Epuka muhuri wa shetani

Introver

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2019
Posts
565
Reaction score
655

JE! UNAJUA JAMBO GANI LITAMPATA MTU YULE, ALIYESIKIA UKWELI HALAFU HATAKI KUBADILIKA?

Biblia inaeleza wazi kabisa kulingana na maandiko hayo hapo juu, Mtumwa yule aliyetangaziwa uhuru wake baada ya kutumika miaka 6 akakataa (Yaani akaona ni vyema kuendelea katika utumwa wake.). Jambo linalotokea ni hili bwana wake huyo mtumwa atachukua sindano na kutoboa SIKIO lake, kuwa kama MUHURI wa kukataa kuwekwa huru, Hivyo basi huyo mtumwa atamtumikia bwana wake milele, Na kama tunavyofahamu sikio likishatobolewa haliwezi kurejea tena katika hali yake ya kwanza. Na ndio maana ilikuwa inatumika kama ISHARA YA MAPATANO(MUHURI).
Vivyo hivyo kwa wanadamu wa leo, Kristo alikuja kututangazia uhuru wetu kutoka katika UTUMWA WA DHAMBI kulingana na
Mathayo 11:28-29 (Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; “),
Kwasababu Bwana Yesu alisema Yohana 8:34-36″ ….Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
Bwana Yesu pia alisema maneno haya luka 4:18-19″ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, KUWAACHA HURU WALIOSETWA,Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. “
Kwahiyo injili ililetwa kwetu mahususi kwa kutuweka HURU mbali na dhambi. Hapo anaposema
“kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” akiwa na maana kuwa ndio mwaka wa maachilio, ule mwaka wa saba ( Kwa maana mahali pengine anasema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa.

MUHURI WA MUNGU:

Mungu anao MUHURI wake, na shetani pia anao muhuri wake kwa watoto wake. Wale waliokubali kuwekwa huru na BWANA wanatiwa MUHURI WA MUNGU nao ni ROHO MTAKATIFU kulingana na
waefeso 4:30″(Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa MUHURI hata siku ya ukombozi). , na pia biblia inasema katika
2 Wakoritho 3:17 .. walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. “.
Kwahiyo unaona unapoukubali UHURU Mungu anakupa zawadi ya kupokea Roho Mtakatifu kama Muhuri wa uhuru wako. Lakini kama hauna Roho wa Mungu wewe bado ni mtumwa wa dhambi na UNAJUA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI. Warumi 8:9″….Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. ”

MUHURI WA SHETANI:

Kwa wale waliokataa uhuru kwa makusudi angali wakijua kabisa wapo kwenye utumwa na wangepaswa wawe huru, lakini wakapenda kumtumikia bwana wao shetani katika dhambi zao kuliko kumtumikia Mungu nao pia wanatiwa MUHURI. Na mihuri hiyo YA SHETANI wanatiwa katika MASIKIO YA MIOYO YAO, maana yake ni hii HAWATAKUWA TENA NA NEEMA YA MUNGU JUU YA MAISHA YAO!,baada ya kuisikia injili na kuikataa Haiwezekani wao kumgeukia Mungu tena, Hata waelezweje injili hawawezi kusikia tena wageuke hao wameshakuwa mali halali ya shetani. Hii ni hatari sana tuwe makini tunaposikia wito wa Mungu.
Na huu muhuri wa shetani mpaka sasa hivi unaendelea kuwapiga watu,
leo hii umeshaisikia injili mara ngapi, umehubiriwa uache uzinzi mara ngapi ewe kijana ewe binti,? umehubiriwa utubu dhambi zako mara ngapi? lakini umekuwa wa kwanza kufanya mizaha? umehubiriwa uache ulevi mara ngapi? unavuta sigara, unaangalia pornoghaphy, unafanya mustarbation, binti unasagana, umekuwa shoga kijana, unaenda kwa waganga, unajifurahisha katika anasa na miziki ya kidunia,
Mwanamke unavaa suruali, vimini, unapaka rangi kucha, kijana unanyoa mitindo isiyofaa na kusuka nywele ,na tatoo kwenye mwili wako, wanawake usengenyaji na umbea, mtukanaji, unajichanganya na watu waovu kwa jinsi isivyopasa, unachati nao mambo maovu, huku ukijua kabisa watu wanaoyafanya hayo wataishia katika jehanum ya moto, JE! UNADHANI NEEMA YA MUNGU ITAENDELEA KUDUMU JUU YAKO MILELE?.
Mungu hadhihakiwi apandacho mtu ndicho atakachokivuna. Tutawezaje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii?.
Unashindwa kuona jinsi unavyozidi kutiwa ule MUHURI wa shetani? kwa kuukataa uhuru wako ambao BWANA aliokutangazia pale KALVARI?. Maana kama unasikia sauti ya Mungu kila siku ikisema moyoni mwako UTUBU lakini unaipuuzia nakwambia ukweli utafika wakati HAUTAKAA UISIKIE TENA NDANI YAKO!!,
Na unajua ni kitu gani kitaenda kukutokea? Ni kwamba utafika wakati utaona mambo yote kuwa ni sawa, kuwa ulevi ni sawa,utaona uasherati hauna ubaya wowote, Mungu aliyetuumba hawezi kutuhukumu, hautaamini tena kama kuna jehanamu, utaishia kuwaona watumishi wote wa Mungu ni waongo, utaishia kuukosoa kila siku ukristo na biblia ukisema hayo mambo ni ya kale.
Utaanza kujiona kuwa ni haki yako kuishi unavyotaka hata kujichubua, kubadili maumbile, kuvaa unavyotaka ni sawa, Utajiona kutukana ni sehemu tu ya maisha ya binadamu hakuna kosa lolote kwasababu Roho Wa Mungu hayupo tena ndani yako kwasababu UMESHATIWA MUHURI, utaanza kuona kujipenda mwenyewe ni sawa, Kutazama pornography na kufanya musturabation ni sehemu maisha ya kila mwanadamu ukijidanganya kuwa Mungu hawezi kumuhukumu mtu kwa kufanya hivyo, unajikuta unaanza kupenda kufuatilia mafundisho ya mashetani kuliko mafundisho ya Mungu, Biblia hutaki kusoma kusoma lakini habari za freemasons, na zi kichawi, na filamu pamoja na vitabu kama , harryporter, twightlight, vampires,n.k. ndivyo vinavyokuvutia kusoma na kuangalia, jiulize ni roho gani inakuendesha? n.k.
Ndugu ukishaanza kuona dalili ya mambo kama hayo yanakuja ndani yako, jua kabisa neema ya Mungu ndivyo inavyoondoka kwako kidogo kidogo na ndo unavyoupokea MUHURI wa shetani hivyo, maana jua tu wewe unayeisikia injili kila siku unaambiwa utubu hautaki, neema yako haiwezi kuwa sawa na mtu yule ambaye hajawahi kusikia injili kabisa. soma mstari ufuatao;
Kwahiyo ndugu maneno hayo hayakuogopeshi?? TUBU! yamkini hii sauti ya upole inayokuambia kila siku utubu bado inaendelea KULIA NDANI YAKO! ..itii na ugeuke maana upo katika HATARI, Maana hiyo sauti haitadumu milele ndani yako. Na ikishaondoka hakutakuwa na njia ya kurudi tena. YAANI MOYO WA KUTUBU hautakuwepo tena ndani yako utafanana na hao watu unaowaona huko ulimwenguni watendao matendo ya giza si kana kwamba hawasikii au hawakusikia injili hapana lakini mioyo yao imeshatiwa MUHURI, hawatakaa wasikie tena na kubadilika, ndugu usifanane nao. Mtii Mungu tubu dhambi zako muda umeenda sana kuliko unavyofikiria.Yesu yupo mlangoni kurudi.
Maana biblia inasema…
Naomba umalizie kwa kuyatafakari maneno yafuatayo ujue hatma ya WALIOUKATAA UHURU WAO KUTOKA KWA BWANA;
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…