Facebook Waanza Kuverify Pages

Given Edward

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Posts
850
Reaction score
203
Rais Kikwete mwenyewe kakutumia friend request?Sasa hivi mbona utajua kwa urahisi tu, shukrani kwa feature mpya ya Facebook : Verified Pages.

Kama ilivyo kwa verified accounts za Twitter, verified Facebook pages zitakuwa zinawekewa alama ya tiki ya blue pembeni mwa jina la page hiyo. Alama hiyo pia itaonekana pembeni ya jina la page hiyo kwenye search results, na kwingine kotote ndani ya Facebook.




Pia, kama ilivyo kwa Twitter, verification haitatolewa kwa kila mtu. Verified accounts zitatolewa kwa watu mashuhuri wenye mashabiki wengi kama vile, celebrities, viongozi wa serikalini, bidhaa kubwa/maarufu and waandishi wa habari maarufu wachache.

Hii feature imeanza rasmi mwezi uliopita. Hivi karibuni viongozi na wasanii mbali mbali wamekuwa wakilalamika watu kutumia majina yao kufanya utapeli na kuwalazimu kupata usumbufu wa kutangaza kila sehemu accounts zao official ili kuepusha mchanganyiko.

Kwa viongozi nadhani rahisi kuwa verified ila kwa wasanii you have to be like really international ili uwe verified, kama ilivyo Twitter.

Facebook wamesema wataanza kufanya verification automatically kwa pages maarufu zinazofanyiwa duplication sana, then kwa pages nyingine (nadhani) itabidi utume request ya kufanyiwa verification.
 
Dah??? Umetumia Request Na Mheshimiwa raisi Af Unaipiga Na screenshot Kambla Huja Accept Ili Ujigambe kitaaaaa... kumbe Akaunti Fekii........ inauma Sanaaaa
 
mpka sasa kwa tz ambaye anatumia verified account ni flaviana matata ninaye mfahamu mimi kuna mwingine kweli..
Nadhani unaongelea Twitter kwa sababu Flaviana bado hajawa verified Facebook ila kawa verified Twitter. Na pia, hata Twitter kuna watanzania wengine ambayo wameshakuwa verified. Miongoni mwao ni:

1. Rais Jakaya Kikwete


2. January Makamba


3. Tigo Tanzania


4. Ambwene Yessayah (A.Y)
 
Ilianza muda mrefu lakini ilikuwa open kwa US pekee for pilot purposes. Mwezi uliopita ndio ilifunguliwa global.

wanatumia vigezo gani kuverify? na kama nataka kuwa verified nafanyaje? (watu gani wana qualify kuwa verified? usiniambie ukiwa celeb tu inatosha) 50cent na Juma nature wote ni maceleb
 
wanatumia vigezo gani kuverify? na kama nataka kuwa verified nafanyaje? (watu gani wana qualify kuwa verified? usiniambie ukiwa celeb tu inatosha) 50cent na Juma nature wote ni maceleb

mkuu facebook ni wasiri vigezo vyao hawajaviweka public na kuna verification ya vitu viwili.
1.profile
2.pages

kwa profile hapa watakua wanaangalia kama ni wewe au la. mfano huyu ni raisi kikwete au sie? possible kuwe na vitambulisho na vitu vifananiavyo.

kwa pages hapa watakua wanaangalia popular brands hapa verification itaenda kwa page likes. mfano mtaawasaba pale tunapata like kama milioni hivi unafkiri fb wataacha kutuekea kitiki cha verified?
 
wanatumia vigezo gani kuverify? na kama nataka kuwa verified nafanyaje? (watu gani wana qualify kuwa verified? usiniambie ukiwa celeb tu inatosha) 50cent na Juma nature wote ni maceleb

mkuu Hapo sawa Unasema Saccos Na Barclays Zote ni taasis Za Fedha.... Ila zna level tofaut.... Ila mbona twitter wame mveryfy ay... mayb Hata kina Dogo aslay Watakua Verified
 
Kwa Facebook ili kua Verified bado sijajua unafata utaratibu gani.
Ila kwa Twitter ili kua Verified ,kigezo kikubwa ni Account yako kua connnected na official website yako (verification ni kwa public figures tu) . .na hapo kwa wabongo walokua verified umemsahau Hasheem Thabeet mkuu!
 
Mbona Jamii forums wanazo verified accounts? Tuthamini vya kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…