jf user
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 777
- 625
1/Acha dhambi.
Dhambi ni msingi wa matatizo yote hapa duniani. Inafahamika ufanyacho ndicho ufanyiwacho kwa hiyo usujisifu kufanya uovu useme MUNGU amekusahau we tambua atakuja kulipizia kwa mkeo, mtoto, baba au mama, ndugu na marafiki wa karibu.
Usaliti, uuaji, udanganyifu, utesaji, dhuluma, laana, kudhulumu haki ya mtu n.k
MUNGU yupo macho kamwe hasahau.
2/Angalia sana vyakula unavyokula pamoja na vinywaji.
Sio siri magonjwa kama presha, kisukari, unene wa kupindukia, magonjwa ya figo na ini husababishwa na ulaji wa vyakula vyamafuta mengi hasa ya wanyama ambayo hulunikana kwenye mishipa ya damu, kuta za moyo, mafuta kwenye mishipa ya kichwani kupasuka hivyo damu kujaa kwenye ubongo hii husababisha kifo, mafuta ya tumboni na sehemu nyingie za mwili haya hukumaliza mapema. Pombe huleta sumu na kemikali mwili mwilini pamoja sigara ambazo hufubaza mapafu yako. Vyakula na vinywaji vichafu nalo ni janga kwa hiyo chakula kizuri ni kile ulichokipika mwenyewe... vyombo safi, nyama safi "Epuka nyama ya kununua kwani waeza kula fisi au kibudu"
Nakushairi usali sana kwa kila kinachoingia tumboni ili MUNGU akitakase chakula chako.
3/Stress.
Majuto na mawazo haya humtafuna mtu mdogo mdogo mpaka anakufa siku sio zao. Moyo huwa unashindwa kuhimili maumivu na mwishowe mtu hufa kwa stress. Ni bora kuachana moja kwa moja na vitu vinavyokufanya uwaze, uishi kwa mashaka na uwe na stress maisha yako yote. Mapenzi huwamaliza watu hapa kwa hiyo lifanyieni kazi, Kwenye mapenzi kuna faida zake ila madhara yake ni makubwa kushinda faida. Mapenzi yanaua, mapenzi yamejaa magonjwa, mitafaruku na mikosi ya kila aina ikiwa mmoja wapo atadhulumiwa au wote watadanganyani ni rahisi kufikishana kifoni au stress za kudumu.
4/Kuishi maeneo hatarishi.
Maeneo hatari pia hummaliza mtu haraka mfano mtaa wenye vibaka, maeneo ya viwandani yenye kutoa kemikali kiholela, meneo ya mabondeno ambako hukumbwa na mafuriko, tectonic place zone kama maeneo ya japan, Malaysia, Indonesia na hapa kweny ni eneo la jangwani, mkoa wa mara kuliko pita bonde la ufa kwa kiufupi eneo la mwanza, kagera na mara ni la mashaka. Pia maeneo ya vita kama Somalia, sudani ya kusini sio ya kuishi chakushangaza wapo wau wako huko wenye roho ngumu wanadai wanasaka pesa kwa uhai wao hauna thamani. Hawa ni wakuachana nao kwa sababu wamejitoa mhanga ila wale wasiojua ni vyema kuwatonya mapema waswahili wanasema mwenye macho haambiwi tazama.
5/Maeneo yenye wanyama wakali.
Kuna sehemu zenye wanyama wakali sana kama simba, chui, fisi tembo, nyoka n.k haya ni kukaa nayo mbali sana. Wale wanaokaa maeneo ya vijiji vilivyo karibu na mapori au misitu ni vyema wajihami mapema.
6/Maeneo hatarishi ya kazi.
Maeneo hayo ni kama hospitali hasa swala la kutibu wagonjwa wanaovuja damu an kudunga sindano ni tatizo sana, pia magonjwa huko huambukiwa kwa hewa na kugusana miili, kazi za viwandani hasa kemikali, moshi, mwanga wa computer hummaliza mtu mdogo mdogo bila kujijua, Vumbi barabarani na wale mafundi seremala hilo vumbi litawamaliza tuu msipotumia njia za kulizua kama kufunika mdomoni kwa kitambaa ili uvute hewa safi iliyochujwa. Kutokua mwangalifu makazini huwasababishia watu vifo! wapo walioangukiwa na vifusi, kupigwa shoti, zana zao za kazi kuwajeruhi wenyewe kwahiyo nagusia uangalifu makazini ndugu zangu.
7/Ajali.
Zipo ajali ambazo ni natural ambazo zinatokana na dhambi za wahusika na zile ajali nyingine ambazo ni makosa ya kibinadamu. Kuvunja sharia ni sababu mojawapo ya ajali za barabarani, majini angani n.k
Ni lazima vigezo vitimie usizidishe Zaidi ya kipimio kilichowekwa na pia wewe kama mjanja unaweza soma usalama wa chombo kwa mfano dereva akiwa na kasi sana au akiwa mlevi mumuonye, chombo cha barabarani, majini au angani kikizidisha mzigo mkatae au usipande kabisa ili kuyaokoa maisha yako pia maisha ya wengine. Ni upuuzi kurudia makosa makosa yanayotokea mara kwa mara huo ni upumbavu.
8/Kutokumtafuta MUNGU.
Wasiojielewa watapinga sana hili ila naomba nifunge nalo. Mwenye kuona na aone... mwenye kusikia na asikie. Usisahau kumwambia na mwenzako unaeona yupo kwenye mazingira hatari bila ya kujijua.
Kwa pamoja tupendane na tusaidiane.
NB: Yapo maeneo mengi mtu unaweza kukaa na kuyatathmini na kutueleza hayo ili tuyaepuke mapema kuokoa maisha ya watu..