GE2025 Esther Matiko aamsha matumaini Tarime Mjini

GE2025 Esther Matiko aamsha matumaini Tarime Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
403
Reaction score
676
Na Brighton Masalu

MGOMBEA ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Tarime Mjini, Esther Nicholas Matiko ameonesha dira thabiti ya maendeleo na kufufua matumaini kwa wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza na halaiki ya wananchi waliohudhuria kwa wingi mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi uliofanyika Tarime Mjini, jana Agosti 31, 2025, Esther Matiko alinadi kwa ufasaha sera na mlengo yakinifu wa CCM kwa wananchi wa Tarime Mjini.

Akishangiliwa kwa nderemo, mbinja, vifijo na furaha wakati wote kutoka kwa wananchi, Esther Matiko alitumia nafasi kueleza ni sababu gani zimempelekea kujiunga na CCM.

"Kuna watu bado wanajiuliza, hivi kweli Matiko amejiunga na CCM?, nataka niwahakikishie ndugu zangu pasina shaka kwamba, mimi ni mwanachama halali na halisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Kazi kubwa iliyofanywa na CCM chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia Watanzania, ndio chachu iliyonifanya nijiunge na CCM na ninajisikia amani, furaha na faraja kubwa sana kuwa CCM," alisema Esther Matiko.

Akiainisha baadhi ya vipaumbele muhimu kwa kufuata misingi ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Esther Matiko alisema atazidi kujikita katika kuzisemea na kuziwakilisha kikamilifu shida za wananchi wa Tarime Mjini.

"Siku zote nitajikita katika kutatua changamoto zinazotukabiri sisi wananchi wa Tarime Mjini, ni bahati kwamba Serikali ya Dkt. Samia ni sikivu na inaguswa na shida za wananchi, hivyo ni rahisi sana kukabiliana na changamoto zetu.

"Naomba wananchi wenzangu wa Tarime Mjini na sehemu mbalimbali nchi nzima, muendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwani ndicho chama pekee chenye dhamira ya kweli katika kuleta maendeleo kwa wananchi," alisema Esther Matiko.

Katika hatua nyingine, Esther Matiko alionesha kutokuwepo kwa makundi ndani ya chama huku akiwashukuru walikuwa wagombea wenzake kupitia CCM, akiwemo mbunge aliyemaliza muda wake, Michael Kembaki.

Awali, akizungumza na wananchi wa Tarime Mjini kabla ya kumkaribisha mgombea ubunge wa jimbo hilo, Esther Nicholas Matiko, Balozi Dkt. Nchimbi alisema;
"Miongoni mwa wanasiasa wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja nzito ni pamoja na Esther Nicholas Matiko, hakika huyu ni mtu potential sana na hapa mmepata bahati kubwa sana kuwa na mgombea huyu.

"CCM tunachukua wenye akili wote, kwa hiyo ndugu zangu wa Tarime Mjini Esther Matiko anawafaa kwa kila namna".

Aidha, Dkt. Nchimbi alitumia mkutano huo kuwaomba wanachama wote wa CCM Tarime Mjini, kuungana na mgombea Esther Matiko huku akimuagiza aliyekuwa mbunge, Michael Kembaki kuongoza na kuratibu kampeni za Esther Matiko (Campaign Manager), ambaye alitii maelekezo hayo.

Esther Nicholas Matiko amekuwa mwanasiasa mahiri katika kutetea, kuwakilisha na kuzisemea shida za wananchi wa Tarime Mjini na Tanzania kwa ujumla, ndani na nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Esther Nicholas Matiko, aliingia Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2010, akiwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mwaka 2015 alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, kupitia Chadema, akiwa Mbunge wa kwanza mwanamke wa jamii ya Kikurya kuwakilisha jimbo la uchaguzi.

Mwaka 2020 hadi 2025, alikuwa Mbunge wa Viti Maalum na sasa amechaguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupeperusha bendera ya Ubunge wa Tarime Mjini.

maxresdefault.jpg
 
Uyo Dada ni Jembe kweli kweli kazi kipimo cha utu.
 
Back
Top Bottom