naumbu
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 4,717
- 8,080
Merry Xmas wanajamii! Nina kero na hii Bank ya Exim kama imechoka kufanya biashara isijitangaze,hii Bank Ina ATM chache na hizo hizo nyingi unakuta hazifanyi kazi.Jana watu walikua wanazunguka jiji la Dar kutafuta ATM ambayo inatoa pesa lakin mpaka imebidi tufanye alternative nyingine za kupata hela za Xmas Wametoa mastercard lakini ukienda kwenye ATM za Bank zinazokubali visa na MasterCard unaambiwa hamuwezi kufanya muamala sababu Bank yako hairuhusu na Muda mwingine unakatwa hela wakati haijatoka,kuipata tena hiyo hela ni siku 20 had 45 baada ya kujaza fomu ya malalamiko.Ingawa huu ni mwezi wangu wa mwisho kuwa mteja wenu ila nawaambia kuweni serious ushindani ni mkubwa na hiyo customer care yenu ni mbovu especially hilo tawi lenu la Shekilango wanahudumia kama wamelazimishwa au mnawalipa hela ndogo?