Evolution nyingine mbaya zaidi kutokea; inayotokea sasa.

Aputwike

Senior Member
Aug 9, 2016
172
189
Hakika kusipofanyika juhudi, siku moja binadamu atazaa nyoka. Evolution hizi zinatupeleka negative badala ya postive, husasani jamii ya kiafrika.

Zamani ulikuwa ili uone makalio ya mwanamke ilikuwa shurti ufunue chupi, lakini sasa ili kuona chupi ni lazima upanue makalio. Dada zetu watohoa utamaduni wakimagharibi wa kutuvalia kamba utadhani wanajinyonga sehemu za siri.

Unakuta li-brothermen limevaa mlegezo na li-boxer lake li-chafu limeshuka hadi mfereji wa panama unaonaonekana ulivyo mchafu alafu lipo ndani ya daladala nyuma wapo mama zake. Ushenzi mtupu!

Unakuta likaka jitu zima limenyoa kiduku utadhani licheza show la Akudo. Saizi hata vidada navyo hamnazo kabisa, vinanyoa viduku utafikiri vipanya road. Muonekano wako ndio unaotoa tafsiri ya tabia yako.

Unakutana na li-dada limevaa majani ya wazungu kichwani(mawigi) ili lionekane kama Shakira, tena saizi yanaweka na rangi utadhani kicha cha mbu. Hata ule muonekano wa asili unapotea libaki kuwa kama jini. Tena ukute limejipaka na zile rangi zao kwenye macho, looh, unaweza ukimbie kabisa. Pendeni uhalisia wenu, basi jaribu kufuga nywele zenu ziwe ndefu ili mfanane na Shakira.

Uakuta lijitu na lidemu lake wameweka picha mitandao ya kijamii wananyonyana denda. Mijitu kama hii ni milimbukeni. Inataka kuchukua mambo ya chumbani kuyaleta hadharani. Tunakoenda tutaja ona mambo ya ajabu.

Zipo nyingi, ila waafrika tumekuwa limbukeni mno.
 
Kudadadeki, kama wana majibu watwambie ila Rika zote za wanawake na wanaume hususani vijana, hatari
 
Ki ukweli mimi napenda mwanamke awe natural asuke tatu kichwa,kilimanjaro au twende kilioni au hata sangita siyo mbaya,lakini wigi sijui human hair sijui na utumbo gani yaani mwanamke hata awe mzuri zaidi ya malaika lakini akishaweka hayo mavitu kichwani yaani namuona kama jini,sijui mawanja ,malipstick aisee tunawapenda wanawake mkiwa natural msitufanyie hivyo
 
Back
Top Bottom