitaji nawe uwe na "asili ya chuma au uwe na nyota ya biashara hizi" ie kuwa uwe mtu mwenye kwendana na biashara zinazohusu vyuma kama vile magari aina yyt nk. Kama huna asili au tuseme bahati hij wanakwambia ni ngumu sana kutoboa. Wapo wengi wanatamani lkn wanakwambia hata wakifanya ataishia kuwa na basi si zaidi ya 10

2. ULOZI
Husema kutoa makafara. Ss hii siwezi kulisema sana coz sina ujuzi nalo (cc Mshanajr)

Je, Falcon Mombasa umejipangaje na haya?

Regards
 
Mada nzuri sana hii!!

Je nna basi moja kama lile la bm au kilimanjaro, je likipiga routi moja kutoka dsm to moshi/arusha naweza pata shi ngapi kama faida? Je gharama zake zikoje per day au per month??
Kwanza ukiwa na basi moja hautaruhusiwa kupiga route.
 
Aiseee summry Yale mabas cjui yalikua yamelaaniwa au nn maana every day
Yalikua yanauwa watu yan hyo kampany
Cjui Kama ilipata faida kabsa maana
Hata hayakudumu kwenye soko
ni kwambie kila biashara ina asili ya nyota yake
 
Sasa Ww Falcon Mbona Huna Ulichochangia Kma Jf Tuna Bahati Ya Kuwa Nawe?Embu Andika Mkuu Usintanie Tuelewe Na Utuambie Wewe Unarogea Wapi Pangani Au Pangarawe Kwenye Kizuizi?Au Umekuja Kuchukua Mawazo Ya Watu Ukaimplement Kwako Bila Nasi Kufaidika Na Yako?
hahaahha mkuu mimi sina cha kufetch toka humu sanasana nyinyi ndio mtafaidika unajua huwez kufunguka kila kitu at once lazima upime upepo
 
Back
Top Bottom