Fahamu aina tano za tabia ambazo ukiziendekeza mpaka ikifika 2025 hutafanikiwa tena maishani

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Jamani leo katika pitapita zangu nilikutana na huu mjadala kuhusu maisha ya vijana na mafanikio kabla haijafika 2025.

Katika mjadala kuna utafiti umefanyika kwa vijana ambao wana umri kuanzia 26 hadi 35 ya kwamba kama mtu hizi tabia kama asipoziacha kipindi hiki ikishafika 2025 hatokuja kufanikiwa tena maishani.

1.TABIA YA KUIGIZA MAISHA AMBAYO SIO YAKO RASMI .

2.TABIA YA MTU KUTUMIA MUDA WAKE MWINGI KUCHUNGUZA NA KUZUNGUMZIA MAISHA YA WATU

3.IMANI POTOFU KWA VIJANA YA MTU AKIONEKANA AMEFANIKIWA BAADHI YA VIJANA HUAMINI NI FREEMASON,KAUWA WAZAZI, ANATUMIA UCHAWI .

4.TABIA YA KUTOKUPENDA KUFANYA KAZI LAKINI KUTUMIA MUDA WAO MWINGI KUFATILIA HABARI ZA WANASIASA, WASANII, MAMBO YA SERIKALI,

5.TABIA YA MTU KUPENDA KUSIFIWA NA KUTAFUTA SIFA ZISIZO NA MSINGI MITANDAONI HII NI KAMA VILE MTU KUPIGA PICHA UNAENDESHA GALI NA KUTUMA PICHA MITANDAONI UONE WATU WATA COMMENT

6.TABIA YA KIJANA KUJIONA YEYE NI BORA KULIKO WENGINE KISA UNA NDUGU ZAKO WAKO NAFASI NYETI SERIKALI HIVO KUWA NA TABIA YA KUTISHIA WATU MTAANI.

7.KUJINGIZA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI AMBAYO YAMEKUFANYA UMEKUWA MTUMWA WA MAPENZI AMBAYO MWISHO WA SIKU YATAGHARIMU MAISHA YAKO.

8.TABIA YA KUTOKUPENDA KUFANYA KAZI NA KUTEGEMEA NDUGU KISA WANA UWEZO.

9.TABIA YA KIJANA KUJIFANYA ANAJUA KILA KITU NA KUTOKUPENDA KUSHAULIWA.

10.TABIA YA KUKAA VIJIWENI KUZUNGUMZIA MAISHA YA WATU MTAANI .

SASA KAMA UNA MTU UNAEFAHAMU NI KIJANA ACHANE NA HIZI TABIA IKIFIKA 2025 ATAKUWA AMESHAANZA KUZEEKA NA UMRI UTAKUWA UMESHAENDA .
 
Tabia ya kushinda instargram, kudiscuss maisha ya watu waliofanikiwa badala ya kupiga kazi
 
Tabia ya kujifananisha na Freeman Aikaeli Mbowe wakati yeye mtaji aliukuta wa ulithi, labda na poda.
Mbowe angekua hajaoa kamanda ungepata wakati mgumu sana kuchagua mke kipindi hiki maana kuna vibinti vya Lumumba vikilala vinakuota wewe mzee wa anga.MTU unatokwa na povu tu ufikirii kinajadiliwa nini
 
Mtoa mada kwani wewe utafika 2025?
mkuu sina uhakika kama nitafika ila kama mkuu saivi una miaka 40 ina maana ikifika 2025 utakuwa na maisha 50,

hivo lengo la mada hii si kumtukana mtu bali kutufanya sisi vijana tusijisahau katika maisha
 
Acheni zenu. Maisha hayana formula
still 88 hapa una maana gani kusema maisha hayana formula .

kwa maana kama sasa hivi una miaka 30 hadi ikifikia 2025 utakuwa na miaka 40 hii ina maana kaka usije ukajisahau katika maisha coz hapa tupo katika kueleweshana tusije tukajisahau katika maisha
 
wazungu walivyosema time will tell hawakukosea ipo siku vijana tutakuja kujuta haya mambo tunayoyafanya baada ya kugundua hayana faida kama uko intagram siku hizi utasikia team wema, team alikiba, team diamond halafu huwa najiulizaga sijui ni kitu gani huwa wanakipata
 
Mimi kuna rafiki yangu mmoja huwa nagombana nae kila siku. Stori zake ni mishahara ya kina Ronaldo tu. Utackia hivi unajua lonado analipwa bilioni mbili kwa wiki wakati yeye hana hata buku.na hana hata mpango angalau wa kumtafuta mkwanja.tujiangalie sana wengine tunaweza tukawa tulizaliwa kusifia wengine.
 
Back
Top Bottom