Emmanuel Okwi aichinjia baharini Simba SC, aamua kujiunga rasmi na SC Villa ya nchini kwao Uganda

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,240
Aliyekuwa(mpaka sasa) mchezaji tegemezi wa Simba SC ameamua kuwatolea nje klabu yake waajiri wake wa zamani yaani Simba SC.

Mchezaji huyo ambaye alivunjiwa mkataba wake kwa makubaliano na klabu aliyokuwa akichezea huko Denmark....ameamua kuikacha klabu yake ya Simba SC ya Tanzania ambayo ilikuwa ikionyesha nia kubwbu mbaa ya kutaka kumsajili ili aongeze makali klabuni hapo...

Baada ya Mazungumzo ya kumrudisha Okwi Msimbazi kushindika kutokana na sababu mbali mbali, Mchezaji huyo ameamua kuwa ni bora ajiunge na mabingwa wa kihistoria wa mchini kwao SC Villa ambayo ina nafasi kubwa ya kushiriki michuano mbalimbali ya kimataifa..

Wachambuzi wengi wa soka hapa nchini wamelichukulia suala hilo kama ni Matokeo ya muenendo wa klabu ya simba ambayo haikumvutia mchezaji huyo kujiunga na Mabingwa hawa wa LigiKuu wa mwaka 2012/13.

Ikumbukwe kuwa baada ya kusikika kwa tetesi kuwa Okwi haitajiki na klabu yake huko Dernmark....Kulikuwa na Mshawasha wa kiwango cha juu kabisa cha furaha miongoni mwa mashabiki wa Simba SC wakitegemea Mchezaji huyo asingeweza kucheza klabu yeyote ile hapa barani Afrika na hatimaye angesaini na kuitumikia Klabu yake ya SImba SC.

images_emmanuel_okwi_zimbabwe.jpg

SOURCE:- Kawowo Sports/Uganda
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Hiyo ni shortcut ya kutua Simba, kama alivyofanya Ngassa baada ya kutoka South alienda uarabuni kidogo kisha akaenda Mbeya City baada ya chama lake kumkataa.
 
Uwe unauliza kwanza ueleweshwe... Huyo okwi walishatoa ufafanuzi hata ukimsajili sasa hawezi cheza hadi usajili ujao kwa sheria za tff. So ulitaka aje simba akae tu hadi majira ya kiangazi?? Tumia kichwa chako kuwaza usitangulize uyanga na usimba
 
Bila shaka we ni shabiki wa mikia fc
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Hiyo ni shortcut ya kutua Simba, kama alivyofanya Ngassa baada ya kutoka South alienda uarabuni kidogo kisha akaenda Mbeya City baada ya chama lake kumkataa.

sio mbaya kujipa moyo!

Si dhani kama yuko tayari kukosa kucheza mechi za kimataifa CAFCL NA CAFCC .....il hali hali halisi ya Simba anaijua ilivyo!
 
Uwe unauliza kwanza ueleweshwe... Huyo okwi walishatoa ufafanuzi hata ukimsajili sasa hawezi cheza hadi usajili ujao kwa sheria za tff. So ulitaka aje simba akae tu hadi majira ya kiangazi?? Tumia kichwa chako kuwaza usitangulize uyanga na usimba

Unajua amesaini miaka mingapi pale?

Mchezaji mwenye kucheza nusu msimu SC Villa anasaini vipi Miaka 2 kama lengo lake ajiunge na Simba mwezi wa 5/2017.
 
sio mbaya kujipa moyo!

Si dhani kama yuko tayari kukosa kucheza mechi za kimataifa CAFCL NA CAFCC .....il hali hali halisi ya Simba anaijua ilivyo!
We jamaa siku ukisikia simba imekufa utasikitika kuliko hata viongozi wa simba wanaoishi na kulea familia zao kwa kutegemea simba.... Mbona yanga kuna madudu mengi sana kwanini huandiki?
 
Sioni sababu ya kuchukizwa na akiandikacho mwingine!

Hebu tusaidie kuandika hayoo madudu ya Yanga SC kwa sababu mimi siyaoni.....
 
Dah ndio basi tena Mikia haichukui ubingwa tena maana walikuwa wanamtegemea Okwi aje kuwasaidia kuchukua Ubingwa.
 
Mimi nilipenda sasa wa matopeni wamsajili ili asaidie kuivuruga timu yao. Mchezaji ana muda mrefu bila kucheza mechi za ushindani na miaka inakwenda.

Okwi wa sasa hawezi kuwa yule wa siku za nyuma. Treatment yake kama mfalme pale matopeni ingewavuruga baadhi ya wachezaji wenye mchango mkubwa.
 
inaelekea ukilala ukiamka unamwa okwi naona bado una kumbukumbu alivyokuwa anaitesa yanga
nkuu
kumbukumbu niliyo nayo mimi ni kwamba kwa kipindi chote ambacho Okwi amekuwa akicheza pale Matopeni , Yanga imekuwa bingwa mara nyingi kuliko wa Matopeni...

Alichokuwa anawasaidia ni kuwafunga Yanga SC na nyinyi mkawa mnaridhika na hilo na kusahau kuwa kuna Ubingwa ...

Unamfunga Yanga SC halafu Bingwa anakuwa yeye! sasa ndio alikuwa na msaada gani pale Matopeni...
 
Mkuu huyu kaifunga Yanga mara mbili tu,walipofungwa 5 na alipomfunga barthez goli la mbali.
 
nkuu
kumbukumbu niliyo nayo mimi ni kwamba kwa kipindi chote ambacho Okwi amekuwa akicheza pale Matopeni , Yanga imekuwa bingwa mara nyingi kuliko wa Matopeni...

Alichokuwa anawasaidia ni kuwafunga Yanga SC na nyinyi mkawa mnaridhika na hilo na kusahau kuwa kuna Ubingwa ...

Unamfunga Yanga SC halafu Bingwa anakuwa yeye! sasa ndio alikuwa na msaada gani pale Matopeni...

Matopeni wakimfunga Yanga, basi roho zao kwatu na hawahitaji kingine zaidi ya hapo.
Ubingwa wa VPL kwao ni bonus tu. Kikubwa wamfunge Yanga basi.
 
Mlipe madeni ya watu mnaweza kushushwa daraja... Ingekuwa simba ungesha andika
Mkuu

sasa TFF ikiishusha Yanga daraja watapata wapi mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao ....?

Mungu akupe maisha ya miaka laki 8...lakini hutopata nafasi ya kuona Yanga SC ikishushwa daraja......kwa sababu hakitawahi kuja kutokea mpaka pale Yesu atakapo rudi mara ya pili kwa ajili ya unyakuo.
 
nkuu
kumbukumbu niliyo nayo mimi ni kwamba kwa kipindi chote ambacho Okwi amekuwa akicheza pale Matopeni , Yanga imekuwa bingwa mara nyingi kuliko wa Matopeni...

Alichokuwa anawasaidia ni kuwafunga Yanga SC na nyinyi mkawa mnaridhika na hilo na kusahau kuwa kuna Ubingwa ...

Unamfunga Yanga SC halafu Bingwa anakuwa yeye! sasa ndio alikuwa na msaada gani pale Matopeni...
Hata mlipo pigwa 5G yanga alikuwa Bingwa msimu ule.
 
Back
Top Bottom