Eti JPM anakandamiza Demokrasia!! Kweli Wapinzani wamefilisika kabisa!

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,854
1,776
Enyi wapinzani, ni nani aliyewaroga? Hata msijue kwamba kuna Serikali na kwamba taratibu za kiulinzi na Kiusalama ni muhimu zaidi kuliko haki yenu ya kukusanyika na kuzomea?? Ina maana mngetawala ninyi mngeacha mambo yaende kiholela na kwamba watu wangejichukulia sheria mkononi, wasingeheshimu Mamlaka zilizopo, wangefurahi kuona Viongozi wenu wakitukanwa na wakosaji kuchangiwa faini Mahakamani??? Majizi yangeachwa yatambe na kupigiwa makofi kwa kuifilisi Nchi? Wazembe kazini wangeshangiliwa chini ya Serikali yenu ya UKAWA? Ndio UKAWA hiyo? Kama ndivyo, hatuwachagui UKAWA MILELE!!

Kama hicho ndicho mnachokusudia kufanya mkipata madaraka, basi ni bora msiende kabisa Ikulu milele na milele , Amina!!
 
True......serikali ya awamu ya 5 ni subscribers wa falsafa ya "the end justifies the means"...
kama "good intention" dictatorship ndo itatufikisha kwenye nchi ya ahadi, basi tutatumia hiyo approach, hata kama ni chungu
 
Enyi wapinzani, ni nani aliyewaroga? Hata msijue kwamba kuna Serikali na kwamba taratibu za kiulinzi na Kiusalama ni muhimu zaidi kuliko haki yenu ya kukusanyika na kuzomea?? Ina maana mngetawala ninyi mngeacha mambo yaende kiholela na kwamba watu wangejichukulia sheria mkononi, wasingeheshimu Mamlaka zilizopo, wangefurahi kuona Viongozi wenu wakitukanwa na wakosaji kuchangiwa faini Mahakamani??? Majizi yangeachwa yatambe na kupigiwa makofi kwa kuifilisi Nchi? Wazembe kazini wangeshangiliwa chini ya Serikali yenu ya UKAWA? Ndio UKAWA hiyo? Kama ndivyo, hatuwachagui UKAWA MILELE!!

Kama hicho ndicho mnachokusudia kufanya mkipata madaraka, basi ni bora msiende kabisa Ikulu milele na milele , Amina!!
Serikali inazo hizo taratibu za ulinzi na usalama lakini ziambatane na Katiba ya nchi. Kinacholalamikiwa ni ile demokrasi ya (ccm) kufanya shughuli zake kuwa ni halali. Wakati huo ni haramu kwa UKAWA kufanya harakati zake eti mpaka ipite miaka mitano ?!. Ukweli uko wapi hapo ?!.
Pili Bungeni upinzani pamoja na uchache wao lakini michango ipo kisheria na kikanuni lakini Dr Tulia alikoelekea ni kulizima bunge na kubaki na ndiooooooo bila changamoto za kuipinga serikali ktk mipango mibovu.

Na kuhusu kuwachagua hata usipowachagua kuna sehemu kubwa ya wananchi waTz wanawakubali na kuwachagua . Kwa hiyo usiseme sisi sema wewe
 
Mleta mada laiti kama Lumumba wakikuvua hilo boga walokutwisha wakakurudishia kichwa chako. Unaweza ukajidharau sana,
 
Back
Top Bottom