Furaha Yako isipotoka Kwa mkeo au Kwa mumeo umeingia kwenye ndoa kufata Nini?
Unless kama unataka kusema watu wasioe Wala kuolewa. Ndoa ni zaidi ya tendo la ndoa na kama hitaji ni tendo la ndoa tu mbona yanapatikana mengi tu nje huko, ila je ndio dhamiri za mahusiano hizo?
Usipopata Furaha Kwa mumeo au mkeo utaipata na kuitafuta Kwa mchepuko.
Asante kwa mtazamo wako mkuu. Lakini unafikiri ndoa ni furaha kila siku. Hujui kama ndoa ina majira. Mungu tu alieumba dunia aliweka majira makusudi ndo itakuwa ndoa.
Watu waingie kwenye ndoa wakijua pia shida, tabu, mateso yapo. Kama kusingekua na mateso tusingeapa katika shida na raha. Shida ziko palepale. Aliye single na aliye kwenye ndoa wote wana tabu tu.
Ukiwa hujaolewa utachezewa na karaha za kutokupewa pesa mpaka uvue chupi. Ukiolewa mtu anaweza achelewe kurudi au hata kakasirishwa huko atokako labda ni kazini lakini joto ukalionja wewe.
Duniani dhiki tu furaha mbinguni. Kama mtu hana utayari na ukomavu wa moyo kuingia kwenye ndoa na asiingie. Kwa sabbu tabu iko palepale. Ndugu tu nyumbani kuna misuguano ndo mtu mliekutana nae utu uzimani. Marriage aint a joke..huo ndo ukweli.
Bado dada hujakutana na mwanaume tayari alishazaa watoto wawili nje afu we ndo unachaguliwa kuolewa na hao watoto ukae nae. Imagine uchelewe kupata mtoto, afu bado unawalea hao. Ukiwafinya au kuwakanya unashangaa mawifi, mama mkwe au hata mama za hao watoto wanakusakama "au kisa hujazaa". Hata kama watoto unawalea kwa upendo. Tena na matusi juu. Na wewe umewapenda na kuwalea vizuri tu. Au yumkini watoto wengine wamepatikana ndani ya ndoa. Mme katika tembea tembea kakuletea hao apo. Na unatakiwa unyamaze tena ulee kana kwamba ni wa kwako. Bila strong mentality hakika utafia jangwani mpendwa. Kweli nakwambia.
Vidada vya siku hizi blue tick tu roho inataka kukutoka shosti. Unaanza kuona hupendwi. Na hivyo mamotiveshen spika walivyojaa. Unakutana na meme "hakuna mtu anaekosa muda kwa mpenzi wake". Shoga unaibeba jumlajumla unaanza kuona huyu hanipendi. Unamuacha na hapo kashakukula sana. Mwanaume hana cha kupoteza. Wewe sasa. Ndo unajikuta muda unaenda tu. Kisa mind games. Blue tick tu...roho juu. Je akirudi saa tisa usiku utahema wewe. Asiporudi siku tatu je..naongea na wewe dada angu. Jipange sawasawa dunia ishavaa chupi. Kula vizuri..ridhika, fanya kazi hata upate 5000 yako tu kwa siku, ishi maisha ya level yako sio social mediaz(usione wenzako vikoba na wewe umo) kumbe huna uwezo. Utat***wa sana nje. Sali sana, toa sadaka, penda sana(upendo) then funga pia, fanya mazoezi...jiweke busy, akili yako ishughulishe..kamwe hutateseka dunia hii. Ila ukikaa kumchunga mtu mzima...heheee