Epuka maisha ya kuigiza

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
156
168
:KIJANA EPUKA MAISHA YA KUIGIZA

Maisha ya kuigiza kwa vijana wengi wa kitanzania kwasasa ni kawaida sana na wengi ndicho kinachowapotezea dira ya maisha..
Kuna mtu anawaza atakula nini sababu hakuna hela lakini akiona nguo mpya kavaa msanii mkubwa mfano diamond platnumz yupo tayari asile lakini avae nguo zile...Maisha haya ni ya kuigiza bila sababu..

Ukifikiria kipindi diamond platnumz hajafanikiwa kuwa msanii mkubwa alikua havai nguo za gharama alikua anakusanya hela kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake na alifanikiwa na sasa anaweza kuvaa nguo za gharama anavyotaka..

Kila mtu anayatamani maisha mazuri na matamu lakini lakini ni lazima upambane ili upate unavotamani.

Vijana wengi wanapoteza muda na pesa nyingi sana kwenye maisha ya kuigiza avae aonekane kama nani aongee kama nan wengine hufika mbali na kuacha vipaji au vipawa walivyojaliwa na Mungu na kufanya vingine ili waonekane kama mtu fulani ukweli ni kwamba utafeli kijana mwenzangu maisha hayaigizwi bali yanafanywa kweli.

Muda na akili vijana wanayotumia kupata hela na kununua suruali tishet na kofia kama ya Diamond au simu kama ya juma jux akili hizo na muda huo wangewekeza katika kutafuta pesa kwa ajili ya maisha ya baadae huenda wangeishi maisha makubwa kuliko hao.

Aliwahi kusema mtu mmoja maarufu kwasasa ni matehemu STEVE JOBS mmiliki wa kampuni ya Apple alisema hivi "Your time is limited, so dont waste it living someone else's life." ( Muda wako ni mdogo/hautoshi hivyo usiupoteze kwa kuishi maisha ya mtu mwingine)

Usiishi maisha ya kuigiza kijana mwenzangu muda unaouona mwingi ni mchache sana ishi maisha yako kwa sasa ili baadae watokee watakao kuigiza wewe

Sio vibaya kufata njia za mafanikio aliyopata mtu ila ni vibaya kuishi kwa kumuiga yeye

By Jay Speed
 
Back
Top Bottom