Eneo jipya lenye Tanzanite hapa nchini liko wapi?

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,244
Wakuu poleni na majukumu,
Nianze kwa kuipongeza serikali kwa kuweza kuipokea ndege kubwa kabisa duniani na kupelekea Kuipandisha hadhi nchi yetu.

Baada ya Salamu hizo nije kwenye swali langu.

Wakati Rais JP Magufuli anazindua ukuta wa Mirerani Simanjiro alitujuza kuwa kuna mahali pengine Pamegundulika kuwa na Kiasi kikubwa cha Tanzinite na hakukitaja ila alisema tutataharuki siku anazungushia Ukuta.

Je ni wapi huko? Wataalamu mliogundua tujuzeni tuanze kupamendea na kununua viamba huko maana nyota njema ni ya asubuhi.

Ahsanteni Karibuni Wataalamu wa Miamba mtujuze.
 
Inasemekana ni kwenye ardhi ulipo uwanja wa ndege wa KIA. Eti Nyerere aliujenga ili kuzuia watu wasiyachimbe.
 
Wilaya ya nyang'wale..nilipata kufaham miaka minne iliyopita..kwa taarifa tajiri anaependa vitalu alinusa mapema tayari ana eneo la kutosha.
 
Wakuu poleni na majukumu,
Nianze kwa kuipongeza serikali kwa kuweza kuipokea ndege kubwa kabisa duniani na kupelekea Kuipandisha hadhi nchi yetu.

Baada ya Salamu hizo nije kwenye swali langu.

Wakati Rais JP Magufuli anazindua ukuta wa Mirerani Simanjiro alitujuza kuwa kuna mahali pengine Pamegundulika kuwa na Kiasi kikubwa cha Tanzinite na hakukitaja ila alisema tutataharuki siku anazungushia Ukuta.

Je ni wapi huko? Wataalamu mliogundua tujuzeni tuanze kupamendea na kununua viamba huko maana nyota njema ni ya asubuhi.

Ahsanteni Karibuni Wataalamu wa Miamba mtujuze.
Hapo ulipo uwanja wa KIA unaambiwa kuna mali baraa. Kuna stori kuwa majirani walizidi kuchimba visima kuusogelea wakatangaza kupanua uwanja, hivyo watu wasogee mbali.
 
Huwezi kujua, labda Magufuli na mchepuko wake mama Geougen ndo wakwambie, au Kagame.
 
Back
Top Bottom