Emmanuel Macron new French president after win with over 60 percent of votes

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
15,502
22,354
68939590d4d2ada6e557e675d62c0ff656261b7990cfd13cb20cfc343d6e5036_3947614.jpg


Mgombea wa Urais, Emmanuel Macron ameibuka mshindi baada ya kupata 65.2% ya kura dhidi ya Marine Le Pen aliyepata 34.8%.

Kufuatia ushindi huu Bwana Macron anaweka historia ya kuwa Rais kijana zaidi kuwahi kushika wadhfa huo katika nchi ya Ufaransa ambapo amekuwa Rais Mteule akiwa na umri wa miaka 39 tu.

Bi. Marine Le Pen amekubali kushindwa kwake katika kinyang'anyiro hicho na kumpigia simu mpinzani wake aliyeibuka kinara katika uchaguzi.

Rais anayemaliza muda wake Bwana Francois Hollande amempigia simu Rais Mteule, Emmanuel Macron na kumpongeza kwa kupata ushindi huo dhidi ya mwanamama Marine Le Pen.

Pia Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May naye ametoa pongezi zake kwa njia ya simu kwa Rais huyo Mteule.

======
Emmanuel Macron has beaten Marine Le Pen in Sunday's French election and taken more than 60 per cent of the vote, according to several early exit polls.

As the poll stations were closing around 7pm Mr Macron was believed to have won 65.5% and Le Pen around 34.4%

Polling conducted by Ipsos, Ifop and BVA all gave Mr Macron, the pro-business candidate, a strong lead over Front National leader Marine Le Pen.

It comes after a massive hacking attack on Mr Macron's campaign database over the weekend which saw hundreds of thousands of private emails and official documents dumped online

Polls close at 8pm with exit polls announced almost immediately offering what is widely thought to be an accurate view of the result.

Macron who has been predicted to win in various polls he will becomes the youngest French president at 39 years old, and he will celebrate with a reception at the Louvre in Paris.

Following the result outgoing president Francois Hollande will welcome his successor to the Elysee Palace within two weeks.

After a private meeting in which he hands over the nuclear launch codes, Mr Hollande will depart.
 
Tanzania lini tutafikia Demokrasia ya Ufaransa yakuwa na Rais asiyekuwa ametoka chama kikubwa cha siasa.

Mkuu, usidanganyike na demokrasia ya Ufaransa.

Ni kitengo ndicho kilimpalilia Macron aje kuwa raisi.

Mfumo ni uleule.

Kumbuka Emmenuel Macron alikuwa waziri katika serikali ya sasa ya raisi Hollande na akajiuzulu.

Walichofanya ni kumtengenezea mazingira mazuri ya ushindi.

Katika umri wake wa miaka 39 amekonga nyoyo za vijana wengi wapiga kura hiyo inaitwa "process of winning hearts and minds".
 
Wanawake wanabahati mbaya sana kwenye uchaguzi wa level za Urais bado wazungu wamekuwa wagumu sana kuchagua wakina mama kwenye level ya Urais lakini wamekuwa wakitulazimisha Waafrica kuwapa wanawake vyeo yani 50/50 lakini kwao ni kinyume chake wanawake bado mpaka leo wanalipwa mshahara mdogo kwa kazi sawa na wanaume

Mpaka sasa record zinaonyesha Mwanamke ameonyesha uwezo mdogo sana kwenye maswala ya uongozi Africa sema Gender Balance zinawabeba
 
Hahaaa wale wazee waliokuwa wanataka huyu bibi apite ili ajenda yao ya kuvuruga EU wamelala
Sasa Ufaransa itatawaliwa na Mwanamke kutokea Berlin(Rejea kauli ya Le Pen wakati wa mdahalo) kupitia kwa kijana Macron. Ufaransa hawakuwa na namna ilikuwa lazima watawaliwe na Mama awamu hii.
 
Ni adui yake?
Putin alikua anamsupport yule bibi ambae alikua anaunga mkono kuivunja EU, Ila huyu Emmanuel alikua hamsapot kwa sababu alikua anaunga mkono EU.Km unavyojua Putin angependa EU ivunjike sema ndoto zake nd hazitotimia. Kuna tetesi kwamba walijaribu kuhack emails zake km walivyfanya kwa Hillary jambo ambalo lingempunguzia kura
 
Tanzania lini tutafikia Demokrasia ya Ufaransa yakuwa na Rais asiyekuwa ametoka chama kikubwa cha siasa.
Uchaguzi unafanyika katika State of emergency huku Rais anayeondoka akiimiza kila waziri kuhakikisha Macron anashinda. Wakati huo huo vyombo vya habari vikitishiwa kushitakiwa ikiwa vitatoa habari za 'madudu' ya Macron. Unaijua demokrasia kweli ndugu!?
 
Uchaguzi unafanyika katika State of emergency huku Rais anayeondoka akiimiza kila waziri kuhakikisha Macron anashinda. Wakati huo huo vyombo vya habari vikitishiwa kushitakiwa ikiwa vitatoa habari za 'madudu' ya Macron. Unaijua demokrasia kweli ndugu!?
Mkuu tunaomba chanzo kuhusu kutishiwa kwa media
 
Uchaguzi unafanyika katika State of emergency huku Rais anayeondoka akiimiza kila waziri kuhakikisha Macron anashinda. Wakati huo huo vyombo vya habari vikitishiwa kushitakiwa ikiwa vitatoa habari za 'madudu' ya Macron. Unaijua demokrasia kweli ndugu!?

Ndiyo maana kila nchi ina demokrasia yake hivyo hapa watu wanaweza kujifunza khasa.

Wewe fikiria hakuna chombo hata kimoja cha habari kilichoruhusiwa kutangaza matokeo ya awali isipokuwa gazeti la Le Soir la Belgium ndilo liliweza kufanya hivyo na kwa kuwa lipo nje na ni lile la French/ Belgium speaking community.

Wenyewe wafaransa wakaambiwa wasithibutu kutangaza matokeo.

Sasa sisi mwaka 2015 watu walipoambiwa wakae mbali zaidi ya mita 200 walilalamika kutoka kwenye vituo vya kupiga kura.
 
Mkuu tunaomba chanzo kuhusu kutishiwa kwa media
Mimi chanzo.
====
Pia na wengi wamepata taarifa hizi kama nilivyozipata mimi ambao ni

French media ordered not to publish Macron's hacked emails

France's electoral commission has ordered media not to publish contents of Emmanuel Macron's leaked campaign emails to avoid influencing the election.It warned news outlets in France that journalists could face criminal charges for publishing or republishing the material, under laws that came into effect at midnight forbidding any commentary liable to affect the presidential race.
 
Back
Top Bottom