EWURA imezifutia leseni Kampuni tisa za mafuta

EWURA imezifutia leseni Kampuni tisa za mafuta

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,060
Reaction score
64,209
images

WAFUTIWA LESENI: Mamlaka ya Udhibti wa Maji na Nishati EWURA yazifutia leseni Kampuni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla kampuni tisa hapa nchini, yasema zimekiuka masharti ya biashara.
------------------------



BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imefuta leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla (Whole Sale Licenses) kwa Kampuni tisa (9) zinazojihusisha na biashara hiyo hapa nchini.
Uamzi huo umefanywa leo (29.4.204) katika kikao chache cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, Bw. Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa leseni hizo kumetokana na ukikaji kwa sheria na kanuni za biashara hiyo.
Bw. Ngamlagosi katika taarifa yake, alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa leseni hizo na EWURA.

Kampuni zilizofutiwa leseni ni pamoja na Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeundwa chini ya sheria ya EWURA, sura namba 414 ya Sheria za Tanzania. EWURA ina majukumu ya kusimamia shughuli za udhibiti, kiufundi na kiuchumi katika sekta Nne (4) za Petroli, Umeme, Gasi Asili na Maji Safi na Maji Taka.

IMETOLEWA NA
BW. FELIX NGAMLAGOSI
MKURUGENZI MKUU
EWURA
 
Mkuu taja hizo kampuni kwa majina vinginevyo tarifa yako inakosa mambo ya msingi.
 
images

WAFUTIWA LESENI: Mamlaka ya Udhibti wa Maji na Nishati EWURA yazifutia leseni Kampuni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla kampuni tisa hapa nchini, yasema zimekiuka masharti ya biashara.
Mkuu kampuni gani hizo?
 
Kobil na Lake Oil haziwezi futiwa leseni kwa kuwa ni za magogoni
 
Zitaje mkuu, kama kati ya hizo lake oil haipo ctaelewa mana hawa wanafanya biashara bila leseni kwa miaka sasa, wanakwepa kodi kwa asilimia 100, kama hawamo ctaelelwa kabisa.
 
Zitaje mkuu, kama kati ya hizo lake oil haipo ctaelewa mana hawa wanafanya biashara bila leseni kwa miaka sasa, wanakwepa kodi kwa asilimia 100, kama hawamo ctaelelwa kabisa.

Mkuu hapo hapaguswi kabisa yaani kugusa hapo ni sawa na kuupiga kwenzi mkuki nchani.
 
Kwanini jamani ile inayoitwa Panone isifutiliwe mbali?

Ngoja tuone kama haki inatendekaga hapa Nchini!
 
Kama ni hivi hii biashara ya mafuta ina hela sana. Maana kila mwezi wanapeleka TRA Bil.9. halafu tunaambiwa wanakwepa kodi kwa 100%!!!?? wangelipa hiyo 100% inayosemekana inakwepwa hii nchi ingekuwa ya maziwa na asali.
Zitaje mkuu, kama kati ya hizo lake oil haipo ctaelewa mana hawa wanafanya biashara bila leseni kwa miaka sasa, wanakwepa kodi kwa asilimia 100, kama hawamo ctaelelwa kabisa.
 
Kama ni hivi hii biashara ya mafuta ina hela sana. Maana kila mwezi wanapeleka TRA Bil.9. halafu tunaambiwa wanakwepa kodi kwa 100%!!!?? wangelipa hiyo 100% inayosemekana inakwepwa hii nchi ingekuwa ya maziwa na asali.

Ni kweli wangelipa kodi wote kihalali huyu manyakazi ambaye hawez kukwepa kodi angeona ahueni ya maisha. Kuna watu wanafanya biashara hii bila leseni na hivyo hawalipi hata sh 1 TRA. Ni ujanja tuu, unalipia moja kati ya kumi, tisa zinaendeshwa bila leseni wala kulipa kodi.
 
Waulizwe akina ndugai waloendesha biashara za mafuta dodoma bila kulipa kodi kwa miaka wakiulizwa wanaanza kukuweka kwenye plot list tu
 
images

WAFUTIWA LESENI: Mamlaka ya Udhibti wa Maji na Nishati EWURA yazifutia leseni Kampuni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla kampuni tisa hapa nchini, yasema zimekiuka masharti ya biashara.
------------------------

naona prnce anazdi kuujumu makampuni mengne ili afanye biashara vzuri na kampuni zake za puma oil na lake oil /gas....alianza kuhujumu Gapco sasa kahamia kampun nyngne
 
Back
Top Bottom