Engine Mitsubishi GDI

michepuko

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2014
Posts
1,192
Reaction score
346
Wakuu naomba msaada kwa hili,
Nimekuwa nikitumia Mitsubish Pajero GDI (siyo turbo cc 660) kwa muda wa miaka 2 sasa,
Tatizo limejitokeza la kuzimazima kila mara,nimesha badili plugs na vitu vingi tu ,lkn inaendelea kunisumbua,
Sasa nimeona ni bora nibadili complete Engine na gear box yake,Kama kuna yeyeto ambaye amewahi kubadili engine ya gari hizi tafadhali anijulishe ni Engine gani ya Toyota inaweza kufit kwenye GDI.
Na kama angeweza kunielekeza inakopatikana egine hiyo ingekuwa vizuri zaidi
Nawasilisha.
 
Sidhani kama kuna GDI yenye CC 650! Nadhani hiyo yako itakuwa Pajero Mini au Junior japo Junior zina CC 1100. Nenda pale Kariakoo karibu na Karume ukamuone 'Mpemba' mmoja anaitwa Chidi. Anazo injini na gearbox za aina mbali mbali za Mitsubish No yake ni 0718 064 600.
 

Mdau tatizo hlo cyo kubwa kama unavyolifikiria na wala cyo la kukuingiza gharama zote hzo tatizo la gdi linachagua mafuta, gdi maana yake ni gassoline direct injection kwa hyo hapa tz tuna uhaba wa aina hyo ya mafuta, ila pia ukiweka mafuta katika vituo visivyo eleweka ndo balaa linaanziaga hapo kwa nakushauri uwe unaweka mafuta aina ya unleaded hasa puma, back to ze topic mtafute kuna jamaa anaitwa kamugisha yuko keko karibu na msd ndo mchawi wa hzo gari atalishughukia utafurahi na declear interest nishawahi kuwa nalo hlo gari
 

Shukrani mkuu,
Naomba nitumie namba ya Huyo fundi mkuu.
 
Kaka hizo specification za hiyo injini sijazielewa. Hebu sema ni pajero gani hiyo?
 
Jamani msichanganye mambo GDI si mafuta ni teknolojia ya mitsubishi kwa injini zake. "Gasoline" ni neno la kiingereza tu maana yake ni "petrol". Unajuwa kukua kwa teknolojia na maendeleo ya masoko kumesababisha kuwe na majina mengi ya petrol. Mfano petrol ilishawahi kuitwa gasoline, super, regular na leo hii tunaiita unleaded. GDI ni trademark ya Mitsubishi, hakuna gari yoyote itakayoitwa gdi isipokuwa kama watanunua trademark hiyo. GDI ni kama D4 au D4D kwa Toyota. Au pengine TDI na HSE kwa landrover au Mvitec kwa honda. Gari ya mshikaji inahitaji service ya kina hasa kwenye ignition.
 

Unajua kuna aina na grade ngapi za hayo mafuta unayoita petrol au ndo walewale ni pm nikupe somo uone tofauti hzo za mafuta faida na hasara zake ktk mfumo mzima wa uunguzaji wa injini mdau
 

ndiyo gari ninalolitumia na huu ni mwaka wa tatu sasa!niliwahi kukumbana na tatizo kama hilo siku za nyuma na chanzo ilionekana ni mafuta machafu,nozel zilikuwa hazitemi mafuta itakikanavyo!nilibadili plug haikusaidia hadi pale nilipo safisha nozel nikaagana na mkorofi tatizo la kuzima hadi leo!kama unafundi mzuri mwambie ajaribu kucheck nozel.
 
Wewe ulisafishia wapi nozel?unaweza nipa contact za fundi kama uko dar?
 
Unajua kuna aina na grade ngapi za hayo mafuta unayoita petrol au ndo walewale ni pm nikupe somo uone tofauti hzo za mafuta faida na hasara zake ktk mfumo mzima wa uunguzaji wa injini mdau
Hakuna haja ya pm, weka uelewa wako wazi ili kila mtu apate faida. Gasoline is American english saa zingine huita "gas" na "petrol" ni British english, hii ni aina ya fuel ambayo hutumika kwenye "internal combustion engine"
 
Min pajero,GDi
Naomba unijibu yafuatayo.
1. Odometer inasoma ngapi?
2. Kuna dalili za kutoa moshi kwenye bomba la moshi?
3. Umewahi kubadili timing belt?
4. Kama kuna dalili za moshi kwenye bomba la moshi je ni moshi wa rangi gani?

Kubadili injini si solution ya tatizo lako. Kitaalamu tunaita "canibalization"
Tatizo la gari yako ni dogo sana ila likipata fundi mhuni utajuta.
 
Gdi ya 650cc ipo. Saa zingine pajero yake inaitwa Nissan KX.
 
kzba, Zamaulid na multmandalin karibuni kwenye jamii ya wenye hekima.
Mmetoa msaada mzuri kwa michepuko nadhani amewaelewa vya kutosha.
Hata mi nimewasoma vizuri sana. Hekima zenu zimeonekana. Niliwahi kutumia Pajero Jr 1100cc ya 1999 ni gari nzuri sana kuanzia fuel efficiency mpaka performance yake ukizingatia kilikuwa manual na 4WD.
Tatizo kubwa sana la gari hizi ni wese tu basi. Ukijichanganya kuweka mafuta mabovu kama yale wanayouza pale Big Bon Sinza Mori lazima ulie na gari kati kati ya barabara. Otherwise uwe na urafiki na Puma na TOTAL.
Mitsubishi is a good car that does not compromise when it comes to fuel standard.
 
Last edited by a moderator:

Odometer = 102,967km
Timing Belt = Sijawahi kubadili.
Moshi= inatoa mweupe mostly nikiiwasha asubuhi.
Kubadili Engine = Nadhani kuweka ya toyota na gear box yake hata system ya mafuta itabadilika,haitakuwa direct injection tena.Napia mfumo wa umeme utakuwa wa toyota pia.
 
JR na mini nazo ni GDI pia, GDI stands for gasoline direct injection, engine yoyote ambayo ni direct injection ni GDI


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…