Enzi za Shy bush (Shinyanga technical school)

Jabman

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,005
1,337
Nakumbuka enzi hizo ugali tuliita ngunga(gima) wali uliitwa bee. Ugali ulikuwa ukilala kesho take unakuwa mweusi kama udongo was mbuga. Maharage yenye funza weupe na weusi yalinogesha mlo.

Tulikula na kushiba japo ukipewa Leo unaweza kimbia. Nyama ilikuwa nadra sana.
Namkumbuka Mwl Okonkwo, TMO, Mwananchi na Peter Simbee. Pia Ncheye ,Mlundwa,Ndege,Mihayo,Madaha,Shiyayi na Robert Mwigulu.

Nakumbuka jumapili Maganzo gulioni. Nakumbuka maeneo kadhaa ya Mwadui ,Utemini na kwingineko.

Hakika nimepamiss sana Shy-bush.
Nikumbushe mengine tafadhali. Ahsanteni na karibuni.
 
Umenikumbusha mbali sana, kuna siku tulikuwa tunatoka Maganzo kuelekea shybush, wakati huo ilikuwa mwishoni mwa masika.

Tuliona dibwi dogo kuangalia vizuri kuna samaki wa kutosha aina ya kambale, aisee! Siku hiyo ilikuwa sherehe kubwa kwetu, unajua tena maisha ya boarding.
 
Pale bondeni maganzo unaiona kwa juu wakulima wa mahindi wa pale walipata shida sana na vijana wa bush penye vile vinjia ilikuwa mtu kama unapita kumbe unavuna mahindi mpaka mwisho wa shamba umejaza kimfuko
 
Mwaka 2011 waligoma pia,shule akabidi ifungwe kwa muda lakini bahati mbaya wakati wasafari ya kuelekea makwao kunaajali ilitokea ambapo wanafunzi kadhaa walifariki akiwemo mwalimu mkuu wa SONGWA secondary.
 
Kweli kabisa mkuu ajali ilitokea Kolandoto njia panda
 
Mwaka 2011 waligoma pia,shule akabidi ifungwe kwa muda lakini bahati mbaya wakati wasafari ya kuelekea makwao kunaajali ilitokea ambapo wanafunzi kadhaa walifariki akiwemo mwalimu mkuu wa SONGWA secondary.
Umenikumbusha mbali sana.Nilikuwa miongoni mwa wahanga, tulifukuzwa shule na kulazimika kukaa miezi3 nyumbani
 
Back
Top Bottom