Benchi la ufundi la Simba na wachezaji wabadilike sasa. Hii habari unakutana na timu unaweza kuifunga goli hata 10 halafu unafunga goli 3 unaridhika unacheza na jukwaa inajenga tabia mbovu sana kwa wachezaji na hata benchi lenyewe la ufundi. Na mbaya zaidi mpaka baadhi ya mashabiki maarufu imewaingia hii tabia kutwa kucha kusifia huko youtube pira biriani. Funga goli 10 halafu sasa anza back pass na pira biriani sio unatofauti ya kagoli kamoja halafu unaanza huo ujinga matokeo yake ndio hayo ya jana na Azam.
Na benchi ufundi la Simba limkumbushe Mohamed Hussein kuwa huwa anaharibu "move" nyingi sana za magoli kwa ile tabia yake ya kufika kwenye nusu ya timu pinzani halafu anaanza kurudi nyuma. Wakati mwingine anafika kwenye kibendera cha kona kabisa na washambuliaji wanasubiri krosi yeye anageuka nyuma. Siku hizi sijui kalogwa maana zamani hakuwa hivyo kabisa. Ajifunze kwa mwenzake Kapombe na hata Nouma namna wanavopiga krosi hata wakivuka tu mstari wa kati tu ilimradi wawaone washamvbuliaji wapo kwenye eneo zuri..