Eti hatoki mtu hapa!! Watu tunatoka

Eti hatoki mtu hapa!! Watu tunatoka

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,521
Reaction score
96,267
Tangazo la Airtel la Hatoki mtu hapa, naona wanajidanganya kwa sababu wateja wengi sasa hivi wanahama kutokana na hao kuongeza tarrif charges zao na kutowajali wateja ktk kitengo chao cha huduma kwa wateja.
 
huu ni mtandao fake toka zaman,sema wabongo wepec wa kusahau,yako wapi sasa,eti oh akatwi mtu hapa!?
 
Ukilinganisha na voda au tigo ni bora hao . Nimetoa elf50 jana wanakta kidog ila wakipandisha natoka
 
Ukilinganisha na voda au tigo ni bora hao . Nimetoa elf50 jana wanakta kidog ila wakipandisha natoka

Kaka kuna vifurushi unanunua vinaitwa bure pack vinakuwezesha kutuma na kutoa hela bure wiki nzima bila makato kwa mitandao yote
Bonyeza *150*60#
Kisha chagua namba 3 ujiunge na bure pack inacharge 1500 kutuma na kutoa hela wiki nzima bure
 
Hakuna wa kushindana na Airtel. Kwanza wametupa huduma ya bure kama miaka 2. Makato yapo fresh sana.
 
Airtel, mnazingua kwenye vifurushi vya internet, mko gharama sana
 
Airtel ni baba lao. Hakun a wa kushindana na Airtel Tanzania nzima. Amia leo AIRTEL
 
Mitandao ya cm wote wanamambo ya kihuni ila Airtel wana nafuu kiasi hao waliobaki majanga matupu hawafai kabsa.
 
Mimi sinaga mkataba wa kudumu na mtandao wowote nafuata hali ya soko zaidi.
 
Kaka kuna vifurushi unanunua vinaitwa bure pack vinakuwezesha kutuma na kutoa hela bure wiki nzima bila makato kwa mitandao yote
Bonyeza *150*60#
Kisha chagua namba 3 ujiunge na bure pack inacharge 1500 kutuma na kutoa hela wiki nzima bure
Hakuna mtu anayetoa hela kila siku.
 
Ngoma ipo kwa customer care wao ni jeuri sana, wanamajibu ya hovyo sana, alafu hadi kuwapata unaweza kupiga saa mzima huja wapata.Nivema uongozi ufuatilie mapungufu ya staff yao.
 
Back
Top Bottom