Epuka kufanya mambo haya ukitoka na mpenzi wako

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
229
Iwe ni mara yako ya kwanza,au umezoea kutoka na mtu wa jinsia tofauti lazima kuna vitu uzingatie ili usiharibu ladha na maudhui ya mtoko wako.Kwani ni ukweli ulio wazi kuwa mpaka umekubali kupata mtoko na mtu wa jinsia tofauti maana yake unafurahia uwepowake karibu yako.Na pengine ushaanza fikiria mipango ya baadaye ukiwa naye.Lakini kuna makosa ambayo tunayafanya wengi wetu siku ya kwanza unapotoka na mtu wa jinsia tofauti.Pitia vipengele vifuatavyo ugundue unafanya wapi makosa na uyaepuke.
1.USIMZUNGUMZIE MTU WAKO ALIYEPITA

Hili ndio kosa kubwa la kwanza ambalo wengi wanalifanya wanapokuwa katika mtoko na mtu mwengine wa jinsia tofauti.Tambua wazi si kwamba utamuonyesha kuwa una hisia na watu unaowahi kuwa nao,lakini ujue unamuudhi mtu uliyetoka naye.Kuleta suala la mtu mwengine aliyepita wakati uko na mwengine halina maana yoyote kama umekosa la kuongea heri unyamaze hadi uulizwe.
2.USIZUNGUMZIE NGONO



Kabla hujajua kama unayetoka naye anapendelea mazungumzo ya aina gani,
usikurupuke kuzungumzia habari hizo kana kwamba wewe ni mtaalamu sana ukidhani utamvutie uliyetoka naye.Kama uliyetoka naye ana malengo ya mbali utamfanya afikirie mara mbili kama utamfaa siku za mbele.
3.USIJIZUNGUMZIE WEWE KILA WAKATI

Kujizungumzia wewe kila wakati itamuonyesha uliyetoka naye kuwa una ubinafsi ndani yako.Kila mtu angependa kupata nafasi ya kujielezea mbele ya mwenzake lakini kama wewe unamkatisha na kujizungumzia wewe tu utamtisha.Ukionyesha unampa nafasi ya kumsikiliza anachoongea yeye utamfanya aone wewe ni msikivu.Na ukiwa msikivu kwa mwenzako utapata nafasi ya kumtambua uliyetoka naye anapendelea mazungumzo ya aina gani.
4.IJUE HISTORIA YAKE

Tafuta taarifa za mtu unayetaka kutoka naye kabla haujafanya hivyo,
kwasababu wengine wana tabia ya kurudia matukio mabaya waliyoyafanya siku za nyuma.Ukijichanganya kutoka na mtu bila kujua ana tabia gani anapofanya mtoko na mtu wa jinsia tofauti usije ukakumbana na balaa.
Wengi walipatwa na mabaya kwa kutojua historia ya wanaotoka nao na baadaye kujutia.
5.USITUMIE LUGHA CHAFU

Hata kama ni kawaida yako kuzungumza kwalugha chafu,unapotoka na mtu kwa mara ya kwanza jitahidi kuficha mizuka yako.Kutumia lugha chafu kwa kudhani utamuonyesha uliyetoka naye kuwa unajiamini na umuogopi ni kujiongopea.
6.KUVAA HOVYO

Tabia ya kumchukulia poa unayetoka naye na kuvaa hovyo ili ujionyeshe kuwa unaamua unalotaka,unaharibu taswira yako kwake.Kwani wengi huona kama umeshindwa kumuonyesha kumuheshimu siku ya kwanza au kabla hamjawa pamoja inawezekana ukamuonyesha dharau zaidi utakapokuwa naye.
7.USIBEBE ZAWADI ZA GHARAMA

Kumbuka huo ni mtoko tu na sio sherehe.Unapobeba zawadi za gharama kubwa kwa mwenzako si kwamba utamfurahisha lakini ndani yake utamfanya akuone kuwa upendo wako pia unajengwa zaidi na vitu vya gharama.
8.USISHAMBULIE WENGINE

Ukiwa umetoka na mtu usianze kumzungumzia vibaya mtu au watu wengine,
kwani utamuonyesha wazi kuwa ipo siku na yeye itakuwa zamu yake.
9.USINYWE MPAKA UKALEWA


Hata kama ulikuwa na kiu kubwa ya kunywa pombe angalia usivuke kiwango mpaka ukalewa na usijielewe.Tabia hii itamuonyesha ishara mbaya juu yako.

UFANYE MTOKO WAKO KUWA WA KAWAIDA,MSAFI, KUFURAHISHA,NA WAKUKUMBUKWA.ANZA SASA KUWA MAKINI UNAPOKUWA UMETOKA NA MTU WA JINSIA TOFAUTI ILI USIHARIBU SIKU YAKO YA KWANZA YA MTOKO NA KUMPOTEZA MTU AMBAYE UNGETAMANI AWE KARIBU YAKO.
 
hiyo ni kwa wazungu tu...kwetu sisi wa uswazi kwanini ujinyime raha kwa kuigiza maisha ambayo sio yako
 
10. Usiongelee siasa siku ya mtoko wa kwanza.
11. Hakikisha hauzungumzii maswala ya dini.
12.usimuulize umri wake wala kazi yake kwani hiyo si siku ya job interview utamboa.
13.namba nne(4) hapo juu ni ngumu wakati mwingine maana tunakutana wakati hatufahamiani na twaweza kuwa tunaishi maeneo ya mbali sana.
14. Usiende na zawadi yoyote kabisa kwani utamfanya mwenzako ajifikirie inakuwaje unatoa zawadi kwa watu usiowafahamu.

15. Hakikish unafanya mambo ndani ya uwezo wako, kama huna pesa fanya vitu vya kawaida, epuka kujifanya kidume wakati uwezo hauruhusu kwani mda si mrefu mwenzako atakujua hali halisi ya uchumi wako na ataku damp kama ulifake
 
Dear once someone talks about number 2 on first date I d
Namba 9 ishanitokea. Nililewa nikapiga sound adi zikapitiliza..
Nikachezea cha mbavu kimoja laaana na kuchambwa juu kesho yake
aahhhhhaaaaaaa pole sana dear .. Thanks....
 
# Usiwe busy na simu yako muda mwingi...siku hizi watu wanatoka lakini kila mtu busy na simu...wajiuliza si wangechati tu remotely

#Usiwe macho juu, kila anaepita wataka kumkodolea ebo?!.

#Usilazimishe kwenda kiwanja chq kifahari au hoteli ya bei juu ilihali kawaida yako no middle class. Unafanya mdhamini kuvunja benki na kuogopa mtoko mwingine
..yaani mtoko wa kwanza Karambezi, wa pili hyatt..
ila ukiwa na rafiki zako hua mnaenda lukas pub....ebo wamkomoa nani?!
 
10. Usiongelee siasa siku ya mtoko wa kwanza.
11. Hakikisha hauzungumzii maswala ya dini.
12.usimuulize umri wake wala kazi yake kwani hiyo si siku ya job interview utamboa.
13.namba nne(4) hapo juu ni ngumu wakati mwingine maana tunakutana wakati hatufahamiani na twaweza kuwa tunaishi maeneo ya mbali sana.
14. Usiende na zawadi yoyote kabisa kwani utamfanya mwenzako ajifikirie inakuwaje unatoa zawadi kwa watu usiowafahamu.

15. Hakikish unafanya mambo ndani ya uwezo wako, kama huna pesa fanya vitu vya kawaida, epuka kujifanya kidume wakati uwezo hauruhusu kwani mda si mrefu mwenzako atakujua hali halisi ya uchumi wako na ataku damp kama ulifake
Nmekupenda ghafla :)
 
Back
Top Bottom