Fahamu vigezo sita ambavyo vinaweza kumfanya mwanamke akukimbie au kukuacha kabisa

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,773
3,471
Wakikosa attention yako. Wasichana hupenda pale wanapofahamu kuwa unawasikiliza na unafahamu nini wao wanahitaji. Kama kutakosekana mawasiliano mazuri na atagundua hilo atauona uhusiano huo haumtimilizii haja zake. Hata kama kila kitu kinaenda sawa. Msikilize anapoongea. Kama akiona hapati penzi analolihitaji atatafuta mwingine ambaye yupo tayari kumtimizia.

2. Kumuheshimu. Msichana huwa anajitoa sana awapo katika mahusiano hivyo anategemea mvulana uheshimu hata kwa chochote kidogo anachokufanyia. Mfanye agundue kuwa umeheshimu kile ambacho amekufanyia.

3. Usaliti. Unaposaliti inamaanisha kuna kitu hakipo sawa katika mahusiano yako hata kama una uwezo wa kushughulikia lakini wewe unaona njia sahihi ni kutoka nje kuwa na mahusiano na msichana mwingine ukidhani ndio unarekebisha. Pale msichana wako akikukamata unamsaliti fahamu hawezi kuvumilia naye atakuacha.

4. Ukosefu wa hisia za kimapenzi. Msichana hupenda kuona kuwa wanapendwa wanathaminwa na wapenzi wao wanawajali sasa wakiona kuwa hakuna conection ya hisia za kimapenzi kutoka kwa mvulana wake huona kuwa hakuna mapenzi ya kweli katika uhusiano aliopo

5. Hawapendi kusikia kuhusu mapenzi mara kwa mara wasichana hupenda kutumia muda mrefu na wapenzi wao bila kusikia neno la kuwataka wafanye mapenzi kama ukiwa nao na ukawataka kimapenzi mara kwa mara watakuwa wanakuavoid hata utakapokuwa ukiwagusa.

6. Unapomcontrol sana. Msichana humpenda mvulana atakayemlinda na kujiona yupo sehemu salama sio kumdhibiti kufanya mambo yake mengine anapenda uhuru.
 
Yote sahihi mkuu, ila hio ya 6 ndio ina utata kidogo. Chukulia mfano una msichana mpenda attention, anatongozwa mara kwa mara na ME wanaoingia kwa gia ya urafiki ila haoneshi msimamo kama yupo kwenye uhusiano mpaka unapo comfront. Yani anakuwa hataki ila ana mu entertain mtongozaji instead ya kumkata wenge mazima ili asiendelee kusumbua. Je, hapo nini kifanyike maana ukisema utaonekana controlling! But the situation unakuta inakera ingawa huwezi zuia mpenzi wako asitongozwe ilihali ana mvuto and it happens multiple times.
 
Tumechoka story za hivi na utambue kila mtu ana experience ;feelings za mapenzi kivyake na malezi
 
Mwanaume Pesa bhana.
zingine zoote mbwembwe tu.
We mpe hela!!
Akigeuka, hela!
Akikohoa, hela!
Akiamka, hela!!

Hata Kama Una kidole cha mtoto atakusifia kuwa unamridhisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom