Sikubaliani na wazo hilo. Hao ni wahalifu na lazima pesa waliyoiiba irudishwe na wahalifu hao kufikishwa mahakamani....wote bila kujali mtu. Utawala bora ukija uhakikishe hilo kwa sababu makosa hayasauliwi, hayasamehewi, hata ichukue miaka mingapi.
Nashauri tu. Naweza kukubaliwa au kukataliwa kwa kupondwa bila ya kupendwa. Kukandiwa kuwa nami nimechotewa. Nipo tayari kuwasilisha tu ushauri wangu. Nashauri kuwa suala la Escrow tuachane nalo,tufanye mambo mengine.
Hili limekwama. Zitapigwa sarakasi hadi watu wavunjike migongo. Na watazamaji wajawe na huruma na usingizi. Mkwamo ulianza Bungeni na hadi lilipo.
Tuachane nalo. Likibidi libaki mioyoni na vichwani mwetu tu. Tuamue kimyakimya. Tuacheni jamani. Vichwa vitauma;midomo itauma;mioyo itakwenda mbio na kadhalika.
Escrow is extremely complicated. Limekwama.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hapa kaka ni kusubiri mpaka Mkulu atoke maana yeye ndiye aliyeratibu,akaidhinisha,akalipwa, na akawapa wengineili kuwafunga midomo.
Sasa kesi ya NYANI utampa ngedere kweli?Kwa sababu mnufaikaji wa kwanza ni MKULU ndiyo maana Mzee Tupatupa katuambia bora tunyamaze tugange yajayo.
Ukifika wizi mwingine tutapiga kelele yataisha,utakuja mwingine vivyo hivyo.Cha msingi wenye pesa zao wandelee kuzifungia mpaka VIONGOZI wetu wapate akili ya kujua mema na mabaya.
Hii bado mkuu tunatafuta Formulation
Kwa kuwa tuna mgogoro na mhimili wa mahakama.
Saizi ndiyo nimegundua hii issue ya Escrow ni zito sana.
Nashauri tu. Naweza kukubaliwa au kukataliwa kwa kupondwa bila ya kupendwa. Kukandiwa kuwa nami nimechotewa. Nipo tayari kuwasilisha tu ushauri wangu. Nashauri kuwa suala la Escrow tuachane nalo,tufanye mambo mengine.
Hili limekwama. Zitapigwa sarakasi hadi watu wavunjike migongo. Na watazamaji wajawe na huruma na usingizi. Mkwamo ulianza Bungeni na hadi lilipo.
Tuachane nalo. Likibidi libaki mioyoni na vichwani mwetu tu. Tuamue kimyakimya. Tuacheni jamani. Vichwa vitauma;midomo itauma;mioyo itakwenda mbio na kadhalika.
Escrow is extremely complicated. Limekwama.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hukunisoma vizuri, nimesema utawala bora ukiwepo washughulikiwe. Tunaona mpaka siku za karibuni wauaji wa Nazi wa Hitler wakisakwa na kuhukumiwa kwa makosa waliyoyafanya miaka 1945!! Inawezekana kabisa kuwatia hatiani kama nia ipo!
Nasisitiza tuachane na masuala ya Escrow
Mzee Tupatupa
Saizi ndiyo nimegundua hii issue ya Escrow ni zito sana.