LTK haujafanya stadi ya kutosha kuweza kufahamu fika kwa nini Wahandisi wetu unadhani ni wavivu wa kutafuta elimu na maarifa mapya. Ukiwa na Degree na unafanya kazi ya "See-and-Do" ambayo hata form six anaiweza, unahitaji Masters au PhD ya nini? Elimu hiyo unayoiita ndogo bado hawapewi nafasi ya kuiweka kwenye uzalishaji. Serikali inawasomesha lakini zikija kazi wanawapa wageni kwa kisingizio kwamba hawana ujuzi! Kama hawana ujuzi nani aliwaandalia mitaala yenye elimu ya utapia mlo? Na kwa nini basi kusiwepo na mpango maalumu wa hao wenye ujuzi kufanya kazi na wazawa ili Taifa lisibaki tegemezi milele?
Engineer wa Tanzania ni hasara sana, yani baada ya kumaliza masomo yao na kufanikiwa kupata kazi, wao hubweteka huko makazini na hakuna maendeleo yoyote ki ujuzi wanayo jiendeleza, kinachobaki anafanya kazi kwa mazoe kwasababu unakuta kakalili machine aina flani au program, siku waki badilisha mfumo alio kua kazoe ana buma ile Mbeya.
Dunia ya sasa ki teknolojia ina badilika kila siku ila Engineer wetu wapo pale pale hawa move na teknolojia, kwasababu hawana tabia ya kujifunza vitu vipya, wao kazi yao ni Service na troubleshooting.
Na ndio maana hata company nyingi zina ajiri wataalamu kutoka nje na si kwamba hapa kwetu hawapo, ila tatizo letu ni watu wa kubweteka hatwendi na dunia ya Teknolojia na hatutaki kujifunza vitu vipya.
Wosia wangu kwenu mnaojiita ma Engineer unakuta hata ERB haiwatambui, mmbadilike ili twende na kasi ya madiliko kwa maendeleo ya nchi yetu.
Hawa watoto wa form six wanaenda lini chuo? Wamechafua kweli nyumba muda huu wa waliokua nyumbani! Na hivi vi 50MB vya mini kabang na wenzake; na simu za kupewa na kaka....imekua kero kwa kweli!! Heri waende chuo wakawe bize tupumuwe kidogo...
Samahani wewe ni mtaalamu wa nini au fani yako ni nini au elimu yako ya juu kabisa ni ipi?Ukishajibu hayo itatuwia rahisi sana kukujibu maana itatusaidia kujua tunaongea na mtu wa aina gani!Wakati mwingine mtoto wa darasa la saba unamjibu kilasaba la saba,wa form 4 kiform 4,wa six kisix six,chuo kichuo chuo,mwanasiasa kisiasasiasa,mwalimu kuualimu alimu,enginer kihandisi handisi.Mwenzetu unaangukia wapi tukujibu!
Engineers always build the world,wapo mainjinia majembe sana..kiteknoham awapo juu..serikali legelege haiwatambui tu.