Experience is better than Knowledge

A man with one idea

Senior Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
125
Reaction score
269
"Dunia ya leo elimu inabadilika sana, na mifumo inabadilika sana, kwahiyo usiseme mimi nilimaliza chuo mwaka 2000 nina digrii, na mtu anayeingia kazini leo 2022 hamfanani"

"Cheti kinaweza kikakufungulia mlango lakini ujuzi ndio unaofanya kazi, mimi nikitafuta mfanyakazi natafuta mtu anayeweza kufanya ile kazi, kama ana cheti na hawezi kufanya kazi hanisaidii chochote"

"Cheti kisikufariji sana kwa sababu kazi zinabadilika mno, kwahiyo lazima ujue una cheti ila hujamaliza kujiboresha"

"Ukijitolea mara nyingi ni maamuzi ya yule anayekupa hiyo kazi, kwahiyo usiende kudai haki, haki yako wewe ni kupata zile skills ambazo unataka, kwahiyo unatakiwa uende ufanye vizuri na mara nyingi ukifanya vizuri hutakaa miaka mitatu"

"Kuna watu ambao wapo specific amesoma uhasibu kwahiyo anatafuta kazi ya uhasibu tu, sahau hilo karne hii hatupo, uwe tayari kufanya chochote"

- Alex Shayo, Mkurugenzi wa Tanzania Institute of Managers #EastAfricaRadio #SupaBreakfast
 
Tittle inasema experience is better than knowledge ila content inazungumzia experience is better than cheti.

Now inabidi tukubali kua cheti sio knowledge. Knowledge ni muhimu, inamfanya mtu awe mbunifu na mweledi. Inaondoa halin ya kufanya kazi kwa mazoea.

Mtu mwenye experience ana nafasi ya kufanya mambo kwa mazoea na matokeo yake yanakua yale yale siku zote maana hakuna ubunifu na new inputs kwenye kazi.

Mtu mwenye maarifa atabuni namna mpya za ufanyaji kazi, ataboresha zilizopo ili ziweze kuleta tija zaidi kwenye kazi.

Kwa hiyo, kwa mtizamo wangu, knowledge ni muhimu, experience ni ,muhimu, unexperienced person mwenye knowledge akiwa exposed kwenye mazingira sahihi na kama ana asili ya kupush, anafika mbali sana.
 
Napenda kujua Speshalist vs Generalist hii vita inaendeleaje katika dunia ya Sasa.
Sasa hivi unatkiwa kuwa multipurpose kushinda vita .ukisema Mimi ni mwalimu wa kiswahili nasubiria shule ya kufundisha kiswahili tu hautoboi ,search challenge any where badae ukishapata skilss unakaa hukohuko .Dunia iko kasi
 
Oky.ila kwà sasa Cheti ,sijui vibanda sio issue issue ni unajua nini?
 
Sio kwa sasa. Siku zote imekua hivyo. Cheti kiendane na utendaji. Mara nyingi elimu yetu ya bongo, tunachosoma darasani hua sio sawa 100% na tunachoenda kufanyia kazi, labda tuseme 50%.

Lakini atakaekua vizuri kazini ni yule aliegrasp vizuri shuleni, akapata na elimu nyingine akiwa anafanya kazi, mwepesi wa kufundishika, anaejiongeza, anaejisomea na kujifunza mwenyewe, mwenye kumbukumbu na mwenye bidii ya kufanya kazi kubwa ndani ya muda mfupi.

Ndio maana huko maofisini, muhindi anaweza fanya kazi mara mbili ya atakayofanya mbantu kwa muda ule ule.

Kuna wakati nilikua nafanya internship kwenye hospitali moja. Tulikua tunafanya kazi ya data entry kuna muhindi alikua anaruhusiwa kuondoka saa nane kamili mchana ila wengine wanafanya hadi saa 11. Sababu ni kua, kazi anayofanya muhindi kwa masaa nane, ni mara mbili ya kazi anayofanya mmatumbi kwa masaa 12.



Oky.ila kwà sasa Cheti ,sijui vibanda sio issue issue ni unajua nini?
 
Sio si unit so be subjective
 
Vipi suala la connection mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…