Escrow: Kumbe PAC walituingiza choo cha sokoni (Part I)

Go away! Njia pekee ya kumaliza ujambazi huu ni kwa fedha zetu kurejeshwa na wahusika kutiwa nguvuni
 

si nasikia ruge ukiachia plot hajatoa hata sent kuchangia mtaji wa iptl?
 
mleta mada hapa kaua bend,hapa hata lisu lazima jasho litoke
 

Hata kama unavyo urge ni kweli, lakini bado hujajenga hoja kwa nini TEGETA ESCROW sio ufisadi ila ni malipo halali. Kwa nini PAC iligushi nyaraka za usajili?Kwa nini watu walipwe pesa na wote na watumishi wa serikali (mawaziri, mawaziri au wabumge wastaafu, majaji nk), kwa nini pesa itolewa haraka haraka katika account na pengine account hizo kufungwa? Na kubwa zaidi, tunajua Seth alikuwa katika scandal ya Kenya ya Goldenberg, tena katajwa safari nyingi sana na report ya wikileak. Iweje FISADI tena mkubwa hivi aruhusiwe kuwekeza kwa mradi sawa na ule ule alo fanya Kenya?Maswali ni mengi sana, ambayo kwayo tu bila hata uchunguzi wa CAJ na PAC akili hata ya mtoto inaelewa kuna ufisadi hapa. Ilichotusaidia kamati ya Zito ni details tu basi.
 
Hapo tumedanganywa hapa huwezi kumuona Tumbiri wala Nyepesi kujibu hoja hizi
 

Mbona mnakuwa kama akili hizipo sawa? Ww unafikili takukuru,CAG,POLICE na bunge wamedanganya?acha kupotosha umma wewe kama una babayako subili utalidhi ujinga badae tuachie kwanza hil taifa cc umoja wa katiba ya wananchi.
 

hata mje na facts zaaje ukweli utabaki kuwa j.kikwete amewalinda wezi walokwapua mabilioni ya umma na wakagawana kama njugu.
Na mbaya zaidi wengine wakabeba kwenye kifuko ya sandalusi!
<<<ikiwa ag alibainika kukiuka taratibu za ushauri wa kifedha basi hata mchakato mzima wote ulikuwa ni kharamu!
 
where did the escrow fund go? hili ndo swali
 
Nilicho jifunza katika matukio kama EPA, Escrow, Richmond, Tan Gold nk, si police, TISS wala chombo chochote cha ulinzi kilichowahi hata kunusa, yote is either vyombo vya habari au wapinzani; to me hawa ndio wanaongoza nchi.
 
Sitaki kuamini kuwa ripoti nzima itakosa uhalali kutokana na kasoro hii ila nachoamini ni kuwa kunahitajika ufafanuzi kidogo tu au kufanya marekebisho ya kiuandishi tu.

hoja kwamba hakukua na ISCID -2 ndo ishu
 

Hii itakuja kuingia kwenye historia. Kwamba mfanya biashara anayefanya biashara "halali" analipwa hela zake kisha anaamua kugawa mabilioni na mamilioni kwa Watendaji wakuu wa serikali mawizarani, RITA, Ikulu, makanisani, TRA na kwingine lakini wote waliofanikisha fedha hizo kutoka.
Huyu ndiye Mfanyabiashara "mwema sana" kuliko hata Bill Gates. Hivyo ndio wanavyotaka kutuaminisha. Sawa, sisi kama Watanzania wanaweza kutulazimisha kukubali kuwa huo ndio ukweli wenyewe lakini ABADANI hilo haliwezekani kwa wale wahisani wanaokusanya kodi kwa raia wao ili kipatokane cha kutupatia sisi kuendesha serikali yetu. Hawatakubali hizi ngonjera.
Hii ni sawa na issue ya RADA, walituambia tunaibiwa sisi tukasema hamna kitu kama hicho. Wakafuatilia na fedha ikapatikana na kuamriwa irudishwe. La ajabu bila aibu eti tukaiita CHENJI YA RADA na bila aibu majadiliano yakatinga Bungeni kubishania jinsi ya kupanga matumizi ya fedha hizo huku tukishindwa kuwafanya kitu wahusika zaidi ya kuwapa vyeo vya wenyeviti wa kamati ya bajeti ili wazipangie bajeti fedha za Chenji ya rada.
Kuna wakati utafika hapa duniani mtu akitaka kukutukana anasema " Wewe mjinga kama Mtanzania!"
 

Hiki ndicho kinachofanyika kwa sasa. Na ni bahati mbaya sana falsafa hii imeshavamia hapa JF kwa nguvu kubwa na watu wako kazini.
 
rushwa ili apate nini ili hali yeye kauza hisa zake?
 
au labda siku hizi ukitaka kuuza hisa mpaka utoe rushwa labda
 
Watanzania tulikua wajinga na wapumbavu kwa kiasi kikubwa. Sasa wajinga wameanza kupungua na ipo siku wataisha kabisa na Tanzania ya waerevu na wazalendo itazaliwa. Hili ndilo mleta mada na CCM hawalioni. Hawaoni mabadiliko yalivyo na kasi katika nchi hii, washinda na kulala wakizania wataendelea kututawala kwa ujinga wetu. Na Mungu atakua upande wetu kwani hatawaamsha hadi pale watakapoanguka.

KIM KARDASH ngoja niamini kuwa haya uliyoyaandika ni mashiko kweli na hivyo fedha zote ni halali kwenda IPTL kama unavyotaka tuamini. Lakini (hata raisi anakiri kuwa) kodi haikulipwa kwa makosa ya AG. Adhabu ya kuikosesha mapato serikali zaidi ya 30bn ni kujiuzulu tu? Eti sasa wameiomba IPTL ilipe kodi, WANAIOMBA. Ni aibu gani hii.

Jambo jingine ndugu yangu hata kama fedha zote zile ni halali kwa IPTL, je utakatishaji wa fedha ulifanywa ili kumficha nani? Uchukuaji fedha Mkombozi Bank na Stanbic ulifuta sheria za nchi kweli? Kama utakubali utakasishaji ulifanywa, je hakuna wa kuwajibika? Lipite tu kama nchi haina watu? Tunaenda wapi?

Ndugu yangu mtoa mada, serikali na Chama cha Mapinduzi hata kikitakasika katika sakata hili la ESCROW lakini bado harufu ya madudu mengi yanayoendelea kufanywa haitaisha. Kubaliana na mimi tunahitaji mabadiliko makubwa kama tuna dhamira ya kweli ya maendeleo yanayowanufaisha Watanzania wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…