Fahamu kuhusu Ramli

Fahamu kuhusu Ramli

gstar

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
814
Reaction score
1,490
Unafahamu Ramli?

Ramli ni mfumo utumikao kutambua matatizo yaliyofichika, mganga huonekana hodari endapo tu akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga ramli inayo endana na ukweli.

Kabla ya kuaguliwa hupenda kwanza kupiga ramli ili kutambua tatizo, mfano kuchora kwenye kibao ama kutumia mashetani kuyapandisha na kuyaruhusu yanene kupitia mwili wake.

Basi anenewayo hivyo hukubali kama ni kweli ama si kweli, utaona kama ni kweli inakuwa rahisi kuendelea na utaratibu unao fuata wa kuaguliwa.

Ramli nyingi huwa ni za uwongo ama chonganishi, nyingi hutegemea na jinsi ulivyojitambulisha kwa mganga mganga hukusoma saikolojia na kutamka kadiri unavyo taka.

Mfano mganga anaweza kukwambia mbaya wako yupo karibu na wewe ama ni ndugu yako ama ni shangazi yako ilimradi tu azue mtafaruku, anakutengenezea ile negative way of viewing things.

Ramli za ukweli hueleza tukio halisi ama tatizo linalo kusumbua hivyo kufikia hatua ya kwenda kwa huyo mganga.

Mganga aweza kukupa dawa hapo ama kukuagiza vingira (kingira) viambatanishi vya kutekeleza uganga wake mfano kalete kuku (mweupe, mweusi, mwekundu, rangi mchanganyiko) ama mbuzi ama mchele ama mayai, ama mchanga wa kaburi n.k.

Utekelezaji wa uganga (kuaguliwa) unaweza fanyika usiku wa manane kwenye mti mkubwa makaburini porini kwenye shimo refu, baharini, mtoni nk. kutokana na tatizo ulilo nalo.

Baada ya hapo unaweza kuchanjwa chale ama usichanjwe sasa kama una matatizo unaweza ukaambiwa ukavunje nazi njia panda ama upasue yai viza!

Unajua nazi inakuwa na nini? nazi inaandikwa majina ya matatizo yako yote hata kama kuna mtu ni tatizo kwako itapaswa uandike huko. Pia unaweza kutumia yai viza kuandika.

Sasa kinachofuata ni tendo la aibu linalo hitaji ujasiri mkubwa kwanza ukavunje nazi ama yai viza njia panda mchana kweupe!

Ama ukaoge maji ya maiti njia panda kabisa ukiwa uchi wa mnyama.

Ama ukazunguke mmbuyu mara sita, tena mchana kweupe ukiwa umebebeshwa kuku mweusi kichwani aliyetulia tuli bila kuanguka kwa kulewa dawa za kiganga tena ukiwa na mganga aliyejifunga kaniki ama kitambaa chekundu kiunoni.

Hayo yote tu ni kwa malengo ya kutatua matatizo yanayo kukabili ama kutafuta mafanikio fulani. Kama uko tayari kutekeleza hayo njia ni nyeupe kwa waganga.
 
Kuna na wale wanaotatua aidha matatizo ya kizazi ama kutuliza wapenzi kwa dada zetu. Ili dawa ikolee na kufika pahala husika, inambidi mtaalam apake dawa kwenye tupu yake halafu amuingize muhitaji tiba. Hapo ndipo dada, mama na wake zetu wanapoliwa na waganga. Kwa kifupi uganga ni usanii na mazingaombwe kuliko uhalisia.
 
Siti ya mbele kabisa kumsubiri Mshana
IMG_20200606_194250.jpg
 
Kuna na wale wanaotatua aidha matatizo ya kizazi ama kutuliza wapenzi kwa dada zetu. Ili dawa ikolee na kufika pahala husika, inambidi mtaalam apake dawa kwenye tupu yake halafu amuingize muhitaji tiba. Hapo ndipo dada, mama na wake zetu wanapoliwa na waganga. Kwa kifupi uganga ni usanii na mazingaombwe kuliko uhalisia.
Na kama ni msela je inakuwaje, au ndo kuliwa ndogo na mganga kwa hiyari yako mkuu...????
 
Hili ni somo zuri msisahau
 
Back
Top Bottom